Air Tanzania’s Airbus A220 suffers engine failure

Air Tanzania’s Airbus A220 suffers engine failure

Duh...!, ama kweli ng'ombe wa masikini hazai!. Haya ndio madhara ya watu kujifanya tunajua!. Tuliuliza humu kwa nini tununue ndege kwa cash money wakati hata hao nchi matajiri wananunua kwa hire purchase?!.

Sababu pekee ni performance guarantee, kikiharibika kitu chochote, suppliers wana ki replace kwa gharama yao. Ukinunua kitu kwa cash, unalipa pesa kidogo, then kinakuwa chako owned by you 100%, manufacturer anajivua responsibility!. Just imagine the cost!. Juzi juzi niliona ndege yetu ilifanyiwa matengezo makubwa kule South, leo tena hili?!.

Niliwahi eleza humu, huku kukimbilia kununua midege mikubwa ya long haul bila a bussiness plan na kuja kuyarusha domestic routes, tunazitesa bure engines kwa kuzichosha na kuzichakaza!.

Sasa tusubirie taarifa rasmi.

P
 
Jet injini waingia shorwe au njiwa lazima lnjini iwe na itilafu. Ata wadudu wakubwa lazima rubani arudi kuitoa
 
Hizi ndege, mh!!!!!

Wahariri kazi kuandika habari za kusifia tu hasa kumsifu bwana yule, ila kuandika habari kama hizi, hawaandiki!!

Inawezekana kweli mnatishwa,lakini swali ni je,na kusifia mnalazimishwa?
Sasa Rais Magufuli anahudika na nini katika hiyo hitlafu ya ndege? Kwani yeye ametengeneza hizo ndege? Ina maana hiyo mitumba yenu ya magari kutoka Japan ikiharibika nyie ndiyo wa kulaumiwa?

Akili zenu ni za kitoto sana. Jaribu kubarehe Kwanza. Mnachukia mtu mpaka mnapoteza fahamu? Poleni sana masikini wa akili.

Ni wagonjwa nyie!
 
Hizi ndege, mh!!!!!

Wahariri kazi kuandika habari za kusifia tu hasa kumsifu bwana yule, ila kuandika habari kama hizi, hawaandiki!!

Inawezekana kweli mnatishwa,lakini swali ni je,na kusifia mnalazimishwa?
Hilo ni swali la msingi sana Mkuu wangu.
 
Sio jambo la ajabu kwa mashine yoyote kupata hitilafu hata kama ni mpya. Hata binadamu huugua. Nashauri serikali ijenge haraka uwanja mkubwa kabisa wa kimataifa Dodoma kwaajili ya dharura kama hizi. Kama alishifika Singida angeweza kutua Dodona ambapo ni karibu zaidi. Dodoma International Airport ijengwe haraka. Hongera rubani kwa kazi nzuri
 
We nawe ni mpuuzi. Wataalam wanashangaa kwa nini engine hizo zimekuwa zikifail, wewe usiye na ujuzi unasema ni kawaida.

Kiuhalisia ndege haistahili kuharibika ikiwa inafanya kazi. Kila part ina muda wake wa replacement, kabla ya muda ambao hiyo part inaweza kupata failure. Kwa hiyo kimsingi ndege haistahili kuharibika na wala replacement ya parts huwa haisubiri part ipate failure.
Kwanini una mwita mpuuzi? Hayo ni mawazo na mtizamo wake na halazimiki kuwaza kama wewe. Sijaona kitu cha kumwita mpuuzi kwenye post yake. Tuheshimu mawazo na mtizamo wa wengine hata kama hatupendezwi ikibidi kupinga tutumie lugha ya staha
 
Unawapongeza kwa lipi? Huo ni wajibu wa kazi yao, na wamefundishwa kukabili zaidi ya hilo.

Kwani pongezi utolewa kwa lipi, labda uelewi unapotekeleza majukumu yako kwa ufanisi ustahili kupongezwa ndiyo maana nimewapongeza. Pole sana kuumia kwa mie kuwapongeza. Na ninasema tena Hongera kwa Rubani wote. Na Mungu ahimidiwe
 
Mwewe wa jiwe amekata moto angani,hizi ndege hazina faida ziuzwe tu,mradi wa mwendokasi na elimu bure mmeshindwa mtaweza ndege??
FB_IMG_1569750560777.jpeg
 
Nahisi matatizo ya kiufundi. Kikubwa imetua salama, wafanye marekebisho vizuri kuepusha maafa yasije tokea na watu ndio wakazidisha maneno mengi zaid. Najua kuna watu kimoyo moyo waliomba ingeanguka na kulipuka pasipo kusahahu kulikuwa na watu mle... siasa mbaya sanaaa 😧😧
 
Nahisi matatizo ya kiufundi. Kikubwa imetua salama, wafanye marekebisho vizuri kuepusha maafa yasije tokea na watu ndio wakazidisha maneno mengi zaid. Najua kuna watu kimoyo moyo waliomba ingeanguka na kulipuka pasipo kusahahu kulikuwa na watu mle... siasa mbaya sanaaa
Wasiwasi ni ugonjwa, ukiona unazidi kamuone daktari.
 
Back
Top Bottom