Aina 10 za wanawake wanaopendwa na wanaume

Aina 10 za wanawake wanaopendwa na wanaume

1.Weupe
2. Wenye chura
3. Wavaa vimini na suruali tight Toto paja paja, kiuno kama dondola .
3. Wasiopenda kugawa vitu hovyo.
4. Wanaopenda kulisha wanaume zao.
Umesema ukweli mtupu maana wanaume wengi hupenda mwanamke ambaye akitembea naye barabarani watu wamsifu kuwa amechagua kifaa:::
Uzuri wa mwanamke uko katika imani yake pamoja na hofu yake juu ya MUNGU.
Mwanamke mchamungu umuhifadhi mumewe kwa zuri n.a. baya lake,daima huwa ana subira nafsini kwake.
Mungu atujaalie wanawake wachamungu lakini na sisi pia tukiwa wachamungu!!!
 
Wanaume wengi sasa hawajui wanachokitaka!
Unaweza ukawa na sifa zote hizo na wasikutake kisa huna Chura,

Hata mimi navutiwa na mwanamke mwenye chura.

Siku nikibalehe nikianza kutafuta mwenza nitamtafuta mwenye sifa alizotoa Joseverest plus awe na chura kidogo.
 
Ukitak kugawan majukumu 50 kw 50 nawe uwe tayar kuzaa kw uchungu...msigeuze maandiko. Mwanaume atakula kw jasho Mwanamke atazaa kw uchungu.kusaidiana kupo lkn sio umwangushie mwenzi wko 50 ...ptuuuh! Mbn na jikon utaingia nanguo utafua. Sio kw kizazi hiki bro utalizwa.
Ila tukifikia huko itakuwa raha sana yaani, mie nafua yeye anapiga deki, ninaondoka kwenda kwenye kikao cha kikoba huku nimeacha maagizo ya chakula gani ningependa kula siku hiyo. Huhuhuuuu!!

Eli79 ukuje useme kama unakubaliana na 50/50.
 
mabadilikooooooooooooooooooo lowasaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Zungusha ngumi kwanza!

Mwanaume kazaliwa ivo mkuu!
Ni nature tangu uumbaji nashangaa kadri mnavopingana na maandiko.
 
Habari za muda huu wanajukwaa, ni mara nyingine tunakutana katika jukwaa letu hili pendwa kwa ajili ya kujifunza.

Nikienda moja kwa moja kwenye mada, leo katika pitapita zangu huku na huko, nikakutana na hii mada na nimeileta hapa tujifunze..

Zifuatazo ni aina kumi za WANAWAKE wanaopendwa na WANAUME;


A. WENYE MSIMAMO
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, walio makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.

B. WAPENDA USAWA
Aina inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50

C. WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa niuwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwasita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani

D. MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida naraha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani

E. WAPENDA UWAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo nawapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.

F. WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina ‘naomba vocha’ au wapiga vibomu kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.

G. WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe nakazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi

H. MARIDADI(Warembo)
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano.

I. WANAORIDHIKA
Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke

J. WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana.“Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.”Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana..

Karibuni kwa majadiliano, kama una nyongeza/chochote unaweza ukaweka

45638f3d79ddbf09124edfd98c13ad5e.jpg


CREDITS TO: Lukemusicfactory and Dodoma Clan
Mimi vyote akose ila ajue kucontrol mambo ya sita×sita
 
Sure, mwanaume by nature yuko juu, na ndio anapenda iwe hivyo. Ndio maana hata pamoja na juhudi za kuhangaika na haki sawa bado haijaweza kufanikiwa maana we'll be fighting nature.

Ngumu mnoo kumwambia mwanaume eti "leo zamu yako kuosha vyombo, au wahi nyumbani ukapike, uogeshe na watoto mie nitachelewa kurudi leo"!!! Hiyo bado sanaaa, sijui ni mwanaume gani atakuelewa kwakweli.
Unaona sasa, kumbe hata wanawake wenyewe hawapendi hizi habari za usawa, nini wanaume tu.
 
Haki zibaki katika mambo ya msingi mfano, kujiendeleza kielimu, uhuru wa kutoa mawazo yako, kuhusiana na marafiki na zenye kufanana na hayo. Ila usawa hauwezi kuwa katika kila jambo. Hatuwezi kuwa sawa katika majukumu yote. Hata jinsi tunavyoingia kwenye mahusiano mpaka kwenye ndoa kuna utofauti mkubwa
Kweli usemalo mkuu ila kuna wengine hata katika hayo mambo ya msingi bado hawataki haki iwepo.
 
Unaona sasa, kumbe hata wanawake wenyewe hawapendi hizi habari za usawa, nini wanaume tu.
Ukichunguza ni kweli kabisa hata wanawake walio wengi hawapendi mwanaume wa "ndio/sawa mama". Sijui ni nature au ndivyo tulivyoaminishwa na jamii zetu. Mwanaume lazima awe juu, ndio maana wanaume wanaoapply 50/50 mara nyingi huwa wanadharaulika(sio na mkewe tu bali hata jamii inayomzunguka). Ni wanawake wachache na wanaume wachache wanaoweza kukubaliana na hilo.
 
Ukichunguza ni kweli kabisa hata wanawake walio wengi hawapendi mwanaume wa "ndio/sawa mama". Sijui ni nature au ndivyo tulivyoaminishwa na jamii zetu. Mwanaume lazima awe juu, ndio maana wanaume wanaoapply 50/50 mara nyingi huwa wanadharaulika(sio na mkewe tu bali hata jamii inayomzunguka). Ni wanawake wachache na wanaume wachache wanaoweza kukubaliana na hilo.
Kwa hiyo una support wanaume wa Tarime wanavyowafanyizia wake zao?
 
Back
Top Bottom