Maisha ya copy paste best, mambo mepesi
Angalia kesi ya hati desi upesi upesi usi face book tetesi
Haya maandiko kati dikodiko mwiko kama kejeli
Kama si burudiko liko liko ujiko wa kitapeli
Mambo ya vijarida vya inda ziso kawaida za ulimbwende
Kutoka kwenye marinda ya mida hii utamu ka peremende
Majira hadhira, madhila hasira zamu za kereng'ende
Kuzila dira iso majira wala ujira, ife kifo cha mende
Ni utani wa ughani, maudhi ya utunzi
Ni kama mpagani umpe shauzi ya jamat ukufunzi
Ni kuweka pana kwenye finyu, utaharibu mambo
Utakana sana mnadhimu mhadimu, kwa kujaribu jigambo
Mtu kwao, hata kama ubao,iga ufe
Mitandao kibao inaiba kwa vitufe
Bonyeza hapa, fanya duara bapa
Halafu wajazie mafala kama we Ben Mkapa
Wasikilize, wameamua kung'amua?
Au umewaua kujua kwa ubua?
Wachote kama maji ya bomba, si NUWA wala mvua
Waondoe akili adili kwa nguvu za bamvua
Maisha kufikirika kuliko tamthiliya
Wengi watamwagika watabaki wanalia...