we dhubutu,yanga ni time ya kualikwa kienyeji kama simba,yanga heshima kaka. inashikiliwa na matajiri wewe.
mkuu kwa hili najuta kuwa simba, ila poa tu najua ligi ikianza watanipoza
we dhubutu,yanga ni time ya kualikwa kienyeji kama simba,yanga heshima kaka. inashikiliwa na matajiri wewe.
Kwanza nimpe pongezi na hongera za dhati kamanda Dr Slaa na timu yake kwa kuzidi kupasua anga na kueneza elimu ya uraia. Jana walipiga mikutano mikubwa mkoani wa Tanga kwa kuanzia wilayani na baadae kumalizia Tanga mjini.
Pili nimpe pole hammy D aka Mwigulu Nchemba aliye wahi kuja jukwaani na kukimbilia kusema kuwa Chadema imekosa watu kabla hata ya mkutano kumbe alikuwa anajua kuwa mpira wa bure utawafanya wana Iramba kwenda kuwaona Simba na kuacha kupata darasa la uraia kutoka kwa Dr wa ukweli.
Wazo la mabadiliko linapo kuwa limefika kichwani, hata zingekuja timu gani kubwa kutoka sayari yoyote! Timu hizo haziwezi kuzuia wazo la mabadiliko vichwani mwa wananchi wanao yataka mabadiliko.
Sio timu ya Simba tu ambayo Mwigulu ameweza kuitumia lakini hata angetumia majeshi bado angekwama, kwa sababu historia ya dunia inaonyesha kuwa hakuna jeshi kubwa lenye nguvu duniani lililo wahi kuzuia wazo la mabadiliko lililo kuwa tayari limejiri vichwani mwa wananchi na kufanikiwa.
Mwigulu bado angeendelea kushindwa tu hata angetumia majeshi ya Misri! Kuna jamaa yangu mmoja alisema "Mwigulu ni mbunge wa muda aliye bakiza miaka 2, mbunge wa jimbo yuko chuo kikuu akinoa mbongo za vijana". Sikutaka kumuuliza kuwa ni nani maana unaye nisoma tayari unamjua.
Tatizo ni Julio Kihwelo na Aden Rage!Nao simba nawalaumu kwa kukubali mwaliko wa kijinga kama huo.
Sina shaka huyu jamaa amekuwa kama zuzu kwani sasa naamini kuwa hata lile jina sekondari ametumia jina la msukuma na thats why hana akili.Ndugu zangu wana JF, Kama ilivoelekezwa hapo awali, Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Wilbroad Slaa anaendelea na ziara yake nchini. Leo hii, Dr. Wilbroad Slaa akiambatana na ujumbe wake wameanza ziara ya kichama Mkoani Singida. Awali, Dr. Slaa alipanga kufanya mkutano Kiomboi leo jioni. Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa Iramba magharibi, Mwigulu Nchema aliialika timu ya Simba kucheza na timu ya Kiomboi bila kiingilio. Hii ilikuwa ni strategy ya makusudi ya kupunguza mahudhurio katika mkutano wa CHADEMA. Lakini pamoja na mbinu hiyo mufilisi, mkutano wa CHADEMA ulioanza majira ya saa nane Mchana ulifurika kupita kawaida, na wananchi walibaki katika hali ya utulivu mpaka pale Dr. Slaa alipomaliza kuhutubia na kupanda Helikopta kuelekea Singida Mjini kwenye mkutano mwingine. Katika mechi hiyo ambayo ilichelewa sana kuanza kutokana na gari waliyokuwa wamepanda timu ya Simba kupata matatizo ya kiufundi njiani ambayo imemalizika hivi punde, Simba S.C ilifanikiwa kuwakung'uta mahasimu wao kwa mabao matatu pasipo majibu. Ndugu yangu Mwigulu, siku baada ya siku mambo yanazidi kukuendea vibaya. Huoni umuhimu wa kujirekebisha na kutimiza majukumu yako ya kibunge? Hizi gharama za kuwaleta Simba S.C hapa Kiomboi zingeweza kuwaleta Kindai Shooters au Magic F.C kutoka pale Singida Mjini na bado zikatosha kuwasaidia wananchi wa Urughu pale wanaojifungulia majumbani mpaka leo kwa kukosa kituo cha afya.. Badala yake, ulijitafutia utukufu kwa kuileta Simba yenye jina na uwezo mkubwa, sio ili kuwaburudisha wananchi au ili kujipima kimchezo, bali ili uizuie CHADEMA. Sina shaka mfululizo wa kushindwa kwako kutakufundisha jambo. "Akili ndogo vs. Akili kubwa".. Naomba kuwasilisha.
siasa tena kwenye mpira duuh wanasimba tunahujumiwa
Acha hizo Rangi na tabia za watu wapi na wapi ?yanga sehemu Kama hizo hawapenyi wapo kimaadili zaidi Ndio Maana Azam Tv wanahaha kuwabembeleza watie sahihi kwani yanga hawaburuzwi kirahisi ! Simba wameingizwa mkenge wanajuta sasadah timu bora na kubwa kama simba kdhalilishwa namna hii haifai.
bora ingekuwa yanga wavaa mavazi ya rangi ya ccm
Yanga jana wametupa raha sana tumechapa Azam. Wakati Simba wameenda kucheza na timu ya kijiji Kiomboi
Kwanza ilikuwaje Mwigulu aalike timu ya Simba ilihali yeye ni shabiki wa Yanga? Au Simba ndiyo timu cheap sana?
dah timu bora na kubwa kama simba kdhalilishwa namna hii haifai.
bora ingekuwa yanga wavaa mavazi ya rangi ya ccm
Mkuu umesahau mwenyekiti wa simba anatokea chama gani!!!
Mtakodisha sana Simba na itabidi muwalete hata Manchester kwa sababu mikutano itakuwa zaidi ya 170 (angalau 10 kila kata) kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani. Itabidi mkubali siasa za kistaraabu na za akili. Siasa za kijinga na fitina hazina nafasi katika karne ya leo. Poleni sana.
Dr Bana!
Mwenyekiti mwenyewe wa simba ndiyo walewalei?Nao simba nawalaumu kwa kukubali mwaliko wa kijinga kama huo.