LHRC: Hakuna anayewajibishwa licha ya Mgawo wa Umeme kuathiri Watanzania wengi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Tamko la LHRC kuhusu hali ya Mgomo wa Umeme nchini la February 19, 2024 limeainisha hoja zifuatazo

Hoja 5 za LHRC kuhusu Mgawo wa Umeme Nchini

1. Serikali imekuwa inatoa ahadi hewa kuwa tatizo la Umeme litaisha toka kipindi cha Mradi wa gesi 2012 hadi leo 2024

2. Kukatika kwa Umeme kunaathiri Haki za Kikatiba ikiwemo
-Ibara ya 22 na 23 (Haki ya Kufanya kazi na kujipatia Ujira)
-Ibara ya 14 (Haki ya Uhai kwa Kupata Huduma Bora za Afya)
-Ibara ya 18 (Haki ya Kupokea na kutoa taarifa)

3. Tatizo linajirudia licha ya Vyanzo mbalimbali vya Uzalishaji ikiwemo Gesi asilia inayozalishwa Mtwara na Lindi (Songo songo, Mnazibay, Msimbati na Madima)

4. Mbali na Changamoto Watanzania wanazopitia kutokana na Mgawo wa Umeme hakuna anayewajibishwa

5. Bunge limeshindwa kusimamia kuhakikisha Serikali inatimiza ahadi ya kupatikana kwa Umeme Machi 2024, badala yake limeongeza muda hadi Juni 2024

Pamoja na hoja hizo wametoa mapendekezo yafuatayo ikiwemo Serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana ndani ya muda mfupi

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetakiwa kupanga ratiba ya matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kuzingatia sayansi ya mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kutoa taarifa zisizo na Mkanganyiko wa Wananchi kuhusu Mgawo wa Umeme

Pia Serikali imetakiwa kuongeza uwekezaji katika vyanzo vya uzalishaji wa nishati ya umeme isiathirika kirahisi na mabadiliko ya hali ya hewa ili kuongeza upatikanaji endelevu wa umeme
 
Attachments

  • KUKOSEKANA_KWA_UMEME_NCHINI_NA_UHUSIANO_WAKE_NA_HAKI_ZA_BINADAMU.pdf
    271.4 KB · Views: 1
Kwa mfumo huu wa ccm bado wananchi wataendeleq kuumia, na shida ya watanzania hawajui haki zao, na waliobaki wamebaki kuwa machawa kama lucas mwashambwa! Wewe unategemeq kuna mtu wa kuitisha serikali, ikifika wakati wa uchaguzi wanagawa vipande vya sabuni, na kofia na kubebwa kwenye malori, uchaguzi ukiisha matatizo yanaendelea, haya matatizo yote yamechangiwa na katiba mbovu ambayo imepelekea kupata viongozi wasiochaguliwa na wananchi, wewe unategemea mbuge aliyepita kwa wizi wa kura au kwa mgongo wa mtu akutete wewe mwananchi??? Kikubwa ngoja tuendelee kuisoma namba na kwa kuwa wapinzani walituchelewesha ngoja tuendelee kuumia mpaka siku wananchi watakapopata ufahamu kuwa CCM kwa sasa ilishachoka!!
 
Inasikitisha ila yana mwisho hayo. Yule.Bibi anaipeleka nchi korongoni. Tukilia sana, yeye asikiaye maombi atatenda jambo
 
Tamko la LHRC kuhusu hali ya Mgomo wa Umeme nchini la February 19, 2024 limeainisha hoja zifuatazo

Hoja 5 za LHRC kuhusu Mgawo wa Umeme Nchini

1. Serikali imekuwa inatoa ahadi hewa kuwa tatizo la Umeme litaisha toka kipindi cha Mradi wa gesi 2012 hadi leo 2024

2. Kukatika kwa Umeme kunaathiri Haki za Kikatiba ikiwemo
-Ibara ya 22 na 23 (Haki ya Kufanya kazi na kujipatia Ujira)
-Ibara ya 14 (Haki ya Uhai kwa Kupata Huduma Bora za Afya)
-Ibara ya 18 (Haki ya Kupokea na kutoa taarifa)

3. Tatizo linajirudia licha ya Vyanzo mbalimbali vya Uzalishaji ikiwemo Gesi asilia inayozalishwa Mtwara na Lindi (Songo songo, Mnazibay, Msimbati na Madima)

4. Mbali na Changamoto Watanzania wanazopitia kutokana na Mgawo wa Umeme hakuna anayewajibishwa

5. Bunge limeshindwa kusimamia kuhakikisha Serikali inatimiza ahadi ya kupatikana kwa Umeme Machi 2024, badala yake limeongeza muda hadi Juni 2024

Pamoja na hoja hizo wametoa mapendekezo yafuatayo ikiwemo Serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana ndani ya muda mfupi

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetakiwa kupanga ratiba ya matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kuzingatia sayansi ya mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kutoa taarifa zisizo na Mkanganyiko wa Wananchi kuhusu Mgawo wa Umeme

Pia Serikali imetakiwa kuongeza uwekezaji katika vyanzo vya uzalishaji wa nishati ya umeme isiathirika kirahisi na mabadiliko ya hali ya hewa ili kuongeza upatikanaji endelevu wa umeme

Bado tunakomaa na sanamu la Nyerere kwanza
 
kelele za chura
 
Mama Kizimkazi kazi yake ni kuzurula tu, mambo ya kuwajibishana ni kutingisha meza ya watu.
 
Dah! Mafisadi wametushika pabaya. Hapo watakuwa wanataka kuiwasha tu ile mitambo yao chakavu ya IPTL, au Mmarekani atakuwa amewakomalia wairejeshe Richmond aka Dowans aka Symbion ili azitafune tena hela zetu.
 
Tamko la LHRC kuhusu hali ya Mgomo wa Umeme nchini la February 19, 2024 limeainisha hoja zifuatazo

Hoja 5 za LHRC kuhusu Mgawo wa Umeme Nchini

1. Serikali imekuwa inatoa ahadi hewa kuwa tatizo la Umeme litaisha toka kipindi cha Mradi wa gesi 2012 hadi leo 2024

2. Kukatika kwa Umeme kunaathiri Haki za Kikatiba ikiwemo
-Ibara ya 22 na 23 (Haki ya Kufanya kazi na kujipatia Ujira)
-Ibara ya 14 (Haki ya Uhai kwa Kupata Huduma Bora za Afya)
-Ibara ya 18 (Haki ya Kupokea na kutoa taarifa)

3. Tatizo linajirudia licha ya Vyanzo mbalimbali vya Uzalishaji ikiwemo Gesi asilia inayozalishwa Mtwara na Lindi (Songo songo, Mnazibay, Msimbati na Madima)

4. Mbali na Changamoto Watanzania wanazopitia kutokana na Mgawo wa Umeme hakuna anayewajibishwa

5. Bunge limeshindwa kusimamia kuhakikisha Serikali inatimiza ahadi ya kupatikana kwa Umeme Machi 2024, badala yake limeongeza muda hadi Juni 2024

Pamoja na hoja hizo wametoa mapendekezo yafuatayo ikiwemo Serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana ndani ya muda mfupi

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetakiwa kupanga ratiba ya matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kuzingatia sayansi ya mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kutoa taarifa zisizo na Mkanganyiko wa Wananchi kuhusu Mgawo wa Umeme

Pia Serikali imetakiwa kuongeza uwekezaji katika vyanzo vya uzalishaji wa nishati ya umeme isiathirika kirahisi na mabadiliko ya hali ya hewa ili kuongeza upatikanaji endelevu wa umeme
Huyu mama nchi imemshinda
 
TAMKO ni sawa lakini ,waende mbali zaidi kwa kuwaongoza Watanganyika kwenda kufungua KESI Mahakamani ili kuiomba MAHAkAMA itamke kwamba;

i.TANESCO imeshindwa kazi ya kuzalisha na kusambaza umeme,hivyo ifungiwe

ii.Viongozi wake,wahukumiwe kwa KUHUJUMU Uchumi

iii.Iamuru Serikali yenye TANESCO kuwalipa wateja waTanganyika wote FIDIA
 
Sasa kama raisi na serikali yake wameshindwa kutatua jambo dogo kabisa la ukosefu wa sukari unadhani ni jambo gani wanaweza kufanya 🤔🤔
Kama Watanzania tungekua ni watu makini hili la umeme lilipaswa kuiondoa serikali ya ccm daima kwenye madaraka, hata huo mwezi wa sita watakuja kudanganya kwa mara nyingine tena huku sisi tukiendelea kulia machozi ya samaki
 
Back
Top Bottom