Afisa Mtendaji Kata ya Lulembela anatisha na kulazimisha wananchi na watumishi kutoa mchango

Mtz kwanza

Member
Sep 5, 2021
7
45
Afisa Mtendaji kata ya Lulembela, wilaya ya Mbogwe, mkoa wa Geita amekuwa Mungu mtu kwa kutisha na kulazimisha wananchi na watumishi kutoa mchango wa maendeleo bila staha na kuzingatia utu wa mtu.

Anamtumia balozi wa nyumba kumi anayeitwa Benard Gwanguru ambaye amekuwa akiambatana na mgambo muda wote
kuwatisha na kuwalazimisha wananchi na watumishi kuchangia mchango kiasi cha elfu kumi na mbili (12000/=) kwa lazima.

Kinachosikitisha ni kwamba hakuna maelezo yanayojitosheleza, wala kikao kilichoitishwa na afisa mtendaji huyu na balozi huyu kuwaeleza wananchi na watumishi katika vituo vyao vya kazi kuhusu mchango huo, zaidi afisa mtendaji huyo na balozi huyo wakiulizwa wanasema ni agizo linalohitaji wananchi na watumishi wachangie mchango huo bila kufafanua agizo hilo limetoka wapi.

Pia mchango unaolazimishwa unabagua watumishi ambapo watumishi wanaoishi katika nyumba za serikali (quaters) hawapaswi kuchangia wakati watumishi wanaoishi uraiani wanalazimishwa kuchangia mchango huo, swali ambalo ukiwauliza kwa nini watumishi wengine wachangie na wengine wasichangie afisa mtendaji huyo na balozi huyo hawana majibu.

Watumishi wanaohoji mchango huo huandikiwa wito "Summons" na afisa mtendaji huyo akiwataka kuhudhuria katika ofisi ya kata ya Lulembela kwa kosa linaloandikwa "KUPINGA MAENDELEO" ambapo kwa waliowahi kuitika wito huo hulazimishwa kuchanga mchango huo kwa kufungiwa na kuteswa katika ofisi ya afisa mtendaji huyo.

Kwa upande wa watumishi hali hii inaathiri molali yao ya utendaji kazi ikiwemo kupunguza mahudhurio ya watumishi katika vituo vyao vya kazi kwa kuhofia kukamatwa.

Dhamira ya Serikali ya Mheshimiwa Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan imejikita katika kuwapunguzia wananchi na watumishi mzigo kwa kutengeneza mazingira rafiki ya ulipaji kodi bila vitisho na kuathiri utendaji kazi wa wananchi na watumishi. Lakini kwa huyu afisa mtendaji kata ya Lulembela ni tofauti kabisa.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu Waziri wa Tamisemi alitoa ufafanuzi juu ya uchangishaji michango ya maendeleo alipotembelea wilaya ya Sengerema August mwaka huu lakini kinachoonekana kwa afisa mtendaji na huyu balozi wa nyumba kumi hawakuelewa alichosema mheshimiwa waziri kutowalazimisha wananchi kuchangia michango ya maendeleo.

Wananchi na watumishi wa kata ya Lulembela tunaomba mamlaka zinazohusika zifuatilie suala hili la afisa mtendaji kata ya Lulembela na balozi wa nyumba kumi aliyetajwa kulazimisha wananchi na watumishi kuchangia mchango bila kuwaelewesha ili kuondoa usumbufu na taharuki kwa wananchi na watumishi wa kata hii.
 
juma mpemba

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
2,969
2,000
Huko wamejaa watu wajinga...Yani eti mtu mmoja ndo anasumbua ivo Tena kudai michango batili....I can feel your fucking chest pain..but your ignorance is overtaking your ego
 
mkupuo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,465
2,000
Balozi wa nyumba 10 umemtaja jina lakini mtendaji wa kata umemuacha kumtaja jina, kwa nini?
 
Mapank

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,421
2,000
Afisa Mtendaji kata ya Lulembela, wilaya ya Mbogwe, mkoa wa Geita amekuwa Mungu mtu kwa kutisha na kulazimisha wananchi na watumishi kutoa mchango wa maendeleo bila staha na kuzingatia utu wa mtu.

Anamtumia balozi wa nyumba kumi anayeitwa Benard Gwanguru ambaye amekuwa akiambatana na mgambo muda wote
kuwatisha na kuwalazimisha wananchi na watumishi kuchangia mchango kiasi cha elfu kumi na mbili (12000/=) kwa lazima.

Kinachosikitisha ni kwamba hakuna maelezo yanayojitosheleza, wala kikao kilichoitishwa na afisa mtendaji huyu na balozi huyu kuwaeleza wananchi na watumishi katika vituo vyao vya kazi kuhusu mchango huo, zaidi afisa mtendaji huyo na balozi huyo wakiulizwa wanasema ni agizo linalohitaji wananchi na watumishi wachangie mchango huo bila kufafanua agizo hilo limetoka wapi.

Pia mchango unaolazimishwa unabagua watumishi ambapo watumishi wanaoishi katika nyumba za serikali (quaters) hawapaswi kuchangia wakati watumishi wanaoishi uraiani wanalazimishwa kuchangia mchango huo, swali ambalo ukiwauliza kwa nini watumishi wengine wachangie na wengine wasichangie afisa mtendaji huyo na balozi huyo hawana majibu.

Watumishi wanaohoji mchango huo huandikiwa wito "Summons" na afisa mtendaji huyo akiwataka kuhudhuria katika ofisi ya kata ya Lulembela kwa kosa linaloandikwa "KUPINGA MAENDELEO" ambapo kwa waliowahi kuitika wito huo hulazimishwa kuchanga mchango huo kwa kufungiwa na kuteswa katika ofisi ya afisa mtendaji huyo.

Kwa upande wa watumishi hali hii inaathiri molali yao ya utendaji kazi ikiwemo kupunguza mahudhurio ya watumishi katika vituo vyao vya kazi kwa kuhofia kukamatwa.

Dhamira ya Serikali ya Mheshimiwa Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan imejikita katika kuwapunguzia wananchi na watumishi mzigo kwa kutengeneza mazingira rafiki ya ulipaji kodi bila vitisho na kuathiri utendaji kazi wa wananchi na watumishi. Lakini kwa huyu afisa mtendaji kata ya Lulembela ni tofauti kabisa.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu Waziri wa Tamisemi alitoa ufafanuzi juu ya uchangishaji michango ya maendeleo alipotembelea wilaya ya Sengerema August mwaka huu lakini kinachoonekana kwa afisa mtendaji na huyu balozi wa nyumba kumi hawakuelewa alichosema mheshimiwa waziri kutowalazimisha wananchi kuchangia michango ya maendeleo.

Wananchi na watumishi wa kata ya Lulembela tunaomba mamlaka zinazohusika zifuatilie suala hili la afisa mtendaji kata ya Lulembela na balozi wa nyumba kumi aliyetajwa kulazimisha wananchi na watumishi kuchangia mchango bila kuwaelewesha ili kuondoa usumbufu na taharuki kwa wananchi na watumishi wa kata hii.
Wacha awapige pesa, mmekusanya mpunga wa kutosha msimu huu
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
8,499

Hakuna Diwani,mkuu wa Wilaya huko?
 
Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,425
2,000
Hii Habari umeileta kishabiki upande mmoja, mtendaji kata hawezi kuamka tu akachangisha michango bila vikao na michango ieleweke inafanya kazi gani? Maeneo mengi ya nchi watendaji wanaandaa madarasa kwa ajili ya kupokea wanafunzi mwakani, lakini pia walio na maboma wanapewa kipaumbele.
Umesema kwamba watumishi waliokambini hawabughudhiwa huenda Kuna makubaliano ya kulipa kwa Kaya ikiwemo yako, lakini 12000 sio pesa nyingi kama unajua inaenda kusaidia kitu
Tuache majungu.
 
nkomelo

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
214
225

Yaani umeona hili ni jukwaa la kusambaza majungu yako. Kila ndama anyonye kwa mama yake.
 
Bzimana

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
499
250
changia maendeleo, acha unafiki, kama mtendaji kata anachangisha michango kinyume na makubaliano si umuone boss wake, acha unafiki.... naludia tena acha unafiki, acha unafiki.
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
5,067
2,000
Acheni kulialia,kwani au mlisema wapinzani wana wacheleweshea kupata maendeleo

tulieni dawa iwaingie Tena wachangishe na mifugo, mfano ukiwa na ng'ombe watano au mbuzi inatakiwa utowe tozo ya mmoja nk
 
Mtz kwanza

Member
Sep 5, 2021
7
45
Hii Habari umeileta kishabiki upande mmoja, mtendaji kata hawezi kuamka tu akachangisha michango bila vikao na michango ieleweke inafanya kazi gani? Maeneo mengi ya nchi watendaji wanaandaa madarasa kwa ajili ya kupokea wanafunzi mwakani, lakini pia walio na maboma wanapewa kipaumbele.
Umesema kwamba watumishi waliokambini hawabughudhiwa huenda Kuna makubaliano ya kulipa kwa Kaya ikiwemo yako, lakini 12000 sio pesa nyingi kama unajua inaenda kusaidia kitu
Tuache majungu.
Siyo kishabiki ndugu, watumishi wanakatwa kodi kwenye mishahara yao kila mwezi, huo ni MCHANGO tosha kwa nchi na jamii yao, mtendaji alipaswa kuwa mstari wa mbele kupigania masilahi ya watumishi badala ya kuwakandamiza. Ukifikiri vizuri utaelewa.
 
Mtz kwanza

Member
Sep 5, 2021
7
45
Yaani umeona hili ni jukwaa la kusambaza majungu yako. Kila ndama anyonye kwa mama yake.
Hayo siyo majungu ni hali halisi. Mtendaji na balozi wake walipaswa kuelimisha wananchi kuhusu mchango huo na si kutumia nguvu. Hata ukusanyaji kodi kwa ngazi ya taifa ungekuwa wa kutumia nguvu namna hiyo hali isingekuwa nzuri
 
Mtz kwanza

Member
Sep 5, 2021
7
45
changia maendeleo, acha unafiki, kama mtendaji kata anachangisha michango kinyume na makubaliano si umuone boss wake, acha unafiki.... naludia tena acha unafiki, acha unafiki.
Si unafiki, namna inayotumika kudai michango si ya kidemokrasia, ni ya unyanyasaji na ukandamizaji. Ungeelewa ni kiasi gani cha Kodi watumishi hulipa kila mwezi usingeandika haya ndugu.
 
BARCA ON

Senior Member
Nov 26, 2011
192
250
Si unafiki, namna inayotumika kudai michango si ya kidemokrasia, ni ya unyanyasaji na ukandamizaji. Ungeelewa ni kiasi gani cha Kodi watumishi hulipa kila mwezi usingeandika haya ndugu.
Ndugu yangu bila shaka wewe ni mwalimu.
Mtendaji kata hawezi amka usingizini akanza kuchangisha fedha bila vikao kuridhia mchango na matumizi yake.

Pili kama unaona haki hazifuatwi katika kudai michango kuna mamlka za kupeleka malalamiko yako.

Mwisho punguza kuandika kwa kuegemea upande mmoja. Unapoandaa stori jaribu kubalance.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom