Muheza: Wanakijiji wamjeruhi Afisa Kilimo na kuchoma gari lake wakimtuhumu kushindwa kusimamia maslahi yao

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Wananchi wa Kijiji cha Kambai, kilichopo Kata ya Kwezitu, Wilaya ya Muheza, Mkoa wa Tanga, wamewasha moto gari la Afisa Kilimo wa Kata ya Tongwe jirani, aina ya Suzuki, na kumjeruhi.

Wanaoshutumu afisa huyo wanadai kwamba ameshindwa kusimamia maslahi ya wananchi, hivyo kuruhusu wawekezaji kupewa eneo la zaidi ya ekari 500 bila kufanyika kwa tathmini ya kina wala kuwashirikisha wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Zainab Abdallah, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Mara tu baada ya kupokea taarifa, alilazimika kufika katika kijiji hicho ili kufanya mkutano na wananchi kwa lengo la kutafuta suluhisho la suala hilo.

"Kumekuwepo na eneo la hekta elfu tatu lenye hati kwa zaidi ya miaka 28 ambalo halijatumiwa kwa maendeleo. Mwaka 2020/2021, mwekezaji wa kwanza alipewa ekari 500 bila kufanyika kwa tathmini ya kina kuona kiwango cha uvamizi kwenye eneo hilo. Vivyo hivyo, mwaka jana, 2023, wawekezaji wanne waliopatikana pia hawakufanyiwa tathmini ya kina," alieleza.

Afisa Kilimo huyo amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Muheza akipokea matibabu, huku baadhi ya watu waliohusika katika kuchoma gari hilo wakishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano.
 
Welldone uzi mzuri kutokea baada ya muda mrefu,push back na within short time DC amekuja kuwasikiliza,hakuna kulalama humu
 
Back
Top Bottom