AFCON 2023 imefana sana kwa sababu ya maamuzi ya haki ya waamuzi waliochezesha mechi zake

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,143
7,909
Watu wengi wamesifia AFCON ya 2023 kwa ushindani ulioonyeshwa na timu nyingi na matokeo yasiyotabirika yaliyofanya mashindano kuwa ya ushindani zaidi.

Pamoja na sababu nyingine kadhaa ikiwemo ongezeko la wachezaji wenye viwango vikubwa kwa timu nyingi, kama kuna jambo moja ambalo limekuwa sababu kuu ya mafanikio yaliyoonekana katika AFCON 2023 kule Ivory Coast basi ni maamuzi ya haki waliyokuwa wanafanya waamuzi viwanjani.

Ukiacha uwepo wa VAR ambazo nazo ziliongeza umakini zaidi, ila hata waamuzi wenyewe walikuwa na weledi mkubwa sana katika maamuzi yao. Haikujalisha status ya timu au ya mchezaji, kwa kiasi kikubwa haki ilikuwa inazingatiwa. Ilikuwa ni nadra sana na sina kumbukumbu ya mechi ambayo unaona hapa kuna timu inabebwa.

Na CAF wameenda mbali zaidi kuhakikisha haki imetamalaki viwanjani. Ilipoonekana kuna maamuzi ambayo yalifanyika au hayakufanyika wakati ushahidi ulionekana dhahiri, tena wakiwa na msaada wa VAR, basi CAF hawakusita kuwachukulia hatua waamuzi husika. Mfano mmoja wapo ni ile rafu aliyofanya Sadio Mane ambayo inaonyesha ingestahili kadi nyekundu katika mechi ya Senegal vs Ivory Coast, halafu mwamuzi akaikaushia. Baada ya mechi ile, yule mwamuzi aliondolewa kwenye mashindano.

Kuna maeneo mengi ambayo bado tunapwaya mnoo katika ligi ya ndani yanayopunguza haki na usawa kwa timu shiriki na hivyo kupunguza quality ya ligi lakini hili la weledi wa waamuzi ni jambo la msingi sana.
 
Mmeona hadi Mourinho karudia maneno yangu, yaani katembea mule mule

Screen Shot 2024-02-12 at 12.16.56 PM.png
 
Back
Top Bottom