Tumeanza kwenda AFCON toka mwaka 1980, bado tunajifunza nini?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,143
7,912
Hivi wadau, mnajua Tanzania ilikwenda AFCON kwa mara ya kwanza mwaka 1980 wakati huo timu zinazofuzu huko ni 8 tu?

Yaani kwa lugha nyingine, tungekaza sasa hivi tungekuwa moja ya magwiji wa mashindano haya na hata ndoo labda tungekuwa tumeshawahi kubeba. Hawa watu wanaosema bado tunajifunza wanajua hili?

Inashangaza leo tunaonekana ni timu changa na dhaifu wakati tumewahi kushiriki mashindano haya kipindi baadhi ya nchi nyingine zinazosumbua sasa hivi hazijapata uhuru.

Cape Verde na Angola ambao leo wanaonekana tishio na wana timu za kubeba ndoo walikuwa na miaka 5 tu. Namibia walikuwa hawajapata hata uhuru.

Ivory Coast ambao juzi juzi tu walikuwa na vita kubwa iliyoigawa nchi katika vipande viwili leo wana uwezo wa kujenga viwanja vya viwango hivi tunavyoviona AFCON halafu wala hawaringi. Sisi mpaka leo vita na Idi Amin bado ni sababu za kukwama kwetu.

Inafikirisha sana.
 
Aliyesema tunajifunza ni nani?
Kuanzia viongozi, kocha, wachaa mbuzi hadi baadhi ya mashabiki wamesema hivyo. Tunashangilia point mbili ambazo imetuchukua miaka 44 kuzipata.
 
Back
Top Bottom