Afanyeje naye anampenda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afanyeje naye anampenda?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ambassador, Jan 21, 2010.

 1. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wadau, kuna issue serious kidogo toka kwa best yangu mmoja. Ameanza kazi katika shirika fulani na hapo katika ofisi yake mpya amebahatika kumkuta dada mmoja mrembo sana ambaye ana vigezo vyote anavyovipenda mshikaji wangu. Akiwa katika kujizoeza na yule dada wafanyakazi wenzake wamemstua kwamba hapo anacheza na moto kwani huyo binti ni muathirika. Anasema amefuatilia stori za huyo dada kwa watu tofauti tofauti na anapata the same story.

  Mshikaji kapagawa na anajipa moyo kwamba kwa kuwa ameshafahamu status ya huyo dada anaona bora endelee nae tu na atahakikisha anajilinda vema asiathirike.

  Nimeshindwa kumshauri la maana huyu mshikaji wangiu kwani nilipomuuliza kama ana uhakika na analolifaya amesema "kwani mtu mwenye UKIMWI hana haki ya kuwa na mpenzi?" Nikaishia kumwambia atafakari kwa makini na awe mwangalifu maana "mambo ya rohoni" ni mtu mwenyewe anayependa. Sio baadae aanza kulaumu watu "mlinishauri vibaya".

  Mwenzetu kafika bei, wadau mnasemaje?
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hapo ushauri wa kumpa huyu rafiki yako mwambie waende wakapime hosp. tofauti tofauti ila wakubaliane kwanza maana naona jamaa hata ndoano hajarusha binti akikubali asikimbilie kumega waende mguu kwa mguu kwa Dr. wapime afya zao.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  The best thing ni kwamba ameambiwa na ameshaelewa kuwa huyo dada ana shida hiyo, so ataamua chochote kwa risk yake(nadhani yuko above 18) na kwa hiyo ni mtu rational, na ana akili timamu!

  Otherwise huwezi kumshauri tofauti na akili yake inavyomtuma...never!
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mambo yanayo epukika ni bora n'tu kumwambia mapema maana tutaanza kupoteza muda kwa kuanza kumjenga kisaikolojia n.k
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  HEHEHE!
  nashukuru mungu sina mapenzi ya staili hiyo
  ....THUG LOVING.....ndio mwendo wangu!
   
 6. N

  Nanu JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapo dawa wakapime pamoja kabla ya kutumikiana!!!!!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Anajidai inzi kufia kwenye kidonda eenh, hahaha wakapime kwanza awe na uhakika 100%, itamwezesha kujua namna ya kujikinga
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Akiendelea kulilia kummmega mwambie atumie condom ndo solution pekee
   
 9. E

  Edo JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jamani huyu kaisha ambiwa demu mgonjwa , akapime nini tena?Sikio la kufa hilo.....
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  Kama amempenda kikweli waende tu wakapime wajue status zao simple ..lakini binadamu siku zote hatupendani kabisa mtu mmoja anaweza kukuzushia una ngoma au baya lolote analojisikia kisa umemtosa /mmegombana na habari ikasambaa dunia nzima na ikakuharibia sifa yako
  Ingawa sometimez wanasema lisemwalo lipo
  Hao watu wamempima kwa macho au wana kithibitisho gani juu ya madai hayo??
   
 11. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Halafu huyo jamaa naye kha! Yaani umeanza kazi ofisini umekuta msichana mrembo wewe tayari unamtaka, ina maana wanaume wenzio hapo ofisini sio marijali?

  Mwambie aende taratibu bwana !!! :)
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  chukulia uko chumbani na mwanamke, mwataka fanya mapenzi (au ngono-call it whatever you want) kisha akakuambia, nimeathirika!!!!!!. Unaweza kuendelea?

  utakalo fikiria ndilo la kumpa huyo jamaa yako.

  Jibu langu ni hili, ikiwa jamaa yako hajaathirika, aachane na huyo mwanamke, PERIOD!!!!!. But ikiwa naye ni mwathirika, he should seek counselling kwanza.

  And he is very funny ameanza kazi na kupenda hapo hapo ofisini? Anajua risks za mapenzi na workmate? na akiacha hapo akaanza kazi sehemu nyingine.....nako atapenda mwingine?
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  lakini kuna uwezekano ni maneno ya waswahili tu kama kuna mtu alishamthibitishia jamaa kuwa aliona majibu ya vipimo vya huyo dada sawa...otherwise wakapime
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  siku akinogewa ? wakapime tu na binti akigoma kupima labda itakuwa kweli
   
 15. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wakapime mara 2 hadi 3 kabla hawajafanya kitu.. La sivyo anajichimbia kaburi.. Wengi wameondoka kwa ubishi kama wake..
   
 16. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Is that guy serious???. One thing they may be only rumours! coz hamna aliyempima! au kuna mgonjwa mwenzie walikutana klinic akaamua kueneza habari.
  Sasa unafikiri kama dada anajua kuwa tayari ashakwama atakubali kwenda kupima.

  Swali kwa fidel
  Ukaambiwa leo vivian ni muadhirika 100% then take a condom and sleep with her, will you dare????
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hehehehe atumie zana kama amependa ua lazima apende na boga lake ndo ngoma hiyo
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Karibu dear Vivian umepotea full category iliisha nn?
  Jibu kwa Vivian kwanza kabisa Mtambo utalala doro hakuna kazi itakayo fanyika hapo 24hrs.
   
 19. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Asanteh kwa kunikaribisha kaka!! nilipata ajali na my car which I bought throgh my 2yrs saving was totally written off. i have been recovering slowly but littlebit stressed. I just thank God I came out alive. anyway yote mipango ya Mungu

  Anyway asante kwa jibu zuri! I think that is the answer you could give to that young boy!

  Nice day Fidel
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Dah pole sana lakini natumaini sasa hivi upo oky!
  Huku umia? Ilikuwaje mpaka ukala bam?
   
Loading...