Afadhali ushike jembe ukalime, kuliko kuomba sala hii

Afadhali ushike jembe ukalime, kuliko kuomba sala hii

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Utapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo:

Kibiblia, hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Bikira Maria amepewa jukumu la kuwa mlinzi wa taifa lolote. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa Mlinzi wa taifa, iwapo taifa hilo linamwamini na kumkubali.
Zaburi 33:12
"Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu.”

Je, Bikira Maria ana uwezo wa kuwaombea watu huko aliko? Biblia haitufundishi popote kwamba wafu wanaweza kuwaombea walio hai. Badala yake, Biblia inaeleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea(Warumi 8:26). Ukisoma pia Ebr 7:25 imeandikwa kuwa Yesu anatuombea.
Naye[Yesu], kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Ingawa Maria aliheshimiwa na Mungu kwa kuchaguliwa kumzaa Yesu, hana mamlaka ya kuombea watu baada ya kifo chake.

Bikira Maria hakuwa Mkingiwa dhambi ya asili. Kuna watu wanafundisha kwamba Bikira Maria "alikingiwa" dhambi ya asili(the dogma of the Immaculate Conception); yaani kwamba alizaliwa bila dhambi ya asili.

Mafundisho hayo sio sahihi kwa sababu Maandiko yanasema:
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 3:23

Andiko hilo halibagui. Watu wote wanahitaji wokovu kwa njia ya Yesu, hata Maria mwenyewe alisema:
“Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” Luka 1:47

Bikira Maria alimtambua Mungu kuwa ndiye Mwokozi wake, hivyo naye pia alihitaji neema ya Mungu kama wengine.

Bikira Maria anastahili heshima kama mama aliyemzaa Bwana Yesu, lakini kama tulivyoona, hatupaswi kumwita mlinzi wa taifa. Kwahiyo ukifunga na kumsihi Bikira Maria akuombee, utapoteza muda wako bure. Afadhali ushike jembe ukalime!

Kama hukubaliani na hoja hizo, weka hapa Maandiko yanayokuambia kwamba "Bikira Maria ni Mlinzi wa Taifa lako, na kwamba yeye ni Mkingiwa dhambi ya asili."

Na kuhusu Maria kwamba anaweza kukuombea, usijitetee kwa kutaja lile tukio la arusi ya Kana ambapo Maria alimwambia Yesu "hawana divai" kisha Yesu akatenda muujiza divai njema ikapatikana. Hilo tukio lilifanyika Maria alipokuwa hai duniani. Sasa hivi Maria hayupo tena. Waliofariki hawasikii wala hawajui chochote kinachoendelea kwa walio hai duniani. Soma Mhubiri 9:6
"lakini wafu hawajui chochote...upendo wao, chuki yao na wivu wao vimetoweka tangu kitambo, kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua."
 
Kama una hitaji lolote, omba kwa kufuata mwongozo huu, utapata majibu ya maombi yako:

1. Omba kwa Jina la Yesu
“Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, nitalifanya.” — Yohana 14:14

2. Omba kwa imani
Yakobo 1:6
"Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.”

3. Omba sawasawa na mapenzi ya Mungu
1 Yohana 5:14
"Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia..”

4. Kabla hujaomba, wasamehe waliokukosea. Usiombe huku una kinyongo
Marko 11:25
"Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu”

5. Omba kwa bidii na kwa uvumilivu
Yak 5:16
"...kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."

Luka 18:1
Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.

Na usisahau, kabla ya kuomba, hakikisha umetubu dhambi zako zote.
Isaya 59:2
"Lakini maovu yenu yamewatenganisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia..”

Zaburi 66:18
"Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia."

Methali 28:9
"Anayekataa kuisikia sheria, huyo hata sala yake ni chukizo kwa Mungu."
 
Utapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo:

Kibiblia, hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Bikira Maria amepewa jukumu la kuwa mlinzi wa taifa lolote. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa Mlinzi wa taifa, iwapo taifa hilo linamwamini na kumkubali.
Zaburi 33:12
"Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu.”

Je, Bikira Maria ana uwezo wa kuwaombea watu huko aliko? Biblia haitufundishi popote kwamba wafu wanaweza kuwaombea walio hai. Badala yake, Biblia inaeleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea(Warumi 8:26). Ukisoma pia Ebr 7:25 imeandikwa kuwa Yesu anatuombea.
Naye[Yesu], kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Ingawa Maria aliheshimiwa na Mungu kwa kuchaguliwa kumzaa Yesu, hana mamlaka ya kuombea watu baada ya kifo chake.

Bikira Maria hakuwa Mkingiwa dhambi ya asili. Kuna watu wanafundisha kwamba Bikira Maria "alikingiwa" dhambi ya asili(the dogma of the Immaculate Conception); yaani kwamba alizaliwa bila dhambi ya asili.

Mafundisho hayo sio sahihi kwa sababu Maandiko yanasema:
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 3:23

Andiko hilo halibagui. Watu wote wanahitaji wokovu kwa njia ya Yesu, hata Maria mwenyewe alisema:
“Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” Luka 1:47

Bikira Maria alimtambua Mungu kuwa ndiye Mwokozi wake, hivyo naye pia alihitaji neema ya Mungu kama wengine.

Bikira Maria anastahili heshima kama mama aliyemzaa Bwana Yesu, lakini kama tulivyoona, hatupaswi kumwita mlinzi wa taifa. Kwahiyo ukifunga na kumsihi Bikira Maria akuombee, utapoteza muda wako bure. Afadhali ushike jembe ukalime!

Kama hukubaliani na hoja hizo, weka hapa Maandiko yanayokuambia kwamba "Bikira Maria ni Mlinzi wa Taifa lako, na kwamba yeye ni Mkingiwa dhambi ya asili."

Na kuhusu Maria kwamba anaweza kukuombea, usijitetee kwa kutaja lile tukio la arusi ya Kana ambapo Maria alimwambia Yesu "hawana divai" kisha Yesu akatenda muujiza divai njema ikapatikana. Hilo tukio lilifanyika Maria alipokuwa hai duniani. Sasa hivi Maria hayupo tena. Waliofariki hawasikii wala hawajui chochote kinachoendelea kwa walio hai duniani. Soma Mhubiri 9:6
"lakini wafu hawajui chochote...upendo wao, chuki yao na wivu wao vimetoweka tangu kitambo, kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua."
Hakuna kitu kinaitwa "Bikira Maria". Maria alipomzaa Yesu hakuwa bikira tena. Ni kweli Maria alipata Neema ya Yesu kupitia kwake lakini yeye alikuwa ni mtumishi wa Mungu kama walivyokuwa na walivyo wengine. Yeye alimaliza kazi yake na baada ya Yesu kufa msalabani na kufufuka Maria alikuwa ni miongoni mwa Wanafunzibwa Yesu. Na alikuwa na option pia ya kutomwamini Yesu.
Yesu Kristo ndiye njia kweli na uzima. Hakuna wokovu ktk mwingine awaye yote. Pia Yesu Kristo ni Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melekzedek naye ndiye anayetuombea kwa baba hakuna mwingine. Roho Mtakatifu yeye anaomba ndani yetu na anatusaidia udhaifu wetu. Hivyo, maombi yenye nguvu ni yale yanayovuviwa na Roho Mtakatifu. Kuomba kupitia Maria ni mapokeo ya Warumi ambao ktk dini yao ya kipagani walikywa na mungu mke. Sasa baada ya ukristo kuingia Rumi wakabadili baadhi ya tamaduni zao kuwa za Kikristo. Mojawapo ni kumuingiza huyo mungu mke wao kinyemela na kumuita Bikira Maria jambo ambalo ni kinyume na maandiko. Hivyo ndugu zetu wakatoliki hebu achaneni na mapokeo yasiyo ya Biblia. Tumtegemee Yesu Kristo peke yake.
 
Yesu Kristo ndiye njia kweli na uzima. Hakuna wokovu ktk mwingine awaye yote. Pia Yesu Kristo ni Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melekzedek naye ndiye anayetuombea kwa baba hakuna mwingine. Roho Mtakatifu yeye anaomba ndani yetu na anatusaidia udhaifu wetu. Hivyo, maombi yenye nguvu ni yale yanayovuviwa na Roho Mtakatifu.
Amina
 
Unahangaika na kanisa katoliki wewe,sijui lilikufanya nini!?
Kwenye uzi huu nimetaja wapi Kanisa Katoliki?
Kwa nini usijikite kwenye kuchapa injili..
Injili ni nini kwako, mkuu? Kwangu mimi Injili ni habari njema. Habari njema ndio hizo nimekupa, kwamba tukimuomba Mungu kwa Jina la Yesu na kuzingatia mambo hayo mengine, tutapewa mahitaji yetu. Tusipoteze muda kumtaja Maria. Muda ni mali.
Efe 5:16-17
"Mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana."
 
Huwezi kupata maana ya kila jambo... Na utakufa ungali hujayajua baadhi ya mambo.
Ni kweli hatuwezi kuelewa kila jambo kikamilifu, maana maandiko yanasema: ‘Mambo ya siri ni ya Bwana Mungu wetu, bali mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele’ (Kumbukumbu la Torati 29:29). Mungu ameishatufunulia vya kutosha katika Neno lake mambo muhimu kuhusu maisha ya wanadamu walio hai na wafu. Hivyo, hatupaswi kupuuza yale ambayo Mungu tayari ametufunulia — kwa mfano, tumeona leo kwamba wafu kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua. (Mhubiri 9:5–6). Hiyo sentensi unahitaji malaika waje wakuambie ina maana gani? Mbona hata mtoto mdogo anaweza kuielewa.
 
Back
Top Bottom