Adhabu ya Viboko Shuleni na Nyumbani,wewe una maoni gani?

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,690
2,000
Ni muda mrefu sasa wanaharakati mbali mbali wamekuwa wakipigia kelele swala hili. Nchi kadhaa duniani ikiwemo Kenya wamefuta adhabu hii.Kwao hii ni jinai;mwalimu au mzazi ukibainika amemchapa mtoto unawajibishwa.Hapa Tanzania adhabu hii bado ipo,ila kuna utaratibu na kikomo cha kuitoa hasa shuleni.

Swali:Kwa mazingira yetu haya,je umefika muda muafaka wa kuiondoa kabisa adhabu hii nyumbani na shuleni? Kama tunataka iendelee je,utumike utaratibu gani wa kuitoa hasa nyumbani?
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
34,773
2,000
akina dogo wenyewe bila kiboko hawaendi kabisa,
ili mradi chapa bila jazba tena chapa makalioni kama tulivyochapwa enzi za mwalimu.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,726
2,000
Mimi naipinga kabisa hiyo adhabu. Unichapie mtoto basi jua utadili na mimi. Ni ngumi tu mwanzo mwisho.
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,722
2,000
ni muda mrefu sasa wanaharakati mbali mbali wamekuwa wakipigia kelele swala hili. Nchi kadhaa duniani ikiwemo kenya wamefuta adhabu hii.kwao hii ni jinai;mwalimu au mzazi ukibainika amemchapa mtoto unawajibishwa.hapa tanzania adhabu hii bado ipo,ila kuna utaratibu na kikomo cha kuitoa hasa shuleni.

Swali:kwa mazingira yetu haya,je umefika muda muafaka wa kuiondoa kabisa adhabu hii nyumbani na shuleni? Kama tunataka iendelee je,utumike utaratibu gani wa kuitoa hasa nyumbani?

mimi napenda iwepo daima, kama siyo adhabu hiyo, uwezekano wa kuwa hivi nilivyo nauona mdogo kabisa. Iliniokoa na tabia za ajabu, ilinifanya nipende masomo, ilinikimboa kifikra.
 

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,690
2,000
Hili jambo kila mtu ana mtazamo wake.Ila tunatakiwa kuangalia mazingira yetu,je kweli tumekia muda muafaka? Maana kila jawabu lina faida na hasara zake juu ya hili.
 

kivyako

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
14,346
2,000
Kudesa(kuiga) kila kitu bila kuangalia mazingira ndo kinachotusumbua watanzania, kwa vile wazungu hawachapi na sisi tusichape, tuko tofauti sana nao kimaadili na kila kitu, watoto wetu lazma wapate kiboko lakini kwa kiwango stahiki na kwa utaratibu bila jaziba.
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,353
2,000
Mtoto aliyekosa kiboko toka kwa ***** huwa mzigo kwa jamii. Ndiyo maana siku hizi unakutana na kitoto kinavuta sigara halafu hata kukizabua unashindwa. Vibinti unakuta kipo na kibabu hata la kusema huna. Ndiyo maana tunaamua kuvimega tu.

Niligongana na binti ya kakangu calabash eti form 5 anasema amekua nikamtimua mbele za watu na ikawa mwanzo na mwisho kutoka usiku kama amekua ahame kwangu kwanza namsaidia ada halafu analeta ukubwa eti im grown up.

Mie kwangu ni kwamba ukileta ujinga ni bakora kwenda mbele. Ukiona umekua then hama nyumbani kwangu. Period.
 

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
4,495
2,000
Kudesa(kuiga) kila kitu bila kuangalia mazingira ndo kinachotusumbua watanzania, kwa vile wazungu hawachapi na sisi tusichape, tuko tofauti sana nao kimaadili na kila kitu, watoto wetu lazma wapate kiboko lakini kwa kiwango stahiki na kwa utaratibu bila jaziba.

Kwa taarifa yako hata hiyo adhabu ya viboko Tanzania walileta wazungu, ndio waliotufundisha kuchapa watoto, yaani jinsi wanavyochapwa leo shuleni, matakoni au mikononi na ni viboko vingapi vinaruhusiwa hayo yote walileta wazungu, na walileta kutoka kwao kwa maana wakati huo hata wao pia watoto wao walikuwa wanachapwa shuleni, lakini sasa hivi hawachapi watoto wao tena kwa maana wameshapima na kujiuliza maswali mengi sana pamoja na hayo unayojiuliza wewe na wakagundua kuwa kumchapa mtoto hakumsaidii chochote katika maendeleo yake ya kitaaluma na kimaisha wakaamua kufuta, sasa kwa nini na sisi tusifute, kama waliotufundisha kuchapa hawachapi tena?

 

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,770
2,000
ni muda mrefu sasa wanaharakati mbali mbali wamekuwa wakipigia kelele swala hili. Nchi kadhaa duniani ikiwemo kenya wamefuta adhabu hii.kwao hii ni jinai;mwalimu au mzazi ukibainika amemchapa mtoto unawajibishwa.hapa tanzania adhabu hii bado ipo,ila kuna utaratibu na kikomo cha kuitoa hasa shuleni.

Swali:kwa mazingira yetu haya,je umefika muda muafaka wa kuiondoa kabisa adhabu hii nyumbani na shuleni? Kama tunataka iendelee je,utumike utaratibu gani wa kuitoa hasa nyumbani?

viboko vikatazwe kimya kimya ole wenu mkiwatangazia wanafunzi kuwa kuanzia sasa hakutakuwa na viboko kwa wanafunzi, siku hiyo hiyo watoto watafanya sherehe kwa mbwembwe barabarani
 

utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,367
0
Viboko vinasaidia sana, hii mambo ya "Precious stop, Wee Clinton acha" yanafaa huko Masaki.
 

Amri kuu ni Upendo

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
765
500
Kwa taarifa yako hata hiyo adhabu ya viboko Tanzania walileta wazungu, ndio waliotufundisha kuchapa watoto, yaani jinsi wanavyochapwa leo shuleni, matakoni au mikononi na ni viboko vingapi vinaruhusiwa hayo yote walileta wazungu, na walileta kutoka kwao kwa maana wakati huo hata wao pia watoto wao walikuwa wanachapwa shuleni, lakini sasa hivi hawachapi watoto wao tena kwa maana wameshapima na kujiuliza maswali mengi sana pamoja na hayo unayojiuliza wewe na wakagundua kuwa kumchapa mtoto hakumsaidii chochote katika maendeleo yake ya kitaaluma na kimaisha wakaamua kufuta, sasa kwa nini na sisi tusifute, kama waliotufundisha kuchapa hawachapi tena?


Ipitie vizuri historia ya mwafrika mzee, adhabu tulizokuwanazo ni mbaya zaidi ya viboko.viboko ilikuwa ni kwa mkosaji wa kosa la kawaida sana aloo!!
 

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,601
2,000
Mkuu Mrimi,

Nadhani, kwa mtazamo wangu,
Mashuleni:
Kuwe na madili(utaratibu), ISIFUTWE bali kuwe na maadili fulani katika kuitekeleza hiyo adhabu, mf. idadi ya viboko fulani atachapwa mwanafunzi, katika eneo fulani la mwili...nasema hivi kwani tumeshuduia wanafunzi wakichapwa hadi kupoteza fahamu wengine kupoteza maisha!

Nyumbani:
Kuna umri fulani mtoto ukimueleza ni viboko kwake, lakinikatika umri mdogo bado anahitaji kufunzwa(kwa kulazimishwa wakati mwingine)..sasa kulazimishwa huku kunategemea na malezi ya mzazi/mlezi..mfano, wengine huwakaripia(kuwagombeza), wengine huwachapa na wengine huwatesa(kuwanyima chakula n.k).

Nadhani kumchapa mtoto hakuna ubaya(hasa kwa kuangalia umri, kosa, mwenendo)..hata kwa malezi ya kidini(Mithali 23:13)/ (Proverbs 23:13) bado inakubaliana na hilo.
 
Last edited by a moderator:

mnogapavanu

Member
Dec 4, 2012
81
125
Hata kwenye BIBLIA imeandikwa kama mtu asipomchapa mwanawe kwa makosa aliyotenda basi huyo mtoto utakuwa mzigo wake.Sema tu kuwa kuna adhabu za aina nyingi anazoweza kupewa mtoto.Kinachotakiwa hii ya vibogo itolewe kwa kiasi,si kuzidisha sana.
 

Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,322
2,000
Wakuu mambo ya kuiga hayo. Hivi tunafahamu jinsi wenzetu wa North wanavyoteseka leo na watoto wao? Tuache upuuzi wa kuiga mambo ya Ulaya. Viboko muhimu. Watu tulikuwa hatujui kusoma lakini vilipotembea mbona within a month tulijua na kuipenda shule jumla? Hongera mwl. wangu late Samson Nyanda (RIP) kwa viboko vyako leo vimenisaidia na mimi leo ni mtu!
 

Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,069
1,750
watoto hawa wa dot com bila viboko hawafiki popote haya ndio mambo ya kuiga bila kujipanga watoto wa wenzetu wahapigwi lakini wameshalelewa katika mazingira fulani ya kutodanganya kuwa na adamu na kadha wa kadha sasa ya kwetu haya waongo watukutu wazazi wenyewe wameshachanganya madesa katika malezi bila viboko kwa kweli hapana hawatafika.
mbona sisi tulichapwa sana na hatukufa?
cha msingi walimu wengine huwa wanawachapa wanafunzi isivyostahili hii ndio hairuhusiwi.
 

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,743
2,000
Jamani ili swala lamalezi kila m2 ana stil yake kuna wa2 ni mabigwa wa kusema sanaaa wenginge bakola2 ila wote tuna lenga ki2 kimoja mtoto ae na maaadili mema .ila mungu kesha tupa mfumo wa malezi kwa watoto wetu kwamba akoseapo achapwe kutokana na umri alio nao kwahiyo bakora ndio njia pekee mungu aliyo tupa kwenye malwzi atakae pinga labda yeye hana dini
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,647
2,000
bakora nyumbani liachiwe mzazi hata nchi nyingi za ulaya hawaruhusu viboko shuleni ila nyumbani wanaruhusu ni chache zinazokataza kote kama ujerumani. nchi kama korea yenye watu wachapakazi sana wanapiga viboko mbaya shuleni na nyumbani na singapore pia. mi siungi mkono viboko shuleni ila kama vinaendelea awepo walau mwalimu mmoja tu wakuitoa tena iwe baada ya njia zote kushindwa sio kila mwalimu anajichapia tu. mbona watoto wakitajiri hawachapwi na ndio wengi mavyuoni kwani ukiwa masikini inamaanisha huwezi kufundishwa bila viboko? tena watoto wa kitajiri wananidhamu kweli chuoni sababu wamezoeshwa kupenda majukumu lakini watoto wa kimaskini kwa vile hakuna viboko wanakosa sense of responsibilities na kuishia kudisco. wataalamu wanasema adhabu haibadili tabia bali inamfanya mtu atafute mbinu mbadala ambayo itamwezesha kuendelea na tabia yake na kuepuka adhabu.
 

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,113
1,250
Mimi naomba bakora iendelezwe, bongofleva na magezeti ya udaku vimeharibu sana vijana wetu. hao wanaotuambia tuache kuchapa mbona wao bado wanafanya. hebu angalia hapo chini:

Corporal Punishment in Public Schools, by State

The following table lists the states allowing corporal punishment in schools according to state name and the number of students hit.

States Allowing Corporal Punishment


StateNumber of
students hit
Percent of
total students
Alabama33,7164.5%
Arizona16([SUP]1[/SUP])
Arkansas22,3144.7
Colorado8([SUP]1[/SUP])
Florida7,1850.3
Georgia18,2491.1
Idaho1110.4
Indiana5770.5
Kansas50.01
Kentucky2,2090.3
Louisiana11,0801.7
Mississippi38,1317.5
Missouri5,1590.6
New Mexico7050.2
North Carolina2,7050.2
Ohio6720.04
Oklahoma14,8282.3
South Carolina1,4090.2
Tennessee14,8681.5
Texas49,1971.1
U.S. total223,1900.46
NOTES: Figures are from 2008.
1. Less than 0.1%
Source: The Center for Effective Discipline, Columbus, Ohio. www.stophitting.com

States Not Allowing Corporal Punishment


The following table lists the states that do not allow corporal punishment in schools, according to state name and the year in which corporal punishment was banned.

StateYear
banned
Alaska1989
California1986
Connecticut1989
Delaware2003
Hawaii1973
Illinois1993
Iowa1989
Maine1975
Maryland1993
Massachusetts1971
Michigan1989
Minnesota1989
Montana1991
Nebraska1988
Nevada1993
New Hampshire1983
New Jersey1867
New York1985
North Dakota1989
Ohio1994[SUP]1[/SUP]
Oregon1989
Pennsylvania2005
Rhode Island1977
South Dakota1990
Utah1992[SUP]2[/SUP]
Vermont1985
Virginia1989
Washington1993
West Virginia1994
Wisconsin1988
1. Corporal punishment is permitted in Ohio schools if a school board follows several procedures before voting to allow it. Parents in districts which allow it may refuse to have their children paddled.
2. Corporal punishment is permitted in Utah schools if a parent or guardian gives written permission for its use.

Source:
The Center for Effective Discipline, Columbus, Ohio. www.stophitting.comRead more: Corporal Punishment in Public Schools, by State — Infoplease.com Corporal Punishment in Public Schools, by State — Infoplease.com
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom