Sehemu anapopata chakula mtoto wako akiwa shuleni pana hali gani?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu kwema?

Shuleni ni sehemu ambako watoto (walioanza kwenda shule) wanatumia muda mwingi kuliko nyumbani. Mbali na masomo, chakula ni kitu muhimu pia ambacho kina nafasi kubwa katika ukuaji wa mtoto.

Sasa je, unajua sehemu anapopata chakula mtoto wako ina hali gani?

Kuna shule ukiona canteen zao yaani unajua ni Mungu tu ndio anawalinda watoto hao, kwa jinsi kulivyokithiri uchafu, maji ya kuoshea vyombo meusiii kwa jinsi yalivyorudiwa kuoshea vyombo hivyo mara nyingi, viazi vya chips unakuta viko kwenye maji machafu, mpishi mwenyewe machafu, sehemu ya kulia haileweki, na hali ni mbaya zaidi kwenye shule za serikali.

Shule nyingine (hasa za serikali) hurusu wafanyabiashara mbalimbali kuuza bites na vyakula hapo, ambao kiukweli hata huwa hawafatiliwi huduma wanayoitoa ina ubora kiasi gani na kama wanazingatia usafi.

Nakumbuka shule niliyosoma (ya serikali) kwakweli ni Mungu tu alikuwa anatulinda, sehemu ilikuwa chafu, maji ya kuoshea viazi vya chips ni balaa, vi bites kachori, sambusa, vitumbua, chips zinafungwa kwenye magazeti, magazeti yenyewe yamefinywangwa hapo, maji ya kunawa mpaka ukalitafute bomba ni mbaali, yaani ni tafrani, uchafu mtindo mmoja.

Tukumbuke bila afya hakuna kitu kinaweza kufanyika. Mbali na kufatilia tabia ya mtoto wako shuleni, ufaulu wake, unafatilia kujua canteen anapokula mtoto wako kuna hali gani?
 
Shule nyingi za kutwa za umma hali ndio huwa mbaya sana, wauzaji hakuna anayejali usafi kabisa, anachowaza ni kuuza chakula chake na kusepa. Wauzaji chakula wakishaondoka, ukitembelea lile eneo la canteen unaweza kutapika kwa uchafu ule.
 
Shule nyingi za kutwa za umma hali ndio huwa mbaya sana, wauzaji hakuna anayejali usafi kabisa, anachowaza ni kuuza chakula chake na kusepa. Wauzaji chakula wakishaondoka, ukitembelea lile eneo la canteen unaweza kutapika kwa uchafu ule.
Ni kweli, mazingira ni machafu sana na walimu hata hawajali kufatilia maana wao wanakuwa na sehemu maalum za wanazonunua chakula
 
Back
Top Bottom