Kwa taarifa yako hata hiyo adhabu ya viboko Tanzania walileta wazungu, ndio waliotufundisha kuchapa watoto, yaani jinsi wanavyochapwa leo shuleni, matakoni au mikononi na ni viboko vingapi vinaruhusiwa hayo yote walileta wazungu, na walileta kutoka kwao kwa maana wakati huo hata wao pia watoto wao walikuwa wanachapwa shuleni, lakini sasa hivi hawachapi watoto wao tena kwa maana wameshapima na kujiuliza maswali mengi sana pamoja na hayo unayojiuliza wewe na wakagundua kuwa kumchapa mtoto hakumsaidii chochote katika maendeleo yake ya kitaaluma na kimaisha wakaamua kufuta, sasa kwa nini na sisi tusifute, kama waliotufundisha kuchapa hawachapi tena?
Bakora ziendelee kama kawaida,tusizidi kudesa kila kitu kutoka katika nchi nyingine.