nameless girl;
1. Kunyonga mtu kwa kwa kosa la kuua ni sawa na kurudia kosa la huyo aliyeua na kujificha nyuma ya mgongo wa sheria. HAKI NA UHURU UTOLEWA NA SHERIA WALA HAIJI BY NATURE, KWA IYO SHERIA IKISTATE, BASI HAPO HAKUNA KUJIFICHA NYUMA YA SHERIA BALI NDO SHERIA INAVOELEKEZA. KAMA MNASEMA HAKUNA SABABU YA KUONDOA UHAI WA MTU ALIYEUA , IYO HAKI INATOKA WAPI?KWA NINI ANAYEUA KWA UPANGA ASIFE KWA UPANGA??
2. Hakuna usawa wa haki nchini kwetu so watu watakaokuwa wananyongwa ni wale watakaokua wanashindwa kutoa corruption so kwa hili, tutapaswa kuita haki au mauaji? HII NI ASSUMPTION, JE NA KWA KWA MAHAKAMA INAYOFUATA HAKI NA KUTOKUWA NA CORRUPTION? JE CORRUPTION INAONDOLEWA KWA KUTONYONGA WAUAJI??
3. Nchi yetu ni masikini sana. Kumpoteza mtu mmoja katika taifa letu ni sawa na kupoteza nguvukazi ya taifa letu. Hao wanaopaswa kuuwawa wanapaswa kupewa kazi tofauti waweze kucontribute chochote kwa taifa lao. MTU AUE THEN AOMBE KUPEWA KAZI NYINGINE??KWA NINI ASINGEMUACHA MWENZIE AISHI THEN WAJENGE TAIFA PAMOJA?? TANZANIA SIO MASKINI ILA WATU WAKE NDO MASKINI
4. Nadhani art 13 inaongelea right to life. Kuwa na hii adhabu ni sawa na kufundisha jamii jinsi ya kukiuka sheria zilizowekwa.KUKIUKA SHERIA ZILIZOWEKWA NI PAMOJA NA KUKIUKA SHERIA YA KUNYONGA WAUAJI NA WENGINE WANAOSTAHILI ADHABU IYO. ARTICLE 13(1) inakataza ubaguzi, iweje mtu aue then yeye aone ana haki ya kuishi?
ibara ya 14 inasema kila mtu anayo haki ya kuishi....je kwa nini mtu aue wakati yeye anatambua haki ya mwenzie kuishi??anayekiuka haki iyo apewe tuzo au adhabu kama iyo?? Ukitetea haki ya kuishi, basi utetee na haki ya kutofungwa kama ibara ya 15 inavyoelekeza....
5. Hao watu wanaonyongwa, l believe wana watu wanaotegemewa, so killing a hero wa familia its like you kill more than one person.
...... HERO WA FAMILIA ANAYEANGAMIZA FAMILIA ZINGINE ANAFAA KUITWA HILO KATIKA ILO TAIFA?? HERO AWE NA UHALALI WA KUUA WENGINE ILA YEYE AISHI??
Hata ivo nakupongeza kwa kutumia haki yako uliyopewa na Jamhuri chini ya ibara ya 18(a)