ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

Hujui hilo?


Cuf na nccr agizo la UKAWA!

Teh teh teh Lipumba alimsaidia kikwete kwenda ilkulu leo agizo la ukawa cuf na nccr mliwakataa mchana kweupe kwamba ccm b leo kulikoni mshawahi kutangazia umma kwamba zile kauli sio za kweli ili tuwaelewe?
 
Ndugu zangu zitto na mbowe ndo walio gombana kwa nini wengine wanashadadia ugon=mvi usio wahusu??? wekeni tofauti zenu chini mfanye siasa dhidi ya CCM ..OVER
 
I beg,I beg,do not let them in.I forbid in the name of the holy creator,it is the time to cast them away.
 
Chama cha ACT-Wazalendo kimeandika barua kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) kikiomba kujua masharti ya kujiunga ili nacho kiwe sehemu yake,imefahamika.

Katibu mkuu was ACT,Maingu Samson Mwigamba,alilithibitishia gazeti hili kwamba chama chake kilituma barua ya kuomba kujiunga UKAWA Jumamosi iliyopita,April 25,2015,kwa vyama vyote vinavyounda UKAWA lakini ile iliyokwenda CHADEMA ilirudi.

"Ni kweli kwamba tuliandika barua kwenda kwa vyama vinne vinavyounda UKAWA. Malengo ya ile barua yalikuwa mawili; moja ni kueleza nia ya kutaka kujiunga na umoja huo na pili ni kuuliza ni utaratibu zipi zinatakiwa kufuatwa kabla ya chama kuruhusiwa kujiunga na umoja huo..."

Chanzo: RAIA MWEMA 29/04/2015


Kitu gani maalum sana ACT wanakiona ni muhimu wakipate ndani ya UKAWA? Kwa mtazamo wangu bado ni chama kichanga kiumri na kinahitaji sana kujijenga ili kiwe na mfumo mzuri wa kisiasa na uendeshaji kabla ya kufikiria kujiunga kwenye ushirikiano wowote ule. Wanahitaji kujipambanua ndani ya jamii na Watanzania, wawe na mfumo na mtandao wa chama chao, waaminike na wawe na uwezo wa kuendesha mambo yao kwa kujisimamia wao wenyewe kwanza.

Kwa hisia za usaliti wanazotuhumiwa nazo na baadhi ya wanaUKAWA ni sababu tosha kuwa wanahitaji kushughulikia chama chao ili kuwaaminisha Watanzania kuwa yanayozungumzwa dhidi yao si sahihi hiyo itawasaidia kupata huruma ya Watanzania na pengine kuchaguliwa vyema wakati wa uchaguzi.

Binafsi sijashawishika kama wanayo dhamira ya kweli ya kuwa chama cha siasa, ukiachilia mbali harakati za mikutano waliyofanya hivi karibuni ambayo bahati nzuri ilipata nafasi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ukiondoa hilo ACT haijafanya sana katika siasa za upinzani. Kujiunga na UKAWA ni kujimeza na watakosa 'identity' kwani wao ni tofauti sana na hivyo vyama vingine kama CUF. NCCR, CDM ambavyo historia zao zinaeleweka na vimeshapitia misukosuko mingi ya kisiasa na NLD ambacho haina cha kupoteza katika umoja huo hata ukisambaratika.


Kukataliwa na CHADEMA ichukuliwe kama chachu ya kufanya kazi na kuondoa doa la usaliti inalotuhumiwa nalo, kung'ang'ania kutamaanisha kuwa hisia za usaliti zina ukweli. Hawakuwepo katika harakati za kuunda huo umoja hadi hapo ulipofika, sioni sababu kwa nini sasa walazimishe hata kama hawakubaliwi na mmoja tu kati ya waundaji wa UKAWA yaani CDM.

Ikumbukwe kuwa wenzao wameshafika mbali sana katika harakati za kuimarisha ushirikiano huo, inawezekana kuwakubalia wao itamaanisha kurudi nyuma hatua kadhaa na kulazimika kurekebisha baadhi ya taratibu za umoja wao. Nawashauri ACT wawaache wenzao waendelee na mipango yao.


Sitaki kuamini kuwa ACT haiwezi kufanya kazi bila UKAWA. Wakiendelea watasababisha UKAWA kutingishika na kusababisha mpasuko au mgawanyiko. Tuhuma zote zitawaangukia wao ACT na wataadhibiwa na Watanzania. Wajipambanue kama chama cha siasa ambacho kilisajiliwa ili kifanye siasa bila kutegemea nguvu ya kutoka nje ya wao wenyewe. Wasimame katika dhana ya kuwa wanaweza kuendesha siasa zao kama ilivyo kwa TLP, UDP na wengine ambao hawamo ndani ya UKAWA.
 
Ukawa washindwa kuafikiana


KIKAO cha viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimeshindwa kuendelea baada ya baadhi ya wajumbe kushindwa kuafikiana kuhusu hoja iliyowasilishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi, ya kutaka kujitoa kwenye umoja huo, imefahamika.
Viongozi hao walikutana jijini Dar es Salaam jana katika Ofisi Kuu ya Chama cha Wananchi (CUF), ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa wakijadili hatima ya kuachiana majimbo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Katika kikao hicho ambacho kilitarajiwa kuanza saa 4 asubuhi kama ilivyokuwa imepangwa na badala yake kilianza saa 6 mchana, ajenda kuu zilikuwa ni kujadili namna ya kuachiana majimbo ambayo bado mwafaka haujapatikana pamoja na utaratibu wa kumpata mgombea urais kupitia Ukawa.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kilichokuwa chini ya Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, kilishindwa kutoa mwelekeo wa majimbo 18 yenye mvutano huku kila chama kikitaka kugombea kivyake.
Hata hivyo hoja hiyo iliibua mvutano mkali baina ya wajumbe wa kikao hicho ambapo kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ujumbe wake uliongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu.
Kwa upande wa CUF, ujumbe wake uliongozwa na Profesa Lipumba, Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya na Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shaweji Mketo.
NCCR-Mageuzi kiliongozwa na Mwenyekiti wake James Mbatia ambaye baada ya kuwasilishwa hoja ya chama chake alishindwa kuendelea na kikao na kulazimika kutoka nje ya ukumbi wa mikutano.
"Mwanzo tulianza kujadili suala la uandikishaji wapigakura kwa mfumo wa BVR na changamoto zake zilizojitokeza pamoja na hatima ya uwezekanao wa kuwapo kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu.
"Pia tulijadili kwa kina mwendelezo wa ugawaji wa majimbo yaliyobaki, lakini hata hivyo tuliacha ajenda hiyo kutokana na kuibuka kwa hoja nzito kwa kila upande," kilisema chanzo chetu ambacho hakikutaka kuandikwa jina lake gazetini.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinapasha kuwa ilipotimu saa 7 mchana, aliingia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Mbatia, ambaye alishiriki katika hatua za awali za majadiliano hayo, lakini ilipofika saa 9:20 aliondoka kabla kuwasilishwa hoja ya chama chake kutaka kujitoa Ukawa.
Hata hivyo wajumbe walishindwa kuendelea na kikao hicho kutokana na NCCR-Mageuzi kutokuwa na mjumbe ambaye angeweza kueleza kwa undani sababu za kutaka kuchukua uamuzi wa kujitoa.
"Hoja iliyokuwa katika ajenda ni ya NCCR-Mageuzi waliyowasilisha ya kutaka kujitoa Ukawa na dai lao kuu ni kutotendewa haki kwa baadhi ya mambo, hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita.
"Na hili jambo si geni kwani mnapokuwa kwenye jumuiya yoyote inawezekana ikatokea hali ya kutoelewana kwa baadhi ya wajumbe kwa kuona kuna sehemu kuna mmoja anaona hajatendewa haki.
"Na jambo ambalo lilitakiwa ni kuzungumza na kulimaliza ili watu wasonge mbele, na NCCR-Mageuzi walileta kama malalamiko… siwezi kulizungumzia vizuri kwa sababu halijazungumziwa kwa undani kwenye kikao," kilisema chanzo chetu.
Mtoa habari wetu alisema kikao hicho kilitarajiwa kumalizika jana usiku, lakini kutokana na hoja ya NCCR-Mageuzi, ilimlazimu Mwenyekiti wa kikao hicho Profesa Lipumba kukiahirisha saa 11 jioni hadi leo ambapo kitaendelea.
Ukawa inaundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kinachoongozwa na Dk. Emmanuel Makaidi.
Hivi sasa joto la kuwatangaza wagombea urais ndani ya vyama vinavyounda Ukawa pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kupanda huku kila upande ukimvizia mwenzake katika kutangaza mgombea nafasi hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Ukawa katika mkutano wao na wanahabari kueleza kuwa mgombea wao atatangazwa Machi mwaka huu, lakini hadi sasa imepita miezi miwili bila kumtangaza.
Wakati hayo yakiendelea ndani ya Ukawa, CCM nayo hadi sasa imeshindwa kueleza ni lini atapatikana mgombea wake pamoja na kutangazwa kwa hatima ya makada sita wa chama hicho ambao wanadaiwa kuanza kampeni kabla ya wakati.
 
Mungu ni mwema sana,nami nawasihi viongozi wa ukawa wasithubutu kumkaribisha huyu kibaraka,kwa sababu mpaka sasa act na ccm wanaimba wimbo mmoja
Tehetehetehetehe, mbona wakati wa escrow ulimkaribisha? Zitto aliwazidi ujanja kitambo
 
Chadema wabaguzi sana kwanini wanaikataa ACT kujiunga ukawa kwani wao ndiyo wana hati miliki ya ukawa?
 
Mkuu vipi kuhusu Lipumba kumsaidia kikwete 2010 na vipi kuhusu Mbatia sio kibaraka tena wa kikwete?

Kwa sasa wameshastukia Janja ya Kikwete ndio maana Lipumba anasota na Kesi Mahakamani.Nadhani unakumbuka Lipumba alivyowaita CCM Maintarahamwe.Huyu Aya-tolah awali alitumwa avuruge Chadema akiwa ndani ya Chama akastukiwa,Katumwa tena avuruge Upinzani akiwa ACT lakini inaonekana mpango huu hautazaa matunda stahiki kwa sababu watu wameshamstukia na CCM inatumia Fedha nyingi kumgharimikia.Njia ambayo ni rahisi kwa sasa ni kujiunga na UKAWA ili apeleke Siri za Mikakati kwa CCM na wapange mikakati ya kuisamabaratisha UKAWA.
 
UKAWA kwisha habari yao
Mkuu tuliwaambia kuwa chadema wamezidi ubaguzi wao wanataka kupewa kila kitu hivi ulishaona wapi wao wanataka kutoa mgombea urais ,watoe waziri mkuu halafu Cuf eti watoe makamu wa rais lakini NCCR hawajapewa nafasi hata moja.

Lakini jambo baya zaidi wanataka majimbo ya dar yote waachiwe chadema sasa nani atakubali ujinga kama huo.
 
Ombi la Zitto -ACT kutaka kujiunga UKAWA ni mtego wa watawala kutaka kuuvunja UKAWA. Wakuu naomba mchukulie hii kama tetesi ama habari isiyorasmi,bt kutoka kwenye chanzo changu cha ndani ya mfumo.

Ni kwamba ombi la kiongozi mkuu wa ACT wazalendo kutaka chama chake kikaribishwe na hatimaye kuwa sehemu ya UKAWA ni mtego kwa viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA,

Ipo hivi baada ya mfumo kuona hakuna namna rahisi ya kuiokoa CCM isianguke lile anguko kuu mbele ya UKAWA imara,jamaa wa magomeni wakaibuka na mpango mkakati wa kuuvuruga UKAWA kupitia kwa kijana wao, wakampa ramani,atangaze chama chake kutaka kujiunga UKAWA,wakiwa wanajua chama chake alichokisaliti CDM hakitakubali wala kumkubali jamaa awe sehemu ya UKAWA,na hapo ndipo mtego ulipowekwa na hao jamaa wa serikali ya CCM,

Baada ya CDM kukataa ACT isiwe sehemu ya UKAWA,wapo waandishi na watu wa kushinda mitandaoni kupotosha na kufanya propaganda ili kuichafua CDM na viongozi wake wakuu kwamba hawataki kuungana ili kuiondoa CCM madarakani,na katika hili mnaweza kuliona limeshaanza kwenyz mitandao na kwenye baadhi ya magazeti.

Mpango utakaofuata ni kuwafata viongozi wa vyama wenza wa UKAWA yaani wale wa NCCR na CUF kuwashawishi kwamba wanaburuzwa na CDM kwenye UKAWA,na kwamba kuifanya CDM ionekane ndo imevaa koti la UKAWA ,na hapa nimedokezwa kuna viongozi wa "kati"ndani ya vyama vya NCCR na CUF hasa wale walionekana tokea awali kupinga UKAWA ama kuipinga CDM isitie mgombea urais waziwazi,

Nafikiri mnamjua,wawachochee viongozi wao wa juu waikaribishe ACT UKAWA na hili watalifanya bila kujua,watapewa sapoti na (mfumo)then kuna kiongozi mkubwa wa vyama hivyo viwili watamtishia kuanika baadhi ya siri zake,kama hatokubali ACT ijiunge UKAWA kama mbadala wa CDM,atakubali na atawaaminisha wenaake kwamba ni faida kuwa na Zzt ndani ya UKAWA kuliko CDM,hapa CDM itaombwa wafanye tathimini upya wa ugawaji wa majimbo na kuachiana ili aje na pendekezo jipya then CDM wagome na waamue liwalo na liwe.

Then atalazimisha CDM iikubali ACT na mwisho CDM itakataa (wanategemea) na hapo watasema wao wataendelea kushirikiana na ACT,hapo ndipo itakuwa mwisho wa UKAWA ya sasa na kuundwa nyingine ikiwemo ACT,na hapo CCM itakuwa na uhakika wa kushinda udiwani,ubunge na urais kwa kiasi kikubwa.

Jiulize leo kiongozi mkuu wa ACT anapata wapi ujasiri wa kuomba ajiunge UKAWA ,wakati aliwabeza kwa kuwaita ni mujngano wa wasaka tonge?je usaka tonge umebadilika lini?unaona magazeti yanayokomaa na issue ya kuionesha jamii kwamba ACT inataka kuungana na UKAWA ili kuitoa madarakani CCM bt CDM haitaki,hapa lengo kuu ni kuchafua taswira ya CDM na viongozi wake kwa wananchi.

Mpango huu nimedokezwa unaratibiwa kwa ufundi sana na idara,na kuna mikono ya vigogo wa magamba nyuma,majina kapuni,wazalendo wanaoipenda nchi na kupenda mabadiriko wanaendelea kutafta data zaidi,nitazidi kuziweka hapa na kuanika nia ovu ya hili tawi la CCM la ACT na viongozi wake.

Niwaombe viongizi wa UKAWA kuwa imara zaidi,kutobadirisha misimamo na wawe makini na baadhi ya viongozi wa chini wa vyama vyao,kamwe giza haliwezi kushinda Nuru,UKAWA tumaini letu,Mungu aubariki umoja huu udumu,na mwisho na waambia ACT ,badala ya kutaka kubomoa UKAWA kwa gia hiyo,bora wajiunge CCM watengeneze muungano wao na tuwajue,hawataweza.

Nasema ACT haina dhamira ya kweli kujiunga UKAWA bali wanatumiwa kuvuruga UKAWA,wanatafta huruma ya wananchi ionekane wanabaguliwa bt ukweli wanatumiwa na mfumo umeoamua kuisaidia CCM,viongozi wangu wa UKAWA msimjibu Zzk na ACT yake,kwani jibu moja litawapa kick.

Viva chadema viva ukawa, wasaliti wasipewe nafasi kamwe.

UKAWA na especially CDM haiwezi kujiunga na CCM !. Huwezi kujiunga na CCM katika mkakati wa kuiondoa CCM madarakani !.

ACT ni moja ya idara ndani ya CCM kujiunga nayo ni kujiunga na CCM kwa hiyo hilo halitawezekana kabisa !. Itakuwa ni rahisi UKAWA kuvunjika kuliko CDM kujiunga na ACT/CCM !. Haitatokea na maana ya UKAWA haitakuwepo kama CCM kupitia idara yake ya ACT itajiunga na UKAWA.

Mungu bado yupo pamoja nasi, mbinu zao zitashindwa
tukutane october

Huyo Zitto ameona hana uhakika wa hata jimbo moja kushinda , na akome tena na akome akae mbali na UKAWA, hawa ni wasaka tonge awawache, aungane na tlp, UDP na kile cha hamadi rashid nimekisahau

Mungu ni mwema sana,nami nawasihi viongozi wa ukawa wasithubutu kumkaribisha huyu kibaraka,kwa sababu mpaka sasa act na ccm wanaimba wimbo mmoja

story umeipika , na umeishakamata wenzako hao chini

hii ni aibu!!
 
Zitto na chama Chake wanaamini ktk siasa za Ujamaa, Zitto na chama chake wanaamini ktk serikali moja ya muungano, ukawa wanaamini ktk serikali tatu! Ni wazi kuwa Zitto anataka kwenda ukawa kuwavuruga na si vinginevyo
 
Chadema wabaguzi sana kwanini wanaikataa ACT kujiunga ukawa kwani wao ndiyo wana hati miliki ya ukawa?

Wajiunge kwalipi waende wakajiunge n.l.d.,t.l.p.ccm waanzishe umoja wao kwani wamevumbua nini UKAWA pana mgodi ama? Hatutaki manafiki UKAWA.
 
Unajua tuwe wakweli.Ilitumwa na Kurudishwa na nani?

Kuna kipindi nilishtuka sana niliposikia Ben Saanane unataka kujiunga na ACT baada ya kuona kuwa kuna dalili za kunyimwa kugombea jimbo la Rombo kupitia CHADEMA....
 
Last edited by a moderator:
Katiba inatakiwa ibadilishe kipengele cha umri ili watu km zzk+makamba wawe incluively kwenye uraisi.
 
Back
Top Bottom