Wakuu naomba mchukulie hii kama tetesi ama habari isiyorasmi,bt kutoka kwenye chanzo changu cha ndani ya mfumo na kwa mfalme --------- ACT.
Ni kwamba ombi la kiongozi mkuu wa ACT wazalendo kutaka chama chake kikaribishwe na hatimaye kuwa sehemu ya UKAWA ni mtego kwa viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA,
Ipo hivi baada ya mfumo kuona hakuna namna rahisi ya kuiokoa CCM isianguke lile anguko kuu mbele ya UKAWA imara,jamaa wa magomeni wakaibuka na mpango mkakati wa kuuvuruga UKAWA kupitia kwa kijana wao ---------,wakampa ramani,atangaze chama chake kutaka kujiunga UKAWA,wakiwa wanajua chama chake alichokisaliti CDM hakitakubali wala kumkubali jamaa awe sehemu ya UKAWA,na hapo ndipo mtego ulipowekwa na hao jamaa wa serikali ya CCM,
Baada ya CDM kukataa ACT isiwe sehemu ya UKAWA,wapo waandishi na watu wa kushinda mitandaoni kupotosha na kufanya propaganda ili kuichafua CDM na viongozi wake wakuu kwamba hawataki kuungana ili kuiondoa CCM madarakani,na katika hili mnaweza kuliona limeshaanza kwenyz mitandao na kwenye baadhi ya magazeti.
Mpango utakaofuata ni kuwafata viongozi wa vyama wenza wa UKAWA yaani wale wa NCCR na CUF kuwashawishi kwamba wanaburuzwa na CDM kwenye UKAWA,na kwamba kuifanya CDM ionekane ndo imevaa koti la UKAWA ,na hapa nimedokezwa kuna viongozi wa "kati"ndani ya vyama vya NCCR na CUF hasa wale walionekana tokea awali kupinga UKAWA ama kuipinga CDM isitie mgombea urais waziwazi,nafikiri mnamjua,wawachochee viongozi wao wa juu waikaribishe ACT UKAWA na hili watalifanya bila kujua,watapewa sapoti na (mfumo)then kuna kiongozi mkubwa wa vyama hivyo viwili watamtishia kuanika baadhi ya siri zake,kama hatokubali ACT ijiunge UKAWA kama mbadala wa CDM,atakubali na atawaaminisha wenaake kwamba ni faida kuwa na Zzt ndani ya UKAWA kuliko CDM,hapa CDM itaombwa wafanye tathimini upya wa ugawaji wa majimbo na kuachiana ili aje na pendekezo jipya then CDM wagome na waamue liwalo na liwe ,then atalazimisha CDM iikubali ACT na mwisho CDM itakataa (wanategemea) na hapo watasema wao wataendelea kushirikiana na ACT,hapo ndipo itakuwa mwisho wa UKAWA ya sasa na kuundwa nyingine ikiwemo ACT,na hapo CCM itakuwa na uhakika wa kushinda udiwani,ubunge na urais kwa kiasi kikubwa.
Jiulize leo kiongozi mkuu wa ACT anapata wapi ujasiri wa kuomba ajiunge UKAWA ,wakati aliwabeza kwa kuwaita ni mujngano wa wasaka tonge?je usaka tonge umebadilika lini?unaona magazeti yanayokomaa na issue ya kuionesha jamii kwamba ACT inataka kuungana na UKAWA ili kuitoa madarakani CCM bt CDM haitaki,hapa lengo kuu ni kuchafua taswira ya CDM na viongozi wake kwa wananchi.
Mpango huu nimedokezwa unaratibiwa kwa ufundi sana na idara,na kuna mikono ya vigogo wa magamba nyuma,majina kapuni,wazalendo wanaoipenda nchi na kupenda mabadiriko wanaendelea kutafta data zaidi,nitazidi kuziweka hapa na kuanika nia ovu ya hili tawi la CCM la ACT na viongozi wake.
Niwaombe viongizi wa UKAWA kuwa imara zaidi,kutobadirisha misimamo na wawe makini na baadhi ya viongozi wa chini wa vyama vyao,kamwe giza haliwezi kushinda Nuru,UKAWA tumaini letu,Mungu aubariki umoja huu udumu,na mwisho na waambia ACT ,badala ya kutaka kubomoa UKAWA kwa gia hiyo,bora wajiunge CCM watengeneze muungano wao na tuwajue,hawataweza,Nasema ACT haina dhamira ya kweli kujiunga UKAWA bali wanatumiwa kuvuruga UKAWA,wanatafta huruma ya wananchi ionekane wanabaguliwa bt ukweli wanatumiwa na mfumo umeoamua kuisaidia CCM,viongozi wangu wa UKAWA msimjibu Zzk na ACT yake,kwani jibu moja litawapa kick.