ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

Ombi la Zitto -ACT kutaka kujiunga UKAWA ni mtego wa watawala kutaka kuuvunja UKAWA. Wakuu naomba mchukulie hii kama tetesi ama habari isiyorasmi,bt kutoka kwenye chanzo changu cha ndani ya mfumo.

Ni kwamba ombi la kiongozi mkuu wa ACT wazalendo kutaka chama chake kikaribishwe na hatimaye kuwa sehemu ya UKAWA ni mtego kwa viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA,

Ipo hivi baada ya mfumo kuona hakuna namna rahisi ya kuiokoa CCM isianguke lile anguko kuu mbele ya UKAWA imara,jamaa wa magomeni wakaibuka na mpango mkakati wa kuuvuruga UKAWA kupitia kwa kijana wao, wakampa ramani,atangaze chama chake kutaka kujiunga UKAWA,wakiwa wanajua chama chake alichokisaliti CDM hakitakubali wala kumkubali jamaa awe sehemu ya UKAWA,na hapo ndipo mtego ulipowekwa na hao jamaa wa serikali ya CCM,

Baada ya CDM kukataa ACT isiwe sehemu ya UKAWA,wapo waandishi na watu wa kushinda mitandaoni kupotosha na kufanya propaganda ili kuichafua CDM na viongozi wake wakuu kwamba hawataki kuungana ili kuiondoa CCM madarakani,na katika hili mnaweza kuliona limeshaanza kwenyz mitandao na kwenye baadhi ya magazeti.

Mpango utakaofuata ni kuwafata viongozi wa vyama wenza wa UKAWA yaani wale wa NCCR na CUF kuwashawishi kwamba wanaburuzwa na CDM kwenye UKAWA,na kwamba kuifanya CDM ionekane ndo imevaa koti la UKAWA ,na hapa nimedokezwa kuna viongozi wa "kati"ndani ya vyama vya NCCR na CUF hasa wale walionekana tokea awali kupinga UKAWA ama kuipinga CDM isitie mgombea urais waziwazi,

Nafikiri mnamjua,wawachochee viongozi wao wa juu waikaribishe ACT UKAWA na hili watalifanya bila kujua,watapewa sapoti na (mfumo)then kuna kiongozi mkubwa wa vyama hivyo viwili watamtishia kuanika baadhi ya siri zake,kama hatokubali ACT ijiunge UKAWA kama mbadala wa CDM,atakubali na atawaaminisha wenaake kwamba ni faida kuwa na Zzt ndani ya UKAWA kuliko CDM,hapa CDM itaombwa wafanye tathimini upya wa ugawaji wa majimbo na kuachiana ili aje na pendekezo jipya then CDM wagome na waamue liwalo na liwe.

Then atalazimisha CDM iikubali ACT na mwisho CDM itakataa (wanategemea) na hapo watasema wao wataendelea kushirikiana na ACT,hapo ndipo itakuwa mwisho wa UKAWA ya sasa na kuundwa nyingine ikiwemo ACT,na hapo CCM itakuwa na uhakika wa kushinda udiwani,ubunge na urais kwa kiasi kikubwa.

Jiulize leo kiongozi mkuu wa ACT anapata wapi ujasiri wa kuomba ajiunge UKAWA ,wakati aliwabeza kwa kuwaita ni mujngano wa wasaka tonge?je usaka tonge umebadilika lini?unaona magazeti yanayokomaa na issue ya kuionesha jamii kwamba ACT inataka kuungana na UKAWA ili kuitoa madarakani CCM bt CDM haitaki,hapa lengo kuu ni kuchafua taswira ya CDM na viongozi wake kwa wananchi.

Mpango huu nimedokezwa unaratibiwa kwa ufundi sana na idara,na kuna mikono ya vigogo wa magamba nyuma,majina kapuni,wazalendo wanaoipenda nchi na kupenda mabadiriko wanaendelea kutafta data zaidi,nitazidi kuziweka hapa na kuanika nia ovu ya hili tawi la CCM la ACT na viongozi wake.

Niwaombe viongizi wa UKAWA kuwa imara zaidi,kutobadirisha misimamo na wawe makini na baadhi ya viongozi wa chini wa vyama vyao,kamwe giza haliwezi kushinda Nuru,UKAWA tumaini letu,Mungu aubariki umoja huu udumu,na mwisho na waambia ACT ,badala ya kutaka kubomoa UKAWA kwa gia hiyo,bora wajiunge CCM watengeneze muungano wao na tuwajue,hawataweza.

Nasema ACT haina dhamira ya kweli kujiunga UKAWA bali wanatumiwa kuvuruga UKAWA,wanatafta huruma ya wananchi ionekane wanabaguliwa bt ukweli wanatumiwa na mfumo umeoamua kuisaidia CCM,viongozi wangu wa UKAWA msimjibu Zzk na ACT yake,kwani jibu moja litawapa kick.
 
bado sijaelewa zzk anachokitafuta ni nini!!??
mwaka huu wafuata mkumbo na wenye viherehere tutaburuzwaje!!
 
Zitto akipatia kitu kimoja tu, mafanikio juu take hakutakuwa na wa kuzuia.
 
Last edited by a moderator:
Duh zitto kiboko yaani pamoja na kumtoa chadema ila bado anasumbua vichwa vya watu namna hii, ukawa kwenye siasa Kuna mambo mengi kuanzia propaganda hadi kuchomekeana mamluki hvyo wote wafanyavyo ndio siasa msiralamike cha msingi nanyi mjiimarishe katika nanda zote mbona wenzenu wako kimya yale MACCM,
Hii kulalamikia inaonyesha hamjawiva sisi tuwakabidhi nchi kama mtu mmoja tu tangia aanze kukitangaza Chama chake hapa amekuwa gumzo zaidi ya all prominent figure waukawa Je maisha serikali si hata vibazazi vitawasumbua sana
Pls ukawa usilalamike huku mitandaoni chukua hatua kimya kimya huo ndo uanaume kwenye siasa
 
UKAWA na especially CDM haiwezi kujiunga na CCM !. Huwezi kujiunga na CCM katika mkakati wa kuiondoa CCM madarakani !.

ACT ni moja ya idara ndani ya CCM kujiunga nayo ni kujiunga na CCM kwa hiyo hilo halitawezekana kabisa !. Itakuwa ni rahisi UKAWA kuvunjika kuliko CDM kujiunga na ACT/CCM !. Haitatokea na maana ya UKAWA haitakuwepo kama CCM kupitia idara yake ya ACT itajiunga na UKAWA.
 
Chama cha ACT-Wazalendo kimeandika barua kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kikiomba kujua masharti ya kujiunga ili nacho kiwe sehemu yake.

Hata hivyo, wakati vyama vitatu vinavyounda umoja huo vimepokea barua huku kimoja kikikataa kuipokea barua hiyo.

Vyama ambavyo vimepokea barua hiyo ni CUF, NCCR na NLD huku CDM kikidaiwa kutoipokea barua hiyo.

Katibu wa ACT alikiri kutuma barua hiyo kuomba kujiunga UKAWA tarehe 25 April mwaka huu, kwa vyama vyote vinavyounda ukawa, lakini ile iliyokwenda CDM ilirudi.

ACT waliandika barua baada ya kushauriwa na baadhi ya viongozi wa UKAWA wafanye hivyo kama sharti la awali kama wanataka kujiunga na umoja huo.

Chanzo: Raia mwema
 
CDM wanachotakiwa kuelewa kwa akili zao walizojaliwa na Mungu ni kwamba ACT-Wazalendo siyo Zitto tu, kuna wafuasi lukuki ambao wanaitakia nchi hii mema.

Hao ndo inatakiwa waangaliwe na wapewe masharti kama ikibidi, nje ya hapo bado mafisadi wa CCM wataendelea kutu-colonize
 
Chama cha ACT-Wazalendo kimeandika barua kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kikiomba kujua masharti ya kujiunga ili nacho kiwe sehemu yake.

Hata hivyo, wakati vyama vitatu vinavyounda umoja huo vimepokea barua huku kimoja kikikataa kuipokea barua hiyo.

Vyama ambavyo vimepokea barua hiyo ni CUF, NCCR na NLD huku CDM kikidaiwa kutoipokea barua hiyo.

Katibu wa ACT alikiri kutuma barua hiyo kuomba kujiunga UKAWA tarehe 25 April mwaka huu, kwa vyama vyote vinavyounda ukawa, lakini ile iliyokwenda CDM ilirudi.

ACT waliandika barua baada ya kushauriwa na baadhi ya viongozi wa UKAWA wafanye hivyo kama sharti la awali kama wanataka kujiunga na umoja huo.

Chanzo: Raia mwema

Sio siri kwamba ACT ni tawi la CCM. ACT kama wameandika barua kutaka kujiunga na UKAWA watakuwa wametumwa na CCM kwenda kuivuruga UKAWA tu na si vinginevyo. Hakuna asiyejua kuwa ACT ni kundi la usaliti likitumiwa na CCM.
 
Kunamipango inapangwa siku ikikamilika nitacheka sana ukawa watakuja kubinuka kirahisi sana wenyewe mtaniambia punde.
 
Chadema mkikataa basibjueni nccr,cuf,nld na act wataungana mkikubali chama kimekufa sababu watz tutawapuuza kwa siasa zenu za chuki na majungu
 
Sio siri kwamba ACT ni tawi la CCM. ACT kama wameandika barua kutaka kujiunga na UKAWA watakuwa wametumwa na CCM kwenda kuivuruga UKAWA tu na si vinginevyo. Hakuna asiyejua kuwa ACT ni kundi la usaliti likitumiwa na CCM.

Mkuu mbona vuvuzela nape alikanusha kuwa ACT na CCM hazina mahusiano yoyote yale....hata kiongozi mkuu wa ACT nae amesema suala hilo ni propaganda tu na halina ukweli wowote ule.
 
Sio siri kwamba ACT ni tawi la CCM. ACT kama wameandika barua kutaka kujiunga na UKAWA watakuwa wametumwa na CCM kwenda kuivuruga UKAWA tu na si vinginevyo. Hakuna asiyejua kuwa ACT ni kundi la usaliti likitumiwa na CCM.
Mkuu umesahau kuwa ccm walishaungana na ccm,

Lakini pia mbatia ni zao la kikwete ndani ya ukawa ukiyajua haya utaacha kupayuka hovyo.
 
Chonde chonde Profesa Lipumba, Abdu Kambaya, James Mbatia, Mbowe na Dr. Slaa...chonde chonde..naamini mmesoma sana na mnajua mbinu za hiki chama CCM,....Chonde Chonde msikubali....
 
Nani aliwaambia kujiunga UKAWA ni kwa njia ya barua ? UKAWA ni jumuiko la wenye dira na malengo yanayofanana
 
Back
Top Bottom