ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

Chadema mkikataa basibjueni nccr,cuf,nld na act wataungana mkikubali chama kimekufa sababu watz tutawapuuza kwa siasa zenu za chuki na majungu

Wacha kuwaogopesha kushikamana kuzuri
 
CDM wanachotakiwa kuelewa kwa akili zao walizojaliwa na Mungu ni kwamba ACT-Wazalendo siyo Zitto tu, kuna wafuasi lukuki ambao wanaitakia nchi hii mema.

Hao ndo inatakiwa waangaliwe na wapewe masharti kama ikibidi, nje ya hapo bado mafisadi wa CCM wataendelea kutu-colonize

Mkuu inaelekea Una Dr ya Diplomasia maana umesema vizuri Sana. Japo hata Mimi barua hiyo nisingepokea endapo ningekuwa Mwenyekiti mwenza wa Ukawa. Ila point uliyoitoa ni nzuri sana
 
Mkuu mbona vuvuzela nape alikanusha kuwa ACT na CCM hazina mahusiano yoyote yale....hata kiongozi mkuu wa ACT nae amesema suala hilo ni propaganda tu na halina ukweli wowote ule.

Hata kwa akili za kawaida tu asingetegemewa asimame na kutangaza kuwa ACT ni tawi la CCM. Vinginevyo tungemuona amechanganyikiwa
 
Mungu bado yupo pamoja nasi, mbinu zao zitashindwa
tukutane october
 
Sio siri kwamba ACT ni tawi la CCM. ACT kama wameandika barua kutaka kujiunga na UKAWA watakuwa wametumwa na CCM kwenda kuivuruga UKAWA tu na si vinginevyo. Hakuna asiyejua kuwa ACT ni kundi la usaliti likitumiwa na CCM.


Agizo la Chama Twawala = ACT
 
Hata kwa akili za kawaida tu asingetegemewa asimame na kutangaza kuwa ACT ni tawi la CCM. Vinginevyo tungemuona amechanganyikiwa

Je kuna vielelezo rasmi vya kuthibitisha suala hilo.....ikibidi hata mahakamani? Kama hakuna bado inabaki kuwa nadharia ombwe isiyo thabiti.
 
Sio siri kwamba ACT ni tawi la CCM. ACT kama wameandika barua kutaka kujiunga na UKAWA watakuwa wametumwa na CCM kwenda kuivuruga UKAWA tu na si vinginevyo. Hakuna asiyejua kuwa ACT ni kundi la usaliti likitumiwa na CCM.

Mkuu vipi kuhusu Lipumba kumsaidia kikwete 2010 na vipi kuhusu Mbatia sio kibaraka tena wa kikwete?
 
Mkuu inaelekea Una Dr ya Diplomasia maana umesema vizuri Sana. Japo hata Mimi barua hiyo nisingepokea endapo ningekuwa Mwenyekiti mwenza wa Ukawa. Ila point uliyoitoa ni nzuri sana

Mimi napenda kuona upinzani ukistawi ndo maana nikasema kuna watu ndani ya ACT wanaopenda mabadiliko (ukimwondoa Zitto na wenzake wanaoshutumiwa). Hao wapewe fursa, namaanisha ikionekana wanakubalika katika maeneo yao waachiwe wachukue udiwani, au ubunge. fullstop.
 
Chadema mkikataa basibjueni nccr,cuf,nld na act wataungana mkikubali chama kimekufa sababu watz tutawapuuza kwa siasa zenu za chuki na majungu

watanzania gani jisemee wewe.ACT ni kundi la wasaliti so halitakiwi kupewa ushirikiano.
 
Naona ACT inatumiwa kutenganisha Ukawa kwani kwa inavyoelekea ndani ya Ukawa wasipokuwa making kuna chama kinaweza kikakubali muvi ya ACT ili kuipunguza nguvu hii alliance,ishu ya kuleta barua ni zengwe ili ionekane ZZK amekuwa humble ila nyuma yake kuna maandishi tofauti na ikitokea mkakubali maigizi haya ya msaliti huyu mmekwisha
 
watanzania gani jisemee wewe.ACT ni kundi la wasaliti so halitakiwi kupewa ushirikiano.

Ina maana umesahau jinsi watanzania mlivyo waaminisha juu ya cuf na nccr ns leo hii ccm b mmeungana nao tuelewe vipi sasa?
 
Huyo Zitto ameona hana uhakika wa hata jimbo moja kushinda , na akome tena na akome akae mbali na UKAWA, hawa ni wasaka tonge awawache, aungane na tlp, UDP na kile cha hamadi rashid nimekisahau
 
Last edited by a moderator:
Mungu ni mwema sana,nami nawasihi viongozi wa ukawa wasithubutu kumkaribisha huyu kibaraka,kwa sababu mpaka sasa act na ccm wanaimba wimbo mmoja
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-hakuyasema-jana-kwenye-hotmix-ya-eatv-3.htmlNi

kweli kabisa na hii ni hatari sana.
Hata ishu ya Zito ilikuzwa sana kwa kutumia magazeti na mitandao.
Kuna ushahidi mwingine unatakiwa uwe unakamilishwa kwa ushahidi wa kitaalam.
Vijana wengi wanakurupuka tu bila kutafakari kwa kina.

Kwa mtizamo wangu adui mkubwa wa demokrasia na harakati za maendeleo ya watanzania ni viongozi wa vyama vya siasa hasa wapinzani .
Ni ukweli usiopingika kuwa hawa viongozi wanatumia siasa na ujinga wa watanzania kujineemesha.

Mfano rahisi ni UKAWA hawa wanatumika kuwahujumu watanzania. Hawa kwa 100% wametumika kutimiza malengo ya CCM ya kutunga katiba inayowabeba watawala. Walijitoa Bungeni ili wasionekane moja kwa moja kwamba wameihijumu rasimu ya Warioba.
Ndio maana walikua wanapinga kura ya wazi. Walishakula vya watu.Wakaona wakipiga kura ya wazi wataumbuka.
Wakatumia mbinu ya kutoka nje ya bunge.Wasiojua kinachoendelea wakawaunga mkono wakina Mbowe.
Katiba ikapita bungeni kilaini kabisa.

Sasa angalia mbinu nyingine Chafu wanayotumia UKAWA ikiongozwa na msaliti wa demokrasia ambaye pia anatumia siasa kujiimarisha kibiashara Mh.Mbowe. Hawa UKAWA wakishirikiana na CCM wanajua wazi kuwa katiba pendekezwa ikipigiwa kura na watanzania wote haiwezi kupita. Hivyo kilichofanyika ni kuwatumia viongozi wa UKAWA kutumika ili kuwazuia na kuwahamasisha wanachama wao wasipige kura yaani wasusie zoezi la kura ya katiba. Lengo la viongozi hawa wa UKAWA walionunuliwa na kundi maalum ndani ya CCM ni kuhakikisha kuwa katiba pendekezwa inapita bila kupingwa.

Ikumbukwe kuwa hawa wasaliti (viongozi wa UKAWA) ndio walipigia debe Samweli Sita kwa nguvu zote ili awe spika wa bunge maalum la Katiba. Watu walifikiri ni mambo yanayotokea kwa bahati mbaya. Ni mambo yanayopangwa na viongozi wa Chadema na UKAWA wanajua kazi wanayoifanya.
Katiba inayopendekezwa ni katiba bora sana kwa chama chochote kinachoingia madarakani kwani kinawapa watawala madaraka makubwa sana huku mwananchi akiwa kama mtumwa ndani ya nchi yake. Ni katiba inayowafaa sana Viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA endapo wataingia madarakani kwani wataendeleza ubabe wa kutopenda kuulizwa wala kukosolewa. Ndio maana wanazunguka nchi nzima ili kuhakikisha kuwa katiba inayopendekezwa haipigiwi kura ya HAPANA.

HEBU KILA MTANZANIA AJIULIZE SWALI HILI:

Ni kwa nini CCM na UKAWA wanazunguka nchi nzima kuwaambia watanzania kuwa waipigie katiba inayopendekezwa kura ya NDIYO .
Au kama hawataki kupiga kura ya NDIYO basi WASIPIGE KURA kabisa..??? Tafakari sana sana!!!
Huu ni mpango uliosukwa kwa ustadi mkubwa.

Watumishi wa Mungu wanalijua hili ndio maana maaskofu waliamua kuwaambia watanzania wapige kura ya HAPANA walishtukiza mchezo mchafu wa UKAWA na CCM kuipitisha katiba yao bila kupingwa.
Hata Pengo alishtuka japo hakuonyesha msimamo mkali kwa kusema kura ipigwe lakini kwa utashi wa mtu( Hii nayo pia ni demokrasia halali kabisa)

Tujiulize ni kwa nini wanaohamasisha watu wasipige kura hawakamatwi kwa kuvunja sheria.
Sheria inasema kuwa patakuwa na nafasi ya wananchi kupiga kura ya ama kuikubali au kuikata katiba inayopendekezwa.
Sasa hiyo mamlaka ya kuvunja sheria na kuwaambia wananchi wasipige kura UKAWA wanayapata wapi?

Kama kweli hatuitaki katiba pendekezwa ni lazima tujitokeze kwa wingi na kupiga kura ya HAPANA.

MUNGU tufungue macho watanzania ili tuone yaliyofichika.
 
Back
Top Bottom