ungonella wa ukweli
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 4,210
- 556
ukawa ni umoja wa wasaka tonge by zitto
Leo ndo ameona umuhimu wa kujiunga na wasaka tonge na madaraka?Kamwe hatutokaa kimya wasaliti wakiwa wanapanga kutuvuruga
Wananchi ndiyo wanaikataa ACT!Chadema wabaguzi sana kwanini wanaikataa ACT kujiunga ukawa kwani wao ndiyo wana hati miliki ya ukawa?
Mkuu tuliwaambia kuwa chadema wamezidi ubaguzi wao wanataka kupewa kila kitu hivi ulishaona wapi wao wanataka kutoa mgombea urais ,watoe waziri mkuu halafu Cuf eti watoe makamu wa rais lakini NCCR hawajapewa nafasi hata moja.
Lakini jambo baya zaidi wanataka majimbo ya dar yote waachiwe chadema sasa nani atakubali ujinga kama huo.
Mkuu tuliwaambia kuwa chadema wamezidi ubaguzi wao wanataka kupewa kila kitu hivi ulishaona wapi wao wanataka kutoa mgombea urais ,watoe waziri mkuu halafu Cuf eti watoe makamu wa rais lakini NCCR hawajapewa nafasi hata moja.
Lakini jambo baya zaidi wanataka majimbo ya dar yote waachiwe chadema sasa nani atakubali ujinga kama huo.
Usaliti unaanza kumtafuna taratibu sasa anataka kuungana na #WasakaTonge. UKAWA hatutafanya makosa ya kumkaribisha msaliti na wasaliti wenzie ambao nia na madhumuni yao makubwa ni kuisambaratisha CHADEMA. Wameona kuisambaratisha CHADEMA ni ndoto za alinacha sasa wanataka kuingia UKAWA ila wakavuruge mshikamano uliokuwepo. UKAWA hatutaki wasaliti wala hatutaki ayatullah.
Kitu gani maalum sana ACT wanakiona ni muhimu wakipate ndani ya UKAWA? Kwa mtazamo wangu bado ni chama kichanga kiumri na kinahitaji sana kujijenga ili kiwe na mfumo mzuri wa kisiasa na uendeshaji kabla ya kufikiria kujiunga kwenye ushirikiano wowote ule. Wanahitaji kujipambanua ndani ya jamii na Watanzania, wawe na mfumo na mtandao wa chama chao, waaminike na wawe na uwezo wa kuendesha mambo yao kwa kujisimamia wao wenyewe kwanza.
Kwa hisia za usaliti wanazotuhumiwa nazo na baadhi ya wanaUKAWA ni sababu tosha kuwa wanahitaji kushughulikia chama chao ili kuwaaminisha Watanzania kuwa yanayozungumzwa dhidi yao si sahihi hiyo itawasaidia kupata huruma ya Watanzania na pengine kuchaguliwa vyema wakati wa uchaguzi.
Binafsi sijashawishika kama wanayo dhamira ya kweli ya kuwa chama cha siasa, ukiachilia mbali harakati za mikutano waliyofanya hivi karibuni ambayo bahati nzuri ilipata nafasi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ukiondoa hilo ACT haijafanya sana katika siasa za upinzani. Kujiunga na UKAWA ni kujimeza na watakosa 'identity' kwani wao ni tofauti sana na hivyo vyama vingine kama CUF. NCCR, CDM ambavyo historia zao zinaeleweka na vimeshapitia misukosuko mingi ya kisiasa na NLD ambacho haina cha kupoteza katika umoja huo hata ukisambaratika.
Kukataliwa na CHADEMA ichukuliwe kama chachu ya kufanya kazi na kuondoa doa la usaliti inalotuhumiwa nalo, kung'ang'ania kutamaanisha kuwa hisia za usaliti zina ukweli. Hawakuwepo katika harakati za kuunda huo umoja hadi hapo ulipofika, sioni sababu kwa nini sasa walazimishe hata kama hawakubaliwi na mmoja tu kati ya waundaji wa UKAWA yaani CDM.
Ikumbukwe kuwa wenzao wameshafika mbali sana katika harakati za kuimarisha ushirikiano huo, inawezekana kuwakubalia wao itamaanisha kurudi nyuma hatua kadhaa na kulazimika kurekebisha baadhi ya taratibu za umoja wao. Nawashauri ACT wawaache wenzao waendelee na mipango yao.
Sitaki kuamini kuwa ACT haiwezi kufanya kazi bila UKAWA. Wakiendelea watasababisha UKAWA kutingishika na kusababisha mpasuko au mgawanyiko. Tuhuma zote zitawaangukia wao ACT na wataadhibiwa na Watanzania. Wajipambanue kama chama cha siasa ambacho kilisajiliwa ili kifanye siasa bila kutegemea nguvu ya kutoka nje ya wao wenyewe. Wasimame katika dhana ya kuwa wanaweza kuendesha siasa zao kama ilivyo kwa TLP, UDP na wengine ambao hawamo ndani ya UKAWA.
Mkuu wangu Ngongo , hebu tuambie lini CUF iliacha kuwa CCM B?
Hapo sasa, ndio maana wahenga walisema njia ya muongo ni fupi!
Chadema wanachekesha sana wanasema Zitto ni CCM wakati ndani ya UKAWA kuna mteule wa Mwenyekiti wa CCM, Mbatia.
Wakati huo wapo na CUF ambao ni washirika wa CCM.
Ukawa ni vituko vitupu.
Kila shetani na mbuyu wake zitto na mbowe watajuana wenyewe kivyao.
Kinachonishangaza wengi wa hawa wanaoshinikiza Zitto na chama chake wajiunge na UKAWA, ni watu ambao wamethibitika humu JF kuwa ni wana CCM damu.Wana Ukumbi,.
Katika gazeti la changamoto katika ukurasa wake wa kwanza unasomeka "Zitto azidi kuwaumiza CHADEMA" na habari hiyo ukiifuatilia ndani inaeleza kuhusu kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe na jinsi Zitto alivyoipokea.
Kwa mujibu wa gazeti hilo ni kwamba, Zitto hakutarajia mtu ambae yeye anamuheshimu katika siasa kuwa na misimamo isiyo tanguliza maslahi ya taifa mbele na badala yake kushikilia matatizo yao yaliyojitokeza huko nyuma ambayo kimsingi yalihusu nafasi za kiuongozi.
Zitto alieleza kuwa kwa sasa hayupo tayari kujibizana na viongozi tena kwa kuwa amekuwa akisema hivyo kila mahali anapokwenda kufanya mikutano yake na amewekeza nguvu nyingi katika kukitangaza chama chake kipya. Pamoja na malengo hayo, ila kwa kauli ile ya jana ameona hana budi kuitolea maelezo!
Zitto alisisitiza kuwa matatizo yake binafsi na viongozi wa chama chake cha zamani yasipewe kipaumbele kuliko maslahi ya taifa. Ameeleza kuwa mara kadhaa ameomba chama chake kijiunge na UKAWA lakini CHADEMA wamekuwa wakigoma. Kauli ile ya jana sio ngeni masikioni pangu. Alieleza Zitto.
Zitto aliongezea kuwa, "kama ni matatizo basi ni kati yangu na viongozi wa CHADEMA na yasifanywe ya taifa zima. ACT-Wazalendo tuna nia ya dhati ya kuwaondoa CCM madarakani. Pia UKAWA wana nia hiyo hiyo. Kwa hali hiyo hatuna budi kushirikiana kummaliza CCM na hilo litafanyika kama kweli tumetanguliza utaifa mbele badala ya matatizo yetu binafsi na viongozi wa chama changu cha zamani."
My Take,
Zitto amekomaa kisiasa na ana ngozi ngumu sana. Pamoja na mihasira ya Mbowe na maneno yake ya ovyo kuhusu Zitto kisa tu uenyekiti wa CHADEMA, lakini kijana Zitto amemjibu kistaarabu sana na bado ameonyesha nia ya kutaka ushirikiano na UKAWA. Kudos.
Teh teh teh Lipumba alimsaidia kikwete kwenda ilkulu leo agizo la ukawa cuf na nccr mliwakataa mchana kweupe kwamba ccm b leo kulikoni mshawahi kutangazia umma kwamba zile kauli sio za kweli ili tuwaelewe?
Chama kikiwa ndani ya UKAWA kimekuwa kipya. Ya kale yamepita, tazama, yamekuwa UKAWA.
Ndio maana hata Alliance for Cowards and Traitors aka Agizo la Chama Tawala (angalia mahali walipofanyia mkutano wao kule Arusha) nao wanataka kujiunga ili usaliti uwe umepita. Lakini kwa bahati mbaya hata huo ulaghai wa kujiunga ni ili wanaendeleze usaliti wao. Bado wako kazini. Hawataki ya kale yaishe bali wanataka wende nayo UKAWA. Wameshindwa! Nilishawaambia tangu awali kuwa hiyo (ACT) ngoma ya kitoto, haikeshi! Utaona.
Salama yao ACT ni kujiunga rasmi na hadharani (sio kufanya sirini) na Umoja wa Katiba ya Chenge (UKACHE) pamwe na wenzi wao CCM, TLP, UMD, nk.
Ukiona adui yako anaomba urafiki wa ghafla na wewe inabidi utafakari kwa jicho la nne kulikoni?
Shtuka!!
Zitto alinukuliwa akisema ACT iko tayari kujiunga na chama chochote ili mradi Umoja huo usiwe na malengo ya kugawana vyeo, lakini pia alitoa masharti kwamba lazima viendane na itikadi ya ACT. Nachujua mimi Ukawa havina sera za kijamaa. Ila nafahamu pia Zitto anaweza kuvishawishi vyama vya ADC, TLP, UPDP, DP, NRA, TFP, Jahazi Asilia, CCK kufuata itikadi ya kijamaa ili waungane pamoja