Zitto ni mnafiki na hapa anataka kucheza na akili za watanzania na ndiyo maana anakimbilia media ili kupiga yowe.
Mbele ya yote, nilitegemea kwanza atazungumzia kauli yake ya kusema 'UKAWA NI WASAKA TONGE", ilikuwa na maslahi gani kwa katiba ya nchi, kitu ambacho kingewapa UKAWA kuikubali nia anayotaka kuwaaminisha kwa sasa.
Zitto amekuwa msaliti wa CHADEMA tangu siku nyingi. Pamoja na kuonywa, bado akafanya mahusiano ya siri na ccm yenye kutakakufanikisha hujuma kwa CHADEMA kama chama. Leo anafunikaje hilo donda wakati linaozidi kuoza na linanuka, halfu ajibaraguze na kujifanya kana kwamba hakuna kilchowahi kutokea? Kama hatatui migogoro aliyoitengeneza kwa kiburi chake, dharau na ubinafisi, na anaiona ni haki yake tu kufaya aliyoyafanya, kuna tatizo gani kwa aliowajeruhi wakikubuka na ku doubt nia yake hata sasa?
Tangu afukuzwe CHADEMA, zito ameendeleza malumbano na hata kina kaijage kila wakati wanasema WANAPAMBANA NA CHADEMA. Na zitto akiwa kiongozi mkuu, hajawahi kusawazisha matamshi ya kaijage. Kwa nini CHADEMA waione wazi kwamba nyoka anatafuta tundu la kuingila tena kwenye nyumba?
Zitto amekuwa mwongo mwongo. Kitendo cha kusema aling'atuka CHADEMA wakati alifukuzwa. Na kuzidi kuhimiza alichokuwa anakifanya ndani ya chadema ni halalai ikiwa ni pamoja na kuanzisha chama kipya ACT akiwa ndani ya CHADEMA, ni dalilil tosha huyu kijana ana tabia chafu kwa asili. Sasa CHADEMA WALIMLEA HADI WALIPOMFIKISHA, AKAWATOLEA MAKUCHA YAKE (AMBAYO NINADHANI HATA KWENYE FAMILIA YALISHINDIKANA NDIYO MAANA "MAMA WA WATU", AKAWAKABIDH CHADEMA WAMLEE KIJANA WAKE)., Kwa kumfahamu ZITTO namna alivyo nyoka ndumila kuwili mbinafsi, penda sifa na uchonganishi, nini kitawafanya wamuone tofauti wakati hata yeye bado hajajitofautisha na matatizo aliyokuwa nayo mwanzo?
Sote tuliona kwenye Escrow alivyokuwa anajaribu kupulizia pulizia ili kujinafikisha kwa ccm. Baada ya kutoka CHaDEMA juzi amekamatwa anamawasiliano na viongozi wa ngazi za juu wa ccm yanayohusu kuiangamiza CHADEMA. Huu mtu leo CHADEMA wamkubali kwa mikono miwili bila matengenezo, watakuwa wenda wazimu.
UKAWA WANAPINGA KWA NGUVU ZOTE UFISADI NA WANAKUBALI KATIKA USAFI, UWAJIBIKAJI, NIDHAMU YA UTENDAJI NA WELEDI. ZITTO juzi juzi kamualika Lowasa fisadi wajiunge naye na amwachie hata nafasi ya ukuu wa chama ili agombee uraisi wa jamhuri. Hapa nia ya Zitto ni madaraka, sifa na vyeo, au ni kulikomboa taifa?
Anasema anataka kulikomboa taifa kutoka mifumo fisadi ya ccm wakati huo huo anashirikiana na hao mafisadi kuhujumu ukombozi wa kweli kiasi cha saa kutaka kuwashawishi watanzania waiweke nchi rehani kwa FISADI LOWASA.
KUNA SABABU GANI UKAWA WAMWAMINI ZITO AMA KUMUONA KAMA NI MWENZAO KATIKA UKOMBOZI? KAMA SIVYO, KWA NINI SASA WAWE WANAFIKI WA KUMKARIBISHA ILI WAONEKANE HAWANA UBAGUZI WAKATI KUMKARIBISHA NI KUDIDIMIZA UKOMBOZI WA TAIFA?
Ninashauri Zito ajiunge na Ccm.