Uchaguzi 2020 ACT-Wazalendo wamuunga mkono Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,913
2,000
RASMI: ACT-WAZALENDO YAMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CHADEMA

Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad ametangaza chama chao kumuidhinisha Mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu kuwa mgombea wao wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maalim Seif ameyasema hayo saa chache zilizopita akiwa kwenye Kampeni katika Jimbo la Donge.


4EA770C6-8A6A-450E-9572-0BAD5E2E0583.jpeg

438971F6-C07A-41D3-82D0-7D78C233B8F3.jpegMsemaji wa ACT-Wazalendo ameithibitishia JamiiForums kuwa huu ndio msimamo wa chama.

Mapema mwezi huu, Lissu alitangaza kumuunga mkono Maalim Seif akisema Chama cha ACT-Wazalendo kinaweza kuiondoa CCM madarakani visiwani Zanzibar

 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
5,349
2,000
Hadi sasa nilichogundua ni kuwa ACT na Chadema wana strategist ambao ni over extra smart. Ni dhahiri sasa CHADEMA NA ACT wamewaoutsmart CCM.

Mwaka huu Historia Kuu inaenda kuandikwa Tanzania.

Tundu Antiphas Lissu Raisi Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020 - 2025

Maalim Seif Raisi wa Zanzibar 2020- 2025.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
12,746
2,000
Sasa Membe kaleta upinzani wa kweli. Huu ndio upinzani tulikuwa tunataka sio ule ukinyimwa kugombea unajitoa. Upinzani wa Dr Slaa na Lipumba. Walipigania haki kwa muda mrefu lakini ilipokaribia kupatikana wakasaliti kati kubwa waliikwisha ifanaya kwa maslahi yao binafsi.

Sasa imani yangu inarejea kwa huyu kachero.

Let us expect huge things to happen very soon.

🔥🔥🔥🔥🔥🔥
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,344
2,000
JP Magufuli hatoachia urais kupitia sanduku la kura. Hivyo hivyo Zanzibar. Maalim Seif hatopewa urais.

Humu jamvini tunajifariji tu. Mwaka 1995 na 2015 bila shaka Wapinzani walishinda (Mrema & Lowassa) lakini hawakupewa Nchi. Maalim anashinda kila uchaguzi. Kwa wenye kumbukumbu kiduchu tu wanakumbuka walichofanya jeshi/TISS mwaka 2015 pale Zenji.... mchana kweupe!

Hii comment ntairudia early November 2020 baada ya NEC & ZEC kufanya yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom