PostGE2025 ACT- Wazalendo: Tusiingie kwenye uchaguzi tena bila Katiba mpya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo wanaendelea na ziara zao katika Mikoa ya Kusini ambapo jana Januari 7, 2026 Kiongozi wa Chama, Dorothy Semu, aliwasili katika Jimbo la Mtwara Mjini na kufanya kikao na uongozi wa jimbo hilo pamoja na waliokuwa wagombea wa udiwani katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2025. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Mangowela Inn uliopo Kata ya Chuno, Mtaa wa Ligula A.

Baadhi walitoa maoni wakiwasihi Viongozi wa Chama kuhakikishs wanapigania Katiba mpya kabla ya chaguzi zijazo.

Akiwahutubia viongozi hao, Semu alisema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi mkuu, akibainisha kuwa baadhi ya watu waliuawa na wengine kufanyiwa vitendo vya kikatili. Amesema hali hiyo imeacha alama mbaya katika historia ya uchaguzi nchini.

Alieleza pia kuwa ACT Wazalendo ilipitia mitihani mizito wakati wa uchaguzi ikiwemo kuenguliwa mgombea wao wa urais, Luhaga Mpina, kuondolewa kwa mawakala wa chama vituoni, na wagombea wa ubunge na udiwani kuenguliwa bila kufuata sheria. Semu amesema hata madiwani wa chama hicho walinyimwa haki ya msingi ya kula kiapo cha kuwa wakala.
Katika hotuba yake, amesisitiza kwa kusoma nukuu ifuatayo kama ilivyo:

"Ni wazi kabisa uchaguzi haukuwa huru, haki na kuaminika. Haki ya mwananchi iliporwa kuchagua viongozi wanaowataka

Ni fedheha kuona Samia Suluhu anashinda Kwa asilimia 98% hata wakati wa chama kimoja enzi za mwalimu haijawahi kutokea." amesema Semu

Semu alisema ACT Wazalendo itaendelea na hatua zake za kimapambano bila kukata tamaa, akieleza kuwa tume mbalimbali za uchunguzi na maridhiano zinazoundwa ni za “kiini macho.”

Alifafanua kuwa chama hicho tayari kimeonyesha njia ya namna ya kutoka katika mtanzuko wa kisiasa uliopo.

Vibweka vimeanza tena? Kwamba, wakati wengine wanawaambia wasiingie kwenye uchafuzi ule walikuwa hawasikii,hawaelewi au ilikuwa ni kiburi na ujuaji tu?Waache usanii.Wanawavizia watu wajae kwenye boksi tena ili wawatumie.Hao watu(ACT,CHAUMMA na wahuni wengine)hawaaminiki na ni wanafiki waliokubuhu.
 
Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo wanaendelea na ziara zao katika Mikoa ya Kusini ambapo jana Januari 7, 2026 Kiongozi wa Chama, Dorothy Semu, aliwasili katika Jimbo la Mtwara Mjini na kufanya kikao na uongozi wa jimbo hilo pamoja na waliokuwa wagombea wa udiwani katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2025. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Mangowela Inn uliopo Kata ya Chuno, Mtaa wa Ligula A.

Baadhi walitoa maoni wakiwasihi Viongozi wa Chama kuhakikishs wanapigania Katiba mpya kabla ya chaguzi zijazo.

Akiwahutubia viongozi hao, Semu alisema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi mkuu, akibainisha kuwa baadhi ya watu waliuawa na wengine kufanyiwa vitendo vya kikatili. Amesema hali hiyo imeacha alama mbaya katika historia ya uchaguzi nchini.

Alieleza pia kuwa ACT Wazalendo ilipitia mitihani mizito wakati wa uchaguzi ikiwemo kuenguliwa mgombea wao wa urais, Luhaga Mpina, kuondolewa kwa mawakala wa chama vituoni, na wagombea wa ubunge na udiwani kuenguliwa bila kufuata sheria. Semu amesema hata madiwani wa chama hicho walinyimwa haki ya msingi ya kula kiapo cha kuwa wakala.
Katika hotuba yake, amesisitiza kwa kusoma nukuu ifuatayo kama ilivyo:

"Ni wazi kabisa uchaguzi haukuwa huru, haki na kuaminika. Haki ya mwananchi iliporwa kuchagua viongozi wanaowataka

Ni fedheha kuona Samia Suluhu anashinda Kwa asilimia 98% hata wakati wa chama kimoja enzi za mwalimu haijawahi kutokea." amesema Semu

Semu alisema ACT Wazalendo itaendelea na hatua zake za kimapambano bila kukata tamaa, akieleza kuwa tume mbalimbali za uchunguzi na maridhiano zinazoundwa ni za “kiini macho.”

Alifafanua kuwa chama hicho tayari kimeonyesha njia ya namna ya kutoka katika mtanzuko wa kisiasa uliopo.

uchaguzi wa Tanzania hufanyika kila baada ya miaka mitano kwa mujibu wa katiba ya nchi. Hakipo cha kuzuia hilo lisifanyike kwa mujibu wa sheria.

porojo zingine ni kupoteza wakati tu na kutafuta kiki bu ni nonsense kabisa :HAhaa:
 
kwakua hakuna uchaguzi mpya au mdogo

TUSUBIRIE KESI YA KIGOMA MJINI tutaona kama hawatashiriki
 
uchaguzi wa Tanzania hufanyika kila baada ya miaka mitano kwa mujibu wa katiba ya nchi. Hakipo cha kuzuia hilo lisifanyike kwa mujibu wa sheria.

porojo zingine ni kupoteza wakati tu na kutafuta kiki bu ni nonsense kabisa :HAhaa:
Screenshot_20251230-124956~2.png
 
Back
Top Bottom