Pamoja na ufinyu wa barabara, kuna mapepo ya ajali hapo. Ushirikina haukwekepi katika jambo hili. Madreva huamua kuchua maamuzi ambayo kama amepona ukimuuliza kwanini alikuwa anaovateki kwenye kona au mlima anaweza kukupa jibu la ajabu sana.
Siku moja niliwahi kumuliza Mama yangu ambaye ni Pastor ni mchungaji na akasema kuwa kuna mashetani ay mapepo saa haya mambo sijui kama ni kweliCan somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?
Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.
Tembeleeni tovuti ya "Bobo" ina picha za ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri hasa Bongo.. na mnaweza kupata picha ya jinsi gani kuna mahali kuna tatizo ambalo linaweza kuelezeka kisayansi na kutatulika kwa kiasi kikubwa kisayansi.
Je.. tuanzishe kampeni ya kusajili upya madereva wote baadaya kutimiza defensive driving course? Yaani, tuanza moja tena na madereva wetu katika kampeni mpya ya kitaifa kwa sababu ukiondoa hizo ajali za sehemu kama Kibaha kuna hizi ajali ambazo zinatokana na "aggressiveness" ya watu kama kuchomekeana n.k hasa katikati ya jiji na miji.
Mkuu pamoja na kukaa na wazee, naamini bado kuwa barabara hii ni FINYU sana na bajeti ingetengwa ili barabara hii ipanuliwe kuanzia Chalinze! Hapo tutapunguza vifo vingi sana.
Nairobi wameweza kwa kiwango kikubwa kupanua barabara zinazoingia katikati ya Jiji, na mpaka sasa wanaendelea na upanuzi huo, sisi tunashindwa nini? Ni nini priorities za serikali yetu?
Kinachosikitisha, wanaendelea na ujenzi wa vibarabara finyu, na hivi vinatuingiza gharama pia tena kwa kubamizwa bei za kifisadi na makampuni yanayojenga vibarabara hivi uchwara!
si lazima uchangie au utoe comment kama hauna.
Wakuu, eneo la kuanzia Luguruni mpaka kibaha yenyewe, lina miteremko na milima kama nane hivi, barabara imetengenezwa bila kufuata safety issues, kuna kona kwenye miteremko kama minne hivi, Hata ni mambo ambayo yangeweza kuepukika. kwani waliotengeneza, waliofanya sijui umbembuzi yakinifu hawakuweza hata kutumia chembe ya busara, achilia mbali taaluma walizonazo.
Can somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?
Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.
Tembeleeni tovuti ya "Bobo" ina picha za ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri hasa Bongo.. na mnaweza kupata picha ya jinsi gani kuna mahali kuna tatizo ambalo linaweza kuelezeka kisayansi na kutatulika kwa kiasi kikubwa kisayansi.
Nakubaliana na wewe MKJJ kwa hii scientific approach to solving a nagging problem.
Suala la barabara kati ya DSM na Mlandizi linaanza kuwa na utata kutikana na sababu za kisayansi.
Naleta sababu kama tatu kuuMKJJ ukiondoa masuala ya uzembe wa madereva, gari kupata hitilafu za ghafla kama breki kufeli, ukweli unabakia pale pale kuwa barabara hii kipande cha DSM- Mlandizi sasa hivi kimepitwa na wakati na ni vyema tukaanza kuipanua au kama ambavyo serikali imeanza, kujenga barabara mbadala kama ya Bagamoyo-Msata.
- Barabara ni FINYU SANA na kila maboresho ya barabara hii yana kumbwa na kelele kubwa za fidia toka kwa wananchi, kitu ambacho kinanyima fursa ya hata kuwa na 4 lane 2way highway.Tukumbuke kuwa hiki kipande ndio mlango mkubwa kuliko yote nchini kuingia jijini DSM
- TOPOGRAPHY-cheki miinuko na mabonde toka Kimara hadi Mlandizi. Maboresho yote yamekwepa kukata vilima na kujaza mabonde katika juhudi za kukwepa gharama.Sasa hivi kuna vikona vya ajabu na vimiinuko/vimteremko vya kuudhi hasa kwa magari makubwa, bila kuongeza upana wa barabara kama ilivyo Chalinze -Morogoro(3lane,2 way)
- Kutokana na kuboreka kwa teknolojia ya magari, mengi yanabeba mizigo mikubwa zaidi na hata madogo yanakwenda spidi kubwa zaidi , hivyo kuongeza uwezekano zaidi wa kuwa na ajali, tena mbaya zaidi.(severity of accidents increase with better roads)
Naomba kutoa hoja!!!!
Asilimia kubwa ya ajali zinasababishwa na ovateki mahali pasipostahili, madereva wengi wanaovateki mahali popote iwe kwenye mlima, kona kali nk...Ajali ya jana ilisababishwa na lori lilikuwa linaovateki likakutana na ile hiace.
Ajari nyingi zinazotokea Tanzania ni za kisayansi. Kuna vitu vingi sana ambavyo ni vya msingi vinakiukwa na watumiaji wa barabara. Mfano: Ukiendesha gari mida ya alfajiri sana (kama saa 9 - 10 hivi) ukitokuelekea Ubungo kwenda Morogoro utakutana na Magari mengi yamewasha full light na kwa uzoefu wangu nimekuwa sioni kabisa mbele ninapopishana na magari ya jinsi hiyo na mengi huwa ni daladala (hiace) na gari ndogo (taxi kwa jina lililozoeleka). Watumiaji hawa hata kama utawaomba wapunguze taa huwa hawa hitikii maombi yako.
Wataalamu wa masuala ya ujenzi wa barabara, wanajua kuwa wakati wanafanya usanifu na ujenzi kuna vitu wanavyotegemea mtumiaji wa barabara awe anavijua na kuvifuata. Watanzania wengi hatutaki kufuata taratibu hizo. Watu wengi na hasa wanasiasa wetu wanapiga kelele kwa matatizo mengine madogo madogo yasiyo na msingi kama kona mbaya, uchawi, tunaiomba serikali ifanye bur buraa!, serikali mbovu n.k
Elimu ya watumia barabara inatakiwaa sana lakini inatolewa kwa usahihi kabisa na wadau mbalimbali kwani ni elimu ya msingi kabisa katika matumizi ya barabara (basic education) ambayo unaweza kuzaliwa nayo pia (yaani kutumia akili na utashi wako kujua.. mfano siyo lazima ufundishwe kuwa kulipita gari (overtake) kwenye kona usiyoona unaweza kusababisha ajari). Ninaamini kuwa tukiwajibika kwa pamoja na kujari taratibu, kanuni na sheria za matumizi ya barabara ajari hizi zitapungua sana.
Matatizo mengine ni ya teknolojia. Teknolojia inabadilika kwa haraka sana. Sasa hivi kuna magari yanaweza kukimbia spidi ya 250 km/saa n.k wakati miundo mbinu yetu in design speed ya 80 km/h.
The problem there is simple and clear.... horizontal curve imeunganishwa na vertical curve bila kuwa na transition curve. Ukiona jinsi magari yanavyoanguka eneo hilo utajua kabisa from basics of physics kuwa ni centrifugal forces ndo inayatoa barabarani.
Teknolojia iliyojenga ile barabara ilikuwa ni ya mwaka 1975 na hivi leo tuko 2010. Wataalamu wetu tulionao wanajua kufanya routine maintenance, periodic maintenance na spot improvement tu lakini hawawezi kuangalia mabadiliko haya ya kiteknolojia na philosophia mpya za ujenzi wa miundo mbinu.