Abood bado hawajabadilika hadi sasa

Abood bado hawajabadilika hadi sasa

Abood ni basi la kiswahili sana Tena sana,inabidi ulizoee tu. Pia wafanyakazi wake kila mmoja ana nguvu kama vile hakuna management. Yeye analeta mabus tu lakini wafanyakazi ndio wanayoendesha.

Abood zote lazima mjazane ndani ya gari ndio wanaondoka.
Halina uzungu wala maajabu yoyote.
 
Gari imegoma kuwaka hata wslipoweks mafuta ya kidebe

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hii gari takataka kabisa
JPEG_20230218_181237_3205908449080894142.jpg


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Na hapo bado mkifika Morogoro mnapelekwa Yard yao
 
Kuna mwaka niliwahi kupanda hilo basi kutoka Mbeya kwenda Morogoro! Ile tuko maeneo ya Melela kwa mbele, si mafuta yakaisha!!

Tulilazimika kusubiri mpaka gari yao ya patrol itoke Morogoro kuja kutuwekea mafuta, ndipo tukaondoka! Achilia mbali kila unapopanda gari zao za Mikoani, ni lazima muingie kwenye karakana yao kule mjini kati, ndipo muendelee na safari.

Mimi Abood napanda pale ninapokosa basi lingine. Kinyume na hapo, hapana aisee.
Hawaweki mafuta kwy Petrol Station ya mtu ila ya kwao tu Moro na Dar ndiyo maana wakiishiwa mafuta wanasubiri hadi gari la patrol lifike. Wako kama Wapemba ambao hawanunui bidhaa duka lisilo la Mpemba.

Shabiby ana Petrol Station yake na Hoteli yake.

BM ana Petrol Station yake.

Abood ana Petrol Station yake.

Msukuma kule Kanda ya Ziwa ana Petrol Station yake kwa ajili ya mabasi yake 50.

Check and balance hakuna.

Ma-RTOs nchi nzima wanayaogopa mabasi hayo ya wanasiasa. Ukiwapelekea kesi hupati msaada wala ushirikiano.

Ombeni MUNGU ampe mama nguvu za kumalizia SGR ndiyo mwarobaini wao na ndiyo mtajuwa JPM alikuwa proactive.
 
Wakuu habari za asubuhi

Abood ameleta mabasi mengi tu lakini hadi sasa hawataki kubadilika na tabia zao za ajabu ajabu.
Leo na safiri na Bus lao la Abood kutoka Tunduma kwenda Dar lakini cha kushangaza linabeba abiria Kama daradara njiani gari imejaa lakini konda bado anapakia watu njiani viti vyote vimejaa Hadi watu wengine wamekaa kwenye korido na wengine wamesimama.

Lakini pia siti uliyokatiwa ticket siajabu usikae unaambiwa kaa popote pale mjiriekebishe

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo mkuu umeamua kunichomea ugali wangu kwa mabosi😓
 
Dar to mwz gari ni ally's star tu ndo unafika kwa wakati
 
Halina uzungu wala maajabu yoyote.
Kuna mdau kasema inawezekana wafanyakazi hawalipwi, naweza kukubali swala. Limekua kama daladala yaaani dereva,makonda,vishoka wote wanapeleka hesabu kwa boss tu ila mishe zote wanafanya wao kuanzia mafuta mpaka kujilipa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom