Huyu nadhan Mabus yake yashazoea uswahili, nimepanda gar la Mwanza tokea Morogoro, ilibidi nicheke vadala ya kukasirika, inasimama kila kituo hadi inauliza watu nyiee mnaenda ilihal hao watu wamebeba majembe wanaonekana wakienda zao shba kabisa.
Haya gari liko full ila as long kuna abiria anataka kupanda atapandiswa,
Kila stendi ya iwe ya kijiji, wilaya au mkoa itaingia, Stendi ya Gairo ikaingia ikakusanya wauza karanga za kuchemsha na wengineo ikawa hata pa kupumlia hamna,
Likafika Mbande stendi likaingia,
Kibaigwa stendi likaingia,
Nikasema hili Mwanza litatembeea week njiani,
Ikabidi nishuke tu njian nikaanzisha shuguli nyingine ku-buy time ili nipange safari nyingine upya na silu nyingine