Abood bado hawajabadilika hadi sasa

Abood bado hawajabadilika hadi sasa

Abood ni basi la kiswahili sana Tena sana,inabidi ulizoee tu. Pia wafanyakazi wake kila mmoja ana nguvu kama vile hakuna management. Yeye analeta mabus tu lakini wafanyakazi ndio wanayoendesha.

Abood zote lazima mjazane ndani ya gari ndio wanaondoka.
🤣🤣🤣🤣😂😂😂🤣🤣😂😂😂😂🤣🤣🤣😂😂😂😂
 
Ninachokiona mamlaka ya kusimamia walaji haifanyi kazi zake sawa sawa.
 
Kuna basi linaitwa Tembo safari, linatokea Dar, walinitapeli kwa kuniambia linafika Kigoma kumbe linaishia Kahama. Wakaniandikia ticket ya Kigoma , tulipofika Kahama konda akanikimbia.

Mbaya zaidi nilikuwa na mizigo na wamenitoza nauli yake Hadi Kigoma. Polisi wa pale stendi ya kahama nao hawana maana. Badala ya kunisaidia wananiomba rushwa
Gari za uhakika zinazojulikana zinaenda kigoma na hautaapata usumbufu ni Adventure na Saratoga tu.
 
Kuna mwaka niliwahi kupanda hilo basi kutoka Mbeya kwenda Morogoro! Ile tuko maeneo ya Melela kwa mbele, si mafuta yakaisha!!

Tulilazimika kusubiri mpaka gari yao ya patrol itoke Morogoro kuja kutuwekea mafuta, ndipo tukaondoka! Achilia mbali kila unapopanda gari zao za Mikoani, ni lazima muingie kwenye karakana yao kule mjini kati, ndipo muendelee na safari.

Mimi Abood napanda pale ninapokosa basi lingine. Kinyume na hapo, hapana aisee.
 
Abood ni basi la kiswahili sana Tena sana,inabidi ulizoee tu. Pia wafanyakazi wake kila mmoja ana nguvu kama vile hakuna management. Yeye analeta mabus tu lakini wafanyakazi ndio wanayoendesha.

Abood zote lazima mjazane ndani ya gari ndio wanaondoka.
Unachosema nakubaliana nawe mkuu ni waswahili haswa. Wiki iliyopita nilichelewa kidogo bus zile za saa 12 asubuhi nilikuta zishatoka, jamaa akanilengesha bus la Abood linalokuja Iringa ilhali mi naenda Mbeya wakaniambia watanifaurishia Iringa.

Wakanipiga hela ndefu lakini sikujali as long as nitafika Mbeya swadaka. Aisee tulikaa toka saa moja ile mpaka saa nne kasoro, abiria tukamaindi sana ndio wakaamua walitoe lilipopark na kulipeleka kwa mabus ya Moro ili kuongezea abiria ili liondoke. So Kama abiria tusingekomaa bhasi lingeendelea kutega tu pale sheinzy.😬

Kimbembe sasa tulipofika gereji yao pale Moro, washenzi walituwekesha pale mpaka abiria mmoja akashuka kwenda kumkwida dereva ndio akalitoa na kuanza safari. Siisahau hii safari tunaingia Iringa stand saa moja kasoro na kufaulishwa bus la Mbeya na kuingia saa nane usiku.

Abood siwahitaji tena maishani mwangu hata mbadirike vipi.😬😬🙌
 
Unachosema nakubaliana nawe mkuu ni waswahili haswa. Wiki iliyopita nilichelewa kidogo bus zile za saa 12 asubuhi nilikuta zishatoka, jamaa akanilengesha bus la Abood linalokuja Iringa ilhali mi naenda Mbeya wakaniambia watanifaurishia Iringa. Wakanipiga hela ndefu lakini sikujali as long as nitafika Mbeya swadaka. Aisee tulikaa toka saa moja ile mpaka saa nne kasoro, abiria tukamaindi sana ndio wakaamua walitoe lilipopark na kulipeleka kwa mabus ya Moro ili kuongezea abiria ili liondoke. So Kama abiria tusingekomaa bhasi lingeendelea kutega tu pale sheinzy.😬
Kimbembe sasa tulipofika gereji yao pale Moro, washenzi walituwekesha pale mpaka abiria mmoja akashuka kwenda kumkwida dereva ndio akalitoa na kuanza safari. Siisahau hii safari tunaingia Iringa stand saa moja kasoro na kufaulishwa bus la Mbeya na kuingia saa nane usiku.
Abood siwahitaji tena maishani mwangu hata mbadirike vipi.😬😬🙌
Kumbe ndo Mana abood zilikuwa zinapita singida sa mbili night uelekeo mwanza from dar
 
Kumbe ndo Mana abood zilikuwa zinapita singida sa mbili night uelekeo mwanza from dar
Wanachelewa sana kutoka pale Magufuri stand mkuu. Wajinga sana hawa, wamekuwa kama daradara mpaka wajaze ndio liondoke. Yale mambo ya time management ukifika muda wa saa 12 au saa moja kamili linaondoka hawana sikuhizi.
 
Kuna basi linaitwa Tembo safari, linatokea Dar, walinitapeli kwa kuniambia linafika Kigoma kumbe linaishia Kahama. Wakaniandikia ticket ya Kigoma , tulipofika Kahama konda akanikimbia.

Mbaya zaidi nilikuwa na mizigo na wamenitoza nauli yake Hadi Kigoma. Polisi wa pale stendi ya kahama nao hawana maana. Badala ya kunisaidia wananiomba rushwa
Polisi dawa yao ni kumpigia mkubwa wao tu
 
Wanachelewa sana kutoka pale Magufuri stand mkuu. Wajinga sana hawa, wamekuwa kama daradara mpaka wajaze ndio liondoke. Yale mambo ya time management ukifika muda wa saa 12 au saa moja kamili linaondoka hawana sikuhizi.
Vituo vingi Sana .. Bora bus masaa ya mbele halina muda wa kupoteza hapo stand sa 12 kamili linachomoka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom