Abiria wa Mwendokasi tuliotakiwa kutoka Kivukoni kwenda Kimara, Dereva katupeleka Morocco kisha akaturudisha Kivukoni

Kwa hali ilivyo mwendokasi (Kivukoni - Kimara) Bora mwingereza angebami kututawala tuu. Labda tungefika mbali. Hali ni mbaya kuliko
Hicho ni kipimo kwa watawala. Manake hapo ni karibu na Ikulu kwa watu wa kivukoni.

Hakukuwa na haja ya kuagiza ndege wakati huku chini makabwela wengi wanateseka kwa usafiri wa mwendokasi. Hesabu za wapi hizo?
.
Ambao hao makabwela kesho unategemea wakupe kura
 
Jana Machi 26, 2024 nikiwa kwenye Kituo cha Mwendokasi cha Kivukoni, kulikuwa na nyomi la hatari mida ya jioni, mabasi mengi yalikuwa yamepaki pembeni na machache yaliyokuja hayakukidhi haja ya huduma iliyotakiwa kutolewa.

Watu walikuwa wengi na wengine wakionekana wanataka kuwahi kwenda kupata futari.

Tukiwa katika hali hiyo, Saa 1:00 Usiku likaja basi kushusha abiria Namba zake za usajili T 591 DWR, baada ya kumaliza kala halijaanza utaratibu wa kuja pale tulipokuwa tumepanga foleni ya kwenda Kimara, Dereva wa Basi hilo akaanza kupandisha Wafanyakazi wenzake na baadhi ya Walemavu.

Wakati akifanya hivyo idadi ya aliokuwa akiwapandisha ni kubwa, ikabidhi watu waanze kuvamia nao waingie bila kufuata utaratibu, nami nikachoma ndani.

Dereva akatutaka tushuke, watu tukakaza, kaona sasa atukomeshe, badala ya Kwenda Kimara akatupeleka Morocco, huko napo watu wakakaza kushuka, eti alitaka tushuke pale.

Baada ya ubishi wa muda mrefu akachoma mafuta akaturudisha Kivukoni, huko napo abiria wakakaza, akaja Msimamizi wake, naye badala atumie busara, akaanz kutuambia “Nyie si mnajifanya vichaa, sasa sisi vicha zaidi yenu, leo mtalala hapohapo.”

Kulikuwa na vijana na madogo kibao wanafunzi wakaanza kuimba nyimbo kama vile wanaandamana.

Ndipo kuna mtu mzima mmoja nikaona ameshika simu akampigia Waziri Mohammed Mchengerwa, akamweleza kinachoendelea, kwanza Waziri hakuamini, akamwambia apige picha au arekodi video amtumie, yule mdingi akafanya hivyo.

Ndipo baadaye nasikia huyu bosi mpya wa Mwendokasi naye akapiga simu na kusema anakuja eneo la tukio, kusikia hivyo yule supervisor na dereva wake wakasepa, wakaona msala huo.

Tukapata dereva mwingine safari ya kuondoka Kivukoni ikaanza Saa 3:25 Usiku, tukafika Kimara almost saa Nne usiku.

Imagine tumekata tiketi Saa 12 Jioni kisha tunafika Kimara Saa Usiku.

Hawa madereva wa Mwendokasi nadhani wanatakiwa kuangaliwa saikolojia ya akili yao, pia huduma kwa ujumla za Mwendokasi ni janga.

Serikali ina kazi kubwa ya kufanya katika huu mradi.

Majibu ya DART - DART kuchukua hatua dhidi ya Dereva na Wasimamizi wa Mwendokasi waliowapeleka Abiria Morocco badala ya Kimara
Hawana hasara hao mshaharA wao mwisho wa mwezi
 
mara ya mwisho kupanda
nilikua msimbazi nmekaa wee nkaona niunge unge usafiri likaja la morocco nikapanda nikajua nashukia mapipa. La haulaa! Naona kitu kinachoma muhimbili nililaani sana
 
Jana Machi 26, 2024 nikiwa kwenye Kituo cha Mwendokasi cha Kivukoni, kulikuwa na nyomi la hatari mida ya jioni, mabasi mengi yalikuwa yamepaki pembeni na machache yaliyokuja hayakukidhi haja ya huduma iliyotakiwa kutolewa.

Watu walikuwa wengi na wengine wakionekana wanataka kuwahi kwenda kupata futari.

Tukiwa katika hali hiyo, Saa 1:00 Usiku likaja basi kushusha abiria Namba zake za usajili T 591 DWR, baada ya kumaliza kala halijaanza utaratibu wa kuja pale tulipokuwa tumepanga foleni ya kwenda Kimara, Dereva wa Basi hilo akaanza kupandisha Wafanyakazi wenzake na baadhi ya Walemavu.

Wakati akifanya hivyo idadi ya aliokuwa akiwapandisha ni kubwa, ikabidhi watu waanze kuvamia nao waingie bila kufuata utaratibu, nami nikachoma ndani.

Dereva akatutaka tushuke, watu tukakaza, kaona sasa atukomeshe, badala ya Kwenda Kimara akatupeleka Morocco, huko napo watu wakakaza kushuka, eti alitaka tushuke pale.

Baada ya ubishi wa muda mrefu akachoma mafuta akaturudisha Kivukoni, huko napo abiria wakakaza, akaja Msimamizi wake, naye badala atumie busara, akaanz kutuambia “Nyie si mnajifanya vichaa, sasa sisi vicha zaidi yenu, leo mtalala hapohapo.”

Kulikuwa na vijana na madogo kibao wanafunzi wakaanza kuimba nyimbo kama vile wanaandamana.

Ndipo kuna mtu mzima mmoja nikaona ameshika simu akampigia Waziri Mohammed Mchengerwa, akamweleza kinachoendelea, kwanza Waziri hakuamini, akamwambia apige picha au arekodi video amtumie, yule mdingi akafanya hivyo.

Ndipo baadaye nasikia huyu bosi mpya wa Mwendokasi naye akapiga simu na kusema anakuja eneo la tukio, kusikia hivyo yule supervisor na dereva wake wakasepa, wakaona msala huo.

Tukapata dereva mwingine safari ya kuondoka Kivukoni ikaanza Saa 3:25 Usiku, tukafika Kimara almost saa Nne usiku.

Imagine tumekata tiketi Saa 12 Jioni kisha tunafika Kimara Saa Usiku.

Hawa madereva wa Mwendokasi nadhani wanatakiwa kuangaliwa saikolojia ya akili yao, pia huduma kwa ujumla za Mwendokasi ni janga.

Serikali ina kazi kubwa ya kufanya katika huu mradi.

Majibu ya DART - DART kuchukua hatua dhidi ya Dereva na Wasimamizi wa Mwendokasi waliowapeleka Abiria Morocco badala ya Kimara
Shida hizi kazi wanazipata kwa connection
 
TUNAMSHUKURU SANA MAMA, KWA KITENDO CHA MZEE KUPIGA SIMU KWA WAZIRI.
 
Sie wa mikoani mwanzoni tulikua tukisikia mwendo kasi tulikua tunatamani sana,nakumbuka siku moja nashuka pale magufuli bus stand..nikasema ngoja leo nijaribu nione yaliyomo yamo..dah nilijuta! Ni usafiri wa hovyo sana!
 
Madereva wa mwendokasi ni wababe sana,majuzi abiria walisema tumejaa tunaumia usipandishe wengine,dereva akaona akisimama wengine watapanda akawa hasimami vituoni na hakuwarudisha abiria
 
Back
Top Bottom