Abiria unachelewaje Ndege (check-in) Airport?

Abiria unachelewaje Ndege (check-in) Airport?

Uuwiiii! Mi mnyamwezi wa watu nitatia aibu siku hiyo ya safari yangu kwa Obama,sasa hizo check-in, sijui ma-boarding gates...sasa kama hawaandiki popote utajuaje kuwa unatakiwa utumie gate flani ili uende check-in sijui nyingine...hapo inakuwaje kwa mgeni,utafaham vipi hiyo issue

Unaunganishia wapi mkuu.........?.......lete uwanja upewe ramani..........
 
ndege inapaswa kuwa kama usafiri wa bajaj yaani ukitaka hata kwenda moro si kutumia masaa 3 njiani fasta tu dakika 20 ushafika moro
 
infact serikali inapaswa kupelekwa mahakamani kwa kuangamiza watu kwa ajali za mabasi na kufanya gharama za usafiri wa anga ghali
 
Kwa nchi hii hakuna cha kushangaa hapo

-mara foleni isiyo na kichwa wala miguu na trafick anaita upande autakao nusu saa!!

-mara umepitia ATM ya kwanza no network ATM ya pili kakadi kamemezwa na upo na Taxi Unadaiwa! Vi m-pesa vimefungwa na driver anataka cash

-masurufu yenyewe umeingiziwa asubuhi na bado hujatoa uache pesa ya mboga nyumbani

-ulipita benki na mama harakaharaka mkagawane chochote halafu akusindikize ile kutoka nje gari imepigwa lock na Parking System sijui YONO

Umemuachia msala wife unakwea boxer hufiki popote inadakwa na madalali sijui

Unarudi kwenye taxi mnazunguka wee mara tazara mchicha mara vingunguti mara kinyerezi mara mkamatwe service rd na ukimwambia askari shida yako huku ukimuonyesha tiketi anasema ungetaka kuwahi ungeondoka jana!! Wakati safari yenyewe umeioata asubuhi!! hadi ufike airport hoii na kadirisha kamefungwa

Labda kama unazungumzia mikoani lakini kwa Dar basi hiyo safari uwe uliipanga miezi mitatu iliyopita

Duh! haaa haaa bongo raha sanaaaaa.
 
ndege inapaswa kuwa kama usafiri wa bajaj yaani ukitaka hata kwenda moro si kutumia masaa 3 njiani fasta tu dakika 20 ushafika moro

Sasa kama sijui airport unakaa masaa mawili si sawa tu na basi kwa safari ya Moro
 
Unayemsema mwenza kuchelewa kwa mji huu ujue hayajakukuta na ipo siku utajua
 
wadada ndo zao kujizungusha mwanzo mwisho mara kajisahaulisha wanja, sijui pafyumu, skin taiti ya kuvaa ukweni basi vurugu tupu mpaka mnachelewa ndege na ukute nauli umelipiwa
 
Ndege kwa nchi zetu za dunia ya tatu si bahati tu bali ni jambo la Sifa na kukuza nafasi (status) yako kwenye jamii husika, wengine hutumia katika mitongozo.
 
Ujuaji wa wabongo eti waonekane wanajua kudai haki!
 
yaani inaboa sana kwa kweli unakuta mtu umetegea tiket za promosheni za fastjet sasa kulipia tena bei inakua juu mno
 
Back
Top Bottom