Kuna rafiki yangu aliwahi kukoswakoswa kuchelewa ndege tena siyo kwa masaa tu machache bali karibu siku nzima, siwezi kusema ni uzembe au ujinga, badala yake naweza kusema ilikuwa ni kwa sababu ya utofauti wa masaa kwa kizungu na kikwetu(Kiswahili).
Ilikuwa hivi; yeye ticket ya ilikuwa imeandikwa safari ni ijumaa saa 7 usiku yaani (departure Friday 1am) Maana yake ilitakiwa aende Airport siku ya Alhamisi walau saa4 usiku ili saa tano usiku aanze ku check in.
Yule jamaa ilifika around saa4:30 usiku akapigiwa simu na rafiki yake, “oya kamanda umeshafika Airport?” Jamaa, “mwanangu nilikwambia safari ni kesho saa7 usiku”. Mabishano yakaanza lakini jamaa akaona arudie tena kusoma ticket na kucheki mtandaoni kwenye booking status. Heeeeeh jamaa anaona check in imeshafunguliwa, kidogo achanganyikiwe. Thank God at the end alifanikiwa kufika airport kwa mda na aka check in vema na akasafiri.
Guess what? Ilikuwa tr 24 September 2015 kwa mara ya kwanza jamaa anaenda Switzerland kwa ajili ya masomo.