Abiria unachelewaje Ndege (check-in) Airport?

Abiria unachelewaje Ndege (check-in) Airport?

and 998 others

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
28,225
Reaction score
39,705
Wewe abiria unajua kabisa kesho nasafiri muda fulani na ninatakiwa reporting time airport masaa 2 kabla lakini cha ajabu unajichelewesha mpaka ndege inakuacha.

Tiketi yenyewe umelipiwa ukishachelewa sasa ni kuanza usumbufu kwa aliyekulipia eti akulipie tiketi nyingine.

Not fair hasa wadada.

Wewe abiria unajua kabisa kesho nasafiri muda fUlani na ninatakiwa reporting time airport masaa 2 kabla lakin cha ajabu unajichelewesha mpaka ndege inakuacha. Tiketi yenyewe umelipiwa ukishachelewa sasa ni kuanza usunbufu kwa aliyekulipia eti akulipie tiketi nyingine. NOT FAIR hasa wadada

Sasa Kama Ndiyo Kwanza Nimetoka Kijijini Kwetu KYAKA NKUNDE Jana Tu Na Leo Nasafirishwa Kwenda India Kutibiwa Moyo Unadhani Sitochelewa Kweli? Kusafiri Na Mbung'o ( Ndege ) Ni Habari Nyingine Mkuu Haswa Ukiwa MLUGALUGA Lazima Tu Utaachwa au Kuchelewa Unless Kuna Mtu Anakupeleka!
 
Kwa kifupi nakubaliana kabisa na uzembe - aidha uzembe wa anayesafiri au wale wanaomzunguka. Safari yoyote inataka good planning ambayo ni rahisi kuitekeleza, pia 'time management' skill. Ukisahau kitu hakuna kurudi, utanunua huko uendako na kuhesabu hasara kwako.
 
Foleni haiwez kuwa sababu stahiki ya kuchelewa. Si ulijua muda wa kureport ni masaa 2 kabla?
 
Foleni, kusahau passport so you have to rush back home. Ni jambo la kawaida especially kama unasafiri mara kwa mara. Kitoka ofisini mbio kuelekea airport

Muhimu sana hasa hapo kwenye "kama ni msafiri wa mara kwa mara..."
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana, siku ya kwanza kuachwa nililia balaa, nilipiga mayowe utadhani nimefiwa na wazazi, ilibidi wale customer care staff swissport watumie muda mwingi kunituliza, ilikuwa the first time naenda nje ya Africa, dah, kitu emirates kikasepa kikaniacha.

Nilikuwa naona soo hata kurudi home, japokuwa nilisafiri the next day. Aisee, kumi na mbili kamili alfajiri nilikuwa tayari airport kwa safari ya saa kumi unusu jioni.

Dah nikikumbuka huwa nacheka mwenyewe, yaani airport ilisimama kwa mshangao wa kilio changu but kidume mpaka leo hii nimeshapata masomo ya kutosha kuhusu usafiri wa anga.
 
Kwa kifupi nakubaliana kabisa na uzembe - aidha uzembe wa anayesafiri au wale wanaomzunguka. Safari yoyote inataka good planning ambayo ni rahisi kuitekeleza, pia 'time management' skill. Ukisahau kitu hakuna kurudi, utanunua huko uendako na kuhesabu hasara kwako.

Wewe umenena point tamu kuliko zote
 
Sasa Kama Ndiyo Kwanza Nimetoka Kijijini Kwetu KYAKA NKUNDE Jana Tu Na Leo Nasafirishwa Kwenda India Kutibiwa Moyo Unadhani Sitochelewa Kweli? Kusafiri Na Mbung'o ( Ndege ) Ni Habari Nyingine Mkuu Haswa Ukiwa MLUGALUGA Lazima Tu Utaachwa au Kuchelewa Unless Kuna Mtu Anakupeleka!

Hata kama ni mluga luga unatakiwa kujua kusoma kama hujui basi uzembe ni kwa wanaokuongoza ili usafiri. Tena mlugaluga ndo atakuwa muoga awahi hata masaa 5 kabla
 
Back
Top Bottom