Mkuu umenikumbusha mbali sana, siku ya kwanza kuachwa nililia balaa, nilipiga mayowe utadhani nimefiwa na wazazi, ilibidi wale customer care staff swissport watumie muda mwingi kunituliza, ilikuwa the first time naenda nje ya Africa, dah, kitu emirates kikasepa kikaniacha.
Nilikuwa naona soo hata kurudi home, japokuwa nilisafiri the next day. Aisee, kumi na mbili kamili alfajiri nilikuwa tayari airport kwa safari ya saa kumi unusu jioni.
Dah nikikumbuka huwa nacheka mwenyewe, yaani airport ilisimama kwa mshangao wa kilio changu but kidume mpaka leo hii nimeshapata masomo ya kutosha kuhusu usafiri wa anga.