Abdalah Zombe: CHADEMA wakiongoza nchi nitajinyonga, adai Lema alikuwa mwizi wa magari!

Watani zangu kule Tarime wanavuta ile kitu ya jamaica iwasaidie kuwa mashujaa, sasa na huyu jamaa inampeleka kubaya, tukae na tusubiri tuone mwisho wake.
Akijinyonga hatazikwa kama Ditto akae akijua, watu siku hiyo watafanya party kubwa - (quarters zote za polisi dar nzima siku hiyo chereko.)
 
huyo hata akijinyonga sawa, maana taifa litapata faida kwa kuwa hana faida kwa taifa hili zaidi ya ule uuaji wake
 
Mbona hata mimi sikuona mahali alipotajwa? bila shaka maruweruwe yamemuanza, damu ya mtu si mchezo ati!
 
hii ndiyo hotuba anayotaka kujiulia ZOMBE duh naona jamaa hata kishwali sasa hajui tuna kaisha poteza channel soma kwenye RED kwa makini kweli sasa CHADEMA ni tishio la uovu huyu jamaa kesi yake ichunguvye tena kunatatizo hawe kuamaki hivyo bila sababu

MAUAJI YA RAIA WASIO NA HATIA

Mheshimiwa Spika
, wakati viongozi wa serikali yetu na wapambe wao wakidai majukwaani, na kwa sauti kubwa, kwamba Tanzania ni nchi ya amani na utulivu, serikali hiyo hiyo kwa kutumia Jeshi lake la Polisi na vyombo vingine vya usalama imekuwa mstari wa mbele kuua raia wasiokuwa na hatia wanapodai haki zao.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii inayohubiri amani kila kukicha, kwa kutumia vyombo vyake vya mabavu, imekuwa inakamata wananchi wasiokuwa na hatia na kuwabambikizia kesi za uwongo pale wanaposhindwa kutoa rushwa katika vituo vya polisi na mahakamani. Watawala hawa, wanaopenda kujidai kwamba mamlaka yao imetoka kwa Mungu na kwa hiyo iheshimiwe, wamekuwa wanatesa wananchi wetu katika vituo vya polisi na magerezani kinyume na sheria za Tanzania na hata za kimataifa.

Mheshimiwa Spika, licha ya maovu yote haya wanayotendewa, Watanzania hawajachukua silaha kujitetea. Hata hivyo, ‘utulivu’ huu hauwezi kuitwa amani, maana amani si uwepo wa ukatili bali ni uwepo wa haki kama tafsiri sahihi ya Dr. Martin Luther King, Jr ilivyosema

Mheshimiwa Spika, Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), imeeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2010 peke yake, watu 52walikufa wakiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama. Kati ya wote waliouawa, watu 10 waliuawa na Jeshi la Polisi katika maeneo ya Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Nyamongo wilayani Tarime peke yake.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika kipindi cha miezi mitano ya mwanzo ya mwaka 2011, tayari Watanzania 21 wameuawa kwa kupigwa risasi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na wengine wengi kuumizwa. Kati ya hao, watu 9 wameripotiwa kuuawa na Jeshi la Polisi katika maeneo yanayozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara peke yake. Vile vile, watu watatu waliuawa katika Jiji la Arusha wakati polisi walipovamia maandamano ya amani kupinga uchaguzi batili wa meya wa Jiji hilo.

Mheshimiwa Spika, cha kusikitisha zaidi, wilayani Tarime Watanzania walishuhudia Jeshi la Polisi likitumia giza la usiku kuiba maiti za marehemu lililowaua na baadae kuwatelekeza barabarani na kukimbia. Sasa tunadhihakiwa na watu wengine duniani kwa kuwa na Jeshi la Polisi linaloiba maiti badala ya kulinda uhai wa raia na mali zao!

Mheshimiwa Spika, mbali na ripoti kuhusu ukiukwaji mkubwa Haki za Binadamu, zilizotolewa na taasisi zisizo za kiserikali, taasisi za kiserikali kama vile Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya Tanzania (CHRAGG) pia zimethibitisha jinsi vyombo vya dola vya nchi hii vilivyo katili. Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya mwaka 2002/03 iliyochapishwa mwezi Mei 2005, ilisema kwamba malalamiko mengi iliyoyapokea yalihusu polisi kubambikizia raia kesi, mahabusu kutopelekwa mahakamani kama taratibu zinavyotaka, watuhumiwa kupigwa na kuteswa wakati wa kuhojiwa na upelelezi hasa wa kesi za mauaji kuchukua muda mrefu

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inatoa haki ya kuishi kwa kila mtu na inaitaka Serikali kumpatia kila mtu hifadhi ya maisha yake. Vile vile, vifungu vya 195 na 196 vya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania vinakataza vitendo vya mauaji vilivyo kinyume na sheria. Kwa mujibu wa ibara ya 30(2)(c) ya Katiba, mauaji yanaweza kuwa halali endapo yamefanywa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa kwa ajili ya “... kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la ... jinai.”

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, mauaji yanayofanyika ili kutekeleza adhabu ya kifo inayokuwa imetolewa na mahakama kwa kosa la mauaji chini ya kifungu cha 197 cha Kanuni ya Adhabu ni mauaji halali kwa mujibu wa sheria zetu. Kinyume kabisa cha sheria hiyo, mauaji yote ambayo yamekuwa yakifanywa na Jeshi la Polisi hayajawahi kutokana na adhabu yoyote ya kifo iliyotolewa na mahakama za Tanzania na kwa hiyo ni mauaji haramu.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo, Sura ya 24 ya Sheria za Tanzania, kifo chochote ambacho kimetokea katika mazingira ya mashaka kinatakiwa kuchunguzwa kwa mujibu wa sheria hiyo. Hatua ya kwanza ya uchunguzi wa kifo cha aina hiyo, kwa mujibu wa sheria hiyo, ni uchunguzi wa kidaktari (autopsy) ili kubainisha sababu halisi ya kifo hicho. Aidha, hatua ya pili ni uchunguzi wa kimahakama – kwa kutumia mahakama ya korona – ili kujiridhisha kwamba kifo hicho hakijatokana na matendo au sababu za kijinai.

Mheshimiwa Spika, katika matukio yote ya mauaji yanayolihusisha Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama vya Tanzania, utaratibu huu wa kisheria haujawahi kufuatwa. Aidha, ukiachia matukio ya mauaji yaliyomhusisha aliyekuwa Afisa Upelelezi wa Jinai wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake ambao hata hivyo waliachiwa huru, matukio mengine yote ya mauaji hayajawahi kuchunguzwa na wahusika kufikishwa mahakamani. Huu ni ushahidi tosha kuwa serikali yetu kupitia Jeshi la Polisi na vyombo vyake vingine vya usalama imekuwa ikiua wananchi wasio na hatia.
 
Zombe saa yako inasoma saa ngap?soma alama za nyakat ndg yng.watanzania wamekuchoka.kama si serekal ya magamba kukulinda nadhani ungekua upo akhera mjini.funga domo lako.
 
Zombe anajua fika kabisa yale aliyoyafanya akiwa polisi na msaada aliopewa na mzee kawawa ilikushinda hiyo kesi...angekuwa na mtu wa bila connection basi angehukumiwa kifungo.....mahakama kila siku zinalalamikiwa kwa rushwa leo anataka tusihoji!!!!! kesi ngapi zimeamuliwa kwa maslahi ya ccm ..kesi ya mgombea binafsi ni ushahidi tosha kwani kamati kuu ya ccm ilisema Tanzania haija komaa kuwa na wagombea binafsi na mahakama ya rufaa ikaidhinisha maamuzi hayo....watu kuchomwa moto, nakupigwa "mob justice" ni dalili tosha kuwa mahakama haziaminiki...mahakama ya rufaa ilikuwa ya akina jaji Lugakingira na Mwalusanya sio hawa wa voda fast bwana....
 
Zombe anapata wapi courage ya kumkosoa Mh Lema? Bunge linatunga sheria, Mahakama inatafsiri na ku-apply sheria, hivyo kwa Mbunge yoyote kuhoji kesi ya Zombe au nyingine inayofanana nayo ni haki maana bunge lina mamlaka ya kuuliza ili kujua mapungufu yako wapi mpaka mtu kama Zombe anaachiwa huru?

Na kama yapo basi sheria inatungwa ili kudhibiti hilo. Pengine Zombe ana hofu kuwa Mh Lema anaelekea kuanika usanii uliofanyika mpaka kuwaacha wauaji wakitembea huru uraini?
 
Mheshimiwa Spika, katika matukio yote ya mauaji yanayolihusisha Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama vya Tanzania, utaratibu huu wa kisheria haujawahi kufuatwa. Aidha, ukiachia matukio ya mauaji yaliyomhusisha aliyekuwa Afisa Upelelezi wa Jinai wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake ambao hata hivyo waliachiwa huru, matukio mengine yote ya mauaji hayajawahi kuchunguzwa na wahusika kufikishwa mahakamani. Huu ni ushahidi tosha kuwa serikali yetu kupitia Jeshi la Polisi na vyombo vyake vingine vya usalama imekuwa ikiua wananchi wasio na hatia.



kama kuna mtu anajua zombe alipo ampelekee hiki kipande kisha haojiwe tena na wana habari
watu wasijekuwa wamemlisha matango pori au kuna ukweli una mpanikisha kila hii kesi inapotajwa na yeye anaona amesha save
 
Naona TBC wataiweka kama leading story na magazeti ya uhuru,jambo leo nk....wanapenda stori za kinafiki kama hizi

wakifanya hivyo waweke na hii
Mheshimiwa Spika, katika matukio yote ya mauaji yanayolihusisha Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama vya Tanzania, utaratibu huu wa kisheria haujawahi kufuatwa. Aidha, ukiachia matukio ya mauaji yaliyomhusisha aliyekuwa Afisa Upelelezi wa Jinai wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake ambao hata hivyo waliachiwa huru, matukio mengine yote ya mauaji hayajawahi kuchunguzwa na wahusika kufikishwa mahakamani. Huu ni ushahidi tosha kuwa serikali yetu kupitia Jeshi la Polisi na vyombo vyake vingine vya usalama imekuwa ikiua wananchi wasio na hatia
.


hapo watakuwa wamekidhi sheria ya habari na kuelimisha umma vinginevyo CHADEMA wana haki ya kuwashitaki au kuomba watoe na habari ya upande wa wa pili ilikuwa je
 
Amesema hivo ili pindi CDM ikiongoza nchi anajua ndo mwanzo wa kifungo kwake kwahiyo atajinyonga ili aukwepe mkono wa sheria
 
kichaa sio lazima aokote makopo.. Kwa maneno hayo tayari ameshagundulika nae kichaa pia, na akijinyonga tutashukuru sababu atakua ametupunguzia kazi ya kuwapoteza watu wachafu km yeye.
 
Huyo anamaanisha CHADEMA hawatawali ng'oo.
Hata Karume aliwahi kusema hakutakuwepo uchaguzi huru Zanzibar kwa miaka hamsini.Guess what happened. So be careful what you wish ( do not wish) for
 
Serikali ya CHAMA cha Mapinduzi ni vyema ikawadhibiti watu wa aina ya Zombe kuvisogelea vyombo vya habari kwa kuwa ndio chanzo cha kuwa kiberiti cha mlipuko wa vuluga za umma.

Kutomdhibiti jamaa huyu kilio kitafuata Serikali ya CCM.

Wamemlea kwa sababu ya collective Responsibility lakini jamaa huyu atawacost kama hawata kuwa na break dhidi yaka manake busara na maono ni hasi hivyo lolote laweza tokea tokana na kauri zake zisizo na brake hata kidogo na zisizo pima madhara ya kauri zake na kuendelea kuamini bado analindwa na mfumo.
 
wakuu nimeshtuka sana kuona yule jamaa zombe anamshutumu mbunge wa arusha alikuwa mwizi wa magari
nimeshtuka sana kwa hilo,je atapona?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom