Lijuakali aagiza polisi wamkamate Godbless Lema kwa uchochezi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1699371136839.png
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ameagiza Jeshi la Polisi kumsaka popote alipo na kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema ili ahojiwe kwa kauli za uchochezi alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 24,2023.

Kwenye Mkutano huo ambao ulifanyika katika kata ya Korongwe jimbo la Nkasi Kaskazini ambako anaelezwa kuwa alitamka kuwa wanaume wa Kijiji Korongwe asilia wamuue Mtendaji wa Kijiji hicho Daud Ismail.

Hata hivyo Lema amekanusha madai ya uchochezi huo akisema alitamka kuwa wanaume ‘wamuoe’ mtendaji huyo akidai ni lugha za kisiasa na wala hakuna madhara yoyote kuhusiana na utendaji wake.

Imedaiwa Lema akiwa na baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema kwenye mkutano huo katika Vitongoji vya Forodhani na Fipa, Kata ya Korongwe, kwa makusudi alitoa kauli ya vitisho kwa mtumishi huo baada ya wananchi kulalamika kwenye mkutano huo kuwa wanasumbuliwa na Mtendaji huyo.

DC Lijualikali alisema haiwezekani kiongozi mwenye ushawishi kuachiwa atambe kwenye kauli hiyo ambayo imepeleka taharuki kubwa kwa wananchi na Mtendaji huo ambaye kwa sasa maisha yake yako hatarini.
 
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ameagiza Jeshi la Polisi kumsaka popote alipo na kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, ili ahojiwe kwa alichoeleza "kutoa kauli za uchochezi" kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 24, 2023.

Katika video ambayo inasambaa kwenye mitandao ya kijamii, Lema anahamasisha wanaume wa Kijiji cha Korongwe Asilia, wamuue Mtendaji wa kijiji chao kwa madai ya kuwasumbua wananchi.

Hata hivyo Lema amezungumzia video hiyo kuwa, hakuhamasisha kitu kama hicho na asingeweza kutoa kauli kama hiyo badala yale aliwaambia wanaume wamuoe mtendaji huyo ili asiwasumbue jambo ambalo amejitetea kwa kusema "lugha za kisiasa."

Kwenye video hiyo, Lema akiwa na baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema katika Vitongoji vya Forodhani na Fipa, Kata ya Korongwe, anaonekana kutamka neno

ambalo limetafsiriwa na Mkuu wa

Wilaya kuwa ni kutaka wanaume wamuue mtendaji anayewasumbua.

Lijualikali amesema haiwezekani kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa watu aachiewe kutamba kwa kauli hiyo ambayo imesababisha taharuki kwa wananchi na Mtendaji huo ambaye kwa sasa maisha yake yako shakani, huku kiwango cha utendaji kikishuka.

"Namuagiza OCD wa Nkasi, kuchukua hatua za kisheria mara moja kumuita kokote aliko Godbles Lema ili afike Nkasi akafanyiwe mahojiano kuhusu kauli yake ya kichochezi ya kuhatarisha hali ya usalama wa mtendaji huyo katika eneo letu na kukwaza juhudi za wananchi kufanya shughuli za maendeleo," amesema Lijualikali.

Akijibu swali ni kwa nini jambo hilo lilitokea muda mrefu lakini wamechelewa kutoa taarifa, Mkuu wa Wilaya amesema walianza kwa uchunguzi kuhusu kauli hiyo ilikuwa na maana gani na ililenga nini kitokee na kwamba wamejiridhisha haikuwa kauli nzuri.
 
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ameagiza Jeshi la Polisi kumsaka popote alipo na kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema ili ahojiwe kwa kauli za uchochezi alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 24,2023...
Na ashughulikiwe barabara akitibitika na uovu huo....
 
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ameagiza Jeshi la Polisi kumsaka popote alipo na kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema ili ahojiwe kwa kauli za uchochezi alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 24,2023.

Kwenye Mkutano huo ambao ulifanyika katika kata ya Korongwe jimbo la Nkasi Kaskazini ambako anaelezwa kuwa alitamka kuwa wanaume wa Kijiji Korongwe asilia wamuue Mtendaji wa Kijiji hicho Daud Ismail.

Hata hivyo Lema amekanusha madai ya uchochezi huo akisema alitamka kuwa wanaume ‘wamuoe’ mtendaji huyo akidai ni lugha za kisiasa na wala hakuna madhara yoyote kuhusiana na utendaji wake.

Imedaiwa Lema akiwa na baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema kwenye mkutano huo katika Vitongoji vya Forodhani na Fipa, Kata ya Korongwe, kwa makusudi alitoa kauli ya vitisho kwa mtumishi huo baada ya wananchi kulalamika kwenye mkutano huo kuwa wanasumbuliwa na Mtendaji huyo.

DC Lijualikali alisema haiwezekani kiongozi mwenye ushawishi kuachiwa atambe kwenye kauli hiyo ambayo imepeleka taharuki kubwa kwa wananchi na Mtendaji huo ambaye kwa sasa maisha yake yako hatarini.

Siku hizi ameacha kulia? DC wa hovyo, hajui mamlaka yake yanaishia humo Nkasi?
 
View: https://youtu.be/p8TMM3xlu6A?si=pkGtZwOsjh3yZ_G1

Kheri James aliposema atamuua Tundu Lissu kwa kumchoma Sindano za Sumu ni Mkuu gani wa Wilaya au Mkoa au OCD au RPC aliyebwabwaja?

Au Tanzania sasa ina Sheria za aina mbili moja kwa CCM na nyingine kwa Wapinzani WAZALENDO?

Nabii Lema huyo hakuwezi.

Sheria za nchi hii hazieleweki kabisa! Huko Iringa mama aliyekutwa na vipande 12 vya nyama ya swala amehukumiwa kwenda jela miaka 22 na faini ya shilingi laki 9 wakati mchina aliyekutwa na meno ya tembo zaidi ya 500 alihukumiwa kulipa shs. Laki 3 na kifungo kisichozidi mwaka mmoja!
 
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ameagiza Jeshi la Polisi kumsaka popote alipo na kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema ili ahojiwe kwa kauli za uchochezi alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 24,2023.

Kwenye Mkutano huo ambao ulifanyika katika kata ya Korongwe jimbo la Nkasi Kaskazini ambako anaelezwa kuwa alitamka kuwa wanaume wa Kijiji Korongwe asilia wamuue Mtendaji wa Kijiji hicho Daud Ismail.

Hata hivyo Lema amekanusha madai ya uchochezi huo akisema alitamka kuwa wanaume ‘wamuoe’ mtendaji huyo akidai ni lugha za kisiasa na wala hakuna madhara yoyote kuhusiana na utendaji wake.

Imedaiwa Lema akiwa na baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema kwenye mkutano huo katika Vitongoji vya Forodhani na Fipa, Kata ya Korongwe, kwa makusudi alitoa kauli ya vitisho kwa mtumishi huo baada ya wananchi kulalamika kwenye mkutano huo kuwa wanasumbuliwa na Mtendaji huyo.

DC Lijualikali alisema haiwezekani kiongozi mwenye ushawishi kuachiwa atambe kwenye kauli hiyo ambayo imepeleka taharuki kubwa kwa wananchi na Mtendaji huo ambaye kwa sasa maisha yake yako hatarini.
Anatafuta Kiki
 
View: https://youtu.be/p8TMM3xlu6A?si=pkGtZwOsjh3yZ_G1

Kheri James aliposema atamuua Tundu Lissu kwa kumchoma Sindano za Sumu ni Mkuu gani wa Wilaya au Mkoa au OCD au RPC aliyebwabwaja?

Au Tanzania sasa ina Sheria za aina mbili moja kwa CCM na nyingine kwa Wapinzani WAZALENDO?

Nabii Lema huyo hakuwezi.

Hatimay Mwenyezi Mungu akamwondoa aliyewapa hii Kiburi mpaka leo wamepoteana.

Nilijuwa wana ubavu huo kumbe walikuwa wanategemea Mwanadamu
 
Back
Top Bottom