Abdalah Zombe: CHADEMA wakiongoza nchi nitajinyonga, adai Lema alikuwa mwizi wa magari!

Naona TBC wataiweka kama leading story na magazeti ya uhuru,jambo leo nk....wanapenda stori za kinafiki kama hizi
Mkuu, habari ya ZOMBE ktk TBC1 ni ya pili ktk dondoo za habari,tena inasema tuhuma nzito kuwa LEMA,mbunge wa Arusha, anashiriki ktk wizi wa magari.
 
acheni hizo bwana, wanaojinyonga hawatangazi, hivi huyu jamaa anatokea wapi? Iringa au?
 
Ina maana m2 mzima kama yule anazungumza ki2 cha namna hii halafu mpk sasa hajatiwa hatiani? Hv hakuna kipengele chochote kinachowalinda watu watoa kauli kama ya huyu MWEHU? Ama anasubiriwa aje ajinyonge ndiyo akamatwe?
 
Abdalla Zombe kasema mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema alikuwa na mtandao wake wa wizi wa magari ambao ulijumuisha wakenya.

Hatua hiyo imekuja baada ya Godbless lema kuhiji kuachiwa kwa Zombe na mahakama kupitia hotuba ya waziri kivuli ya wizara ya mambo ya ndani. Lema amekanusha tuhuma hizo na amedai hajawahi kutuhumiwa wizi tangu alipozaliwa.

Makao makuu ya polisi nayo yamehoji iweje Zombe atoe shutuma hizo sasa na asizitoe wakati akiwa katika jeshi la polisi? Hata hivyo polisi wamesema wataliangalia suala hilo.

source: TBC news
 
Kutokana na hoja ilioletwa bungeni na mmbunge wa arusha mjini godbles lema aliehoji bungeni juu ya swala la kuachiwa kwa aliekua mkuu wa polisi wa mkoa wa dar es salaam bwana abdalah Zombe ...leo hii zombe ameitisha kikao cha waandishi wa habari na kumtuhumu Lema kuwa yeye na wenzake anamtandao wa wizi wa magari kutoka nchin kenya...

My take...hizi ni tuhuma tu za kisiasa zenye lengo la kuchafuliana majina....
 
... There some spell in Zombes statements which tells me that ...Mr Zombie if not very careful will be totaly consumed by his own statements !!
 
Jamaa, kauwasha uliokuwa unaelekea kuzimika. Mpaka anabwabwaja na media tayari kaisha tenda kosa kutokana na hizo maneno yake mbofu mbofu. Pili ajiandae kuisaidia polisi tena kutokana na maelezo aliyoropoka. Mpaka Afande Chagonja kashikwa kigugumizi cha muda. Kazi ipo mpaka ifike 2015 mtanena yote.
 
Nimempenda mh mmoja wa polisi ameulizwa je kwa nini aseme leo hii alikuwa wapi
na pamoja na hayo kama anajua kwa nini akumkamata ..akawaambia waandishi hata mimi nimesshtuka mtu mwenye
cheo kikubwa kama hiki kuongea mambo ya wizi baada ya kukamatwa nimeshindwa kumuelewa alisema bw mmoja aitwa mgonja
kwa nini asiseme wakati akiwa ndan anasema kwa sababu mh amemtaja kwenye bunge aliuliza mh huyo wa polisi
 
huyu Zombwe ni mpungufu wa akili acha aendelee kuwatumikia magamba.
 
Pombe za asubuhi mbaya sana.zombe pombe haziwezi.Huyu jamaa anaumwa!nashangaa cjui alipataje nafasi hiyo ya juu ktk uongozi wa jeshi la polisi.inavyoonekana amehakikishiwa kupewa nafasi katika chama cha magamba.
 
Baada ya mbunge wa Arusha mjini,mheshimiwa Godbless Lema kuhoji kuhusu maendeleo ya kesi ya zombe,zombe naye amejibu mapigo.Zombe amedai kwamba bunge na mahakama ni mihimili tofauti na haitakiwi kuingiliana kwa hiyo mahakama pekee ndiyo inayohusika na hatma ya kesi yake.Kama haitoshi,bwana Zombe aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa DSM amedai kwamba,kabla ya kuwa mbunge,mheshimiwa Lema alikuwa kiongozi wa mtandao uliokuwa unahusika na wizi wa magari kutoka nchini kenya.Lema amekana kuwahi kuhusika na ujambazi na akasisitiza zombe ndiyo jambazi kwani kuna ushahidi tosha wa yeye kuhusika na mauaji ya raia wasio na hatia.(TBC 1)
 
Sorry kwa usumbufu,nime-post thread ambayo mwenzangu kesha-post!
 
Huyu bwana tulikua tumemsahau! Kwa mtazamo wangu nahisi katumwa lakini katika kutumwa kwake ameshindwa kujieleza mbele ya waandishi wa habari na pia mbele wa watanzania woote wakiwepo wale wafiwa wa marehemu wa Mahenge! Abdalla Zombe umezidhihirishia familia zile za Mahenge kua kwa namna moja au nyingine hukumu ya kifo inakusubiri! Watanzania hatutakubali ujinyonge mwenyewe kama tulivyokunukuu bali kwa mujibu wa sheria utahukumiwa kunyongwa kwa mujibu wa sheria! Ulichokiongea leo mbele ya watanzania hakika damu za wale marehemu zinakusumbua! Uliidanganya mahakama sasa unawadanganya hata watanzania???..! Tumekunukuu ukisema kua muheshimiwa Lema alikua ni mshiriki wa uwizi wa magari, je ulikua wapi katika cheo chako wakati ule?????....! Na hata wenzako walioko kazini wameuliza kua wewe ulikua wapi katika njama hizo za muhesimiwa huyu Lema???....! Umeuanza mfungo vibaya!!!!
 
bangi + kuua binadamu wasio na hatia = akili kuruka na kuongea hovyo. Zombe aende akatubu dhambi ya kuua wasio na hatia. Aache kuongea ka mwehu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom