Abdalah Zombe: CHADEMA wakiongoza nchi nitajinyonga, adai Lema alikuwa mwizi wa magari!

Ni Zombe huyu huyu aliyetokeza mbele ya vyombo vya habari na kudai wale wandugu wa Morogoro walikuwa majambazi. Tena akatoa na vielelezo. Lakini ukweli wake umejulikana. Sasa leo anajitokeza tena na kudai Lema ni mwizi wa magari. Lema aliiba lini magari? Kwa nini hakukamatwa? Na kama Lema hakusema chochote kuhusu kuachiwa Zombe angesema haya aliyosema kuhusu Lema? Ina maana Zombe anajuwa wahalifu lakini anakaa kimya unless waanike madhambi yake?
 
Anajua kuwa Chadema ikiwa madarakani haitakuwa na ufisadi wala rushwa kwa hiyo itamshughulikia ipasavyo, itambidi awalipe kwanza ndugu wa marehemu fidia, kisha kifungo cha maisha segerea. So, kuepuka fedhea hiyo ameona ni bora ajinyonge kabisaaa Chadema ikiwa madarakani.
 
Chonde chonde CCM huyu Zombe atawatia kitanzi CCM cha Moto kujitoa itakuwa shida,naona anaendelea na vimbwanga vyake,kwa kuwa sio anahisaida CCM bali anachangia kuivua nguo Serikali ya CCM.
 
Huyu Zombe sii ndiyo yule muuaji wa wafanya biashara? Watanzania hatuna nafasi ya kumsikiliza muuaji.
Damu za marehemu zinamuwewesesha.
KAMANDA LEMA YABANE HAYO MAGAMBA BARAABARA. YATATIA AKILI!!
.
 
jaman kuua watu wasio na hatia sio mchezo ati, yan lazima akili ifyatuke kama ilivyofyatuka ya huyu mbabu!. Huyu inabidi ashtakiwe kwa mara ingine!
 
Lazima ajinyonge kabla ya hukumu ya haki kutolewa kesi ya mauaji huwa haifutwi inaweza fufuliwa wakati wowote.
 
Huyu kweli ni Vampire Zombie,kafunguka na kimeta wa Merelani ''Lema'' kuwa ni wavuna magari akishirikiana na wakenya.Aliyemtizama Zombie na jinsi alivyokuwa akimwaga pembeni ya mti wa mahakama anaweza dhani ni chizi ama kala ''msuba'' maake kwa kujiamini na issue anzo rusha hewani.Hata hivyo hizi za Zombe sio za kupuuza kwa kigezo eti alikuwa wapi mpaka leo?.Kauli ya Chagonja ni danganya toto na hapa ni sungura na sizitaki ''mbivu hizi''.Ukweli ni kuwa hii ni deal kwa polisi sasa kudeal na Lema,kwani kauli ya Chagonja imejicontradict kwa kusema kuwa Zombe by that time RCO alikuwa na mafaili mengi mezani hivyo inawezekana anaijua vizuri issue hii.

Hapa Chagonja anatuaminisha kuwa issue ya Lema kama alivyodai Zombie ni bora uchunguzi ufanyike kujiridhisha kuwa tuhuma hizo ni kweli ama uongo.Humu janvini nimewahi kusikia tetesi juu ya uharifu wa Lema hasa katika mijadala motomoto,pengine kufunguka kwa Zombie (Zombe) ni mwanzo wa kuzua mengi.

Wengi humu tunamuona ''mwehu'' ama mpiga ''pafu'' lakini pia si wakupuuza kwani by that time alikuwa ''king maker'' wa waharifu hivyo sioni ajabu yeye kuwataja wenzie aliokuwa akila nao deal kwani Zombe kwa utata wake anawajua majizi wenzie.Lema anadai Zombe akiwa RCO Dar aliwezaje kujua ya Arusha?.Lema atambue kuwa Zombe alikuwa mpiga deal na uwepo wake Bongo kama ''axes of evil city'' ni dhahili alikuwa na connection kubwa katika nchi hasa Arusha ambapo mzigo ukipigwa na haraka yeye ndiye mpokeaji Bongo na kuweka mazingira ya ''sintofahamu''.

Chagonja tafadharini kamata Zombe atawasaidieni kwani kunafaili nyingi za waarifu wenzie kama hakutia moto basi atakuwa kazibana maara na kuzifujisha pindi anapohisi mtu anaingilia maslahi yake hasa baada ya kuponyoka kitanzi.Nimeipenda hii ya Vampire Zombie,inawezekana akawa raia mwema kama ameanza kutaja dhami zake.
 
Is Zombi alive? Ajinyamazie tu cuz he is gud as dead! Na ni chombo gani cha habari kimedhubutu kwenda kumsikiliza muuaji yule? Maskini...he is so cold and now he want to be hot on Press through Lema bt plz msimpe nafasi hyo, LABDA CKU ATAKAYOAMUA KUCONFESS MAUAJI YA KULE PANDE!
 
Yaani alivyokuwa anaongea hadi nimemwonea huruma/ kama mwehu nadhani damu ya wasokuwa na hatia alowaua bado inamuuma. Kimsingi lazima ajinyonge cdm wakichukua nchi kwakuwa anaelewa kuwa hawawezi kuvumilia mediocrity!
 
Damu za marehemu aliowapiga risasi zinamlilia tayari keshaanza kuwa chizi mda c mda ataanza kuokota makopo
 
sasa nadhani Zombe mwisho wake umefika, off all the people kamchokoza LEMA duh sasa utamu waja!!!!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Lazima ajinyonge kwa sababu anajua kwa mauaji aliyoyafanya chadema hawata mwacha, watamnyonga tu kwa kosa la mauaju hata kama Chama Cha Magamba kimejitahidi kumfunika.
 
Kwahyo alikuwa anajua mh lema ni mwizi akanyamaza? Huo ni aidha uongo 100% au yeye zombe alikuwa mwizi pia.lol.huyo jamaa ni hatari kwa usalama wa ccm,anaweza kutoka na kauli tata sana ikaiangusha sirikali ya JK
 
Jamani tusimlaumu sana Zombe..kwa experience ya kule magereza, inawezekana kabisa jamaa wa mle ndani wameshaharibu sana mifumo yake mikuu ya ufahamu,uelewa,
na kumbukumbu hiyo inatakiwa huyu jamaa apelekwe mirembe..
 
Jamani yaani mnapoteza muda wenu ku-brainstorm mambo ya Zombe!!

The guy is psyco case!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom