A Program Note: Tutaweka Hoja Zetu Wazi

A Program Note: Tutaweka Hoja Zetu Wazi

MM
Ni vizuri kutoa ya moyoni. Ukimya wa Dr haulipi. Wengi tunasononeka.

Ombi langu kwako: Kwa namna yoyote mtakavyotoka, ni vema mlenge kuimarisha umoja ndani ya CDM na UKAWA kwa ujumla. Kinyume na hapo mtakuwa mmeipa kick ya uhakika CCM.

Nasubiri hoja zako.

Mkuu najua unahofu zaidi na chama kuliko taifa, sisi tumeshachora mstari ya kwamba uzalendo wetu katika chama hauwezi kuzidi hata nchi moja zaidi ya ule wa taifa na hususani kipindi ambacho maslahi ya vitu hivi viwili vinapogongana kama wakati huu wa sasa.

vyama vinaweza kufa na tukaanzisha vyama vingine kama nchi itabaki salama,ila ni upumbavu uliopitiliza kufikili kiyume chake.

daima tutasimama na kusimamia haya na hilo ndio agano letu kwa taifa

nukukumbushe tu ya kwamba

"Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho"
Mzee Mwanakijiji
 
Imebaki kona moja tufike.. Msishuke kwenye bus tafadhali..!!!
 
Kwa mara ya kwanza ni mwanaChadema ntakayempigia kura Magufuli wa CCM. Kisa? Ni huku kutokujali kulikopitiliza kwa akina Mbowe na Lowassa wake.

Nilimsikia Tundu Lissu anajitetea eti ni uwendawazimu kumpuuza Lowassa huku akiwa na watu wengi hivi na nguvu kubwa vile. Kwangu mimi hii naita worshipping of persons.Chadema haijawa hivi kwa sababu ya nguvu ya mtu mmoja, na kumkaribisha mtu hadi chumba chako cha ndani kisa ana hela na nguvu mtatushawishije kwamba hamtaiuza nchi kwa wenye hela na nguvu zaidi?
 
Namuelewa Dr. Slaa; namuelewa Mbowe pia. Mbowe kadharau madhara ya uamuzi wake kama mwenyekiti kumualika mtu ambaye alikuwa na sifa inayopingana na "brand"/jina la chama pasipo kutoa majibu yenye mantiki na mashiko kwa wanachama na wananchi wasioelewa "move" yake na waliohatarisha uhai wao kutetea "brand" ya chama. Ikumbukwe kwamba "brand" ya Chadema ilikuwa ni chuki na vita dhidi ya ufisadi. Na hii "brand" ilijengwa kwa wanachama wa Chadema kama Josephine Mshumbusi kupigwa na serikali ya CCM mpaka kuvuja damu huku akiwa mjamzito.

Kwa upande wa Slaa, ameshikilia msimamo mkali bila kujua kwamba lengo kuu la chama chochote cha siasa na ambalo ni la muhimu zaidi ni kushika dola. Wazo la muhimu katika kushika dola ni kwamba ukishika dola una nafasi kubwa ya kueneza itikadi na sera zako kwenye maisha ya kilasiku ya wale unaowaongoza. Mbowe anaonekana kujali Chadema kushika dola zaidi, kuliko mchakato wake.

Wote, Mbowe na Slaa wapo sahihi. Anachosimamia Mbowe kina umuhimu sawa na kile anachosimamia Slaa, kwani huwezi kuwa na lengo bila kuwa na njia madhubuti ya kufikia hilo lengo. Katika huu mtafaruku, unaweza kusema kwamba Slaa ni njia, na Mbowe ni lengo la kufikia hiyo njia. Kinachotakiwa ni kwamba mawazo ya hawa watu wawili yaheshimiwe kwa uwiano sawa. Chukulia mfano wa uwanja wa mpira wa miguu; hapa kila mmoja atoke kwenye goli lake wakutane katikati ya uwanja, kimawazo. Wasipoweza kufanya hivyo chadema imekufa - haijalishi kwamba itashinda urais au haitashinda.
 
Nafikiri unamaanisha ya Zitto kufukuzwa
mimi sikulitaja hilo
mimi nalitaja la Zitto kuzuiwa kugombea uenyekiti
msingi wa demokraia ilikuwa wamshinde kwa hoja na kushawishi wanachama wasimchague
lakini sio kumzuia hata kugombea tu,wakati chama ni cha kidemokrasia

Huo ni mmoja wa mifano ambapo chama kiliuka misingi yake yenyewe tu inayojitangaza kuisimamia
na suala la Kafulila pia....tena Slaa huyu huyu ndo alikuwa jeuri kwa Kafulila...

Mkikiuka misingi kwa kuwatazama watu na kusema huyu ni sisimizi aende zake
na watu kama Mwanakijiji wakiona ni sawa...leo misingi hiyo hiyo inakiukwa tena
na sasa hivi ndio watu wanaamka kupinga...laiti mtu kama Mbowe angezoea kupingwa
toka mwanzo akileta kitu hakiko sawa..asingeleta haya ya sasa[/QUOTEl]

Umesema vizuri sana mkuu,issue ya zitto kukatazwa kumchallenge mbowe Mara mbili,issue ya kafulila kuitwa sisimizi na issue ya rasta chacha wangwe kuzuiwa milele kumchallenge mbowwe kwenye kugombea uenyekiti ndivyo vilivyompa kiburi mbowe kujiona yeye ndio yeye chadema ni Mali yake na mke wake kupitia Mzee mtei,slaa nae analo la kujibu kwa kushirikishwa na mbowe kuwadhuru chacha,zitto,kafulila,habibu mchange,Juliana,kitilla na wengine kwa kujua ama kutojua,ifike mahali wanasiasa waache kuunga mkono kila analosema na kulifikiria mwenyekiti,nayasema haya nikikumbuka pia mchango Wa kina zitto,kafulila,mnyika,slaa na halima mdee katika kumsaidia mbowe kumshughulikia marehemu chacha wangwe alipoanzisha vuguvugu la kumkataza na kumkemea mboweasifike huku alikofika sasa.
 
Namuelewa Dr. Slaa; namuelewa Mbowe pia. Mbowe kadharau madhara ya uamuzi wake kama mwenyekiti kumualika mtu ambaye alikuwa na sifa inayopingana na "brand"/jina la chama pasipo kutoa majibu yenye mantiki na mashiko kwa wanachama na wananchi wasioelewa "move" yake na waliohatarisha uhai wao kutetea "brand" ya chama. Ikumbukwe kwamba "brand" ya Chadema ilikuwa ni chuki na vita dhidi ya ufisadi. Na hii "brand" ilijengwa kwa wanachama wa Chadema kama Josephine Mshumbusi kupigwa na serikali ya CCM mpaka kuvuja damu huku akiwa mjamzito.

Kwa upande wa Slaa, ameshikilia msimamo mkali bila kujua kwamba lengo kuu la chama chochote cha siasa na ambalo ni la muhimu zaidi ni kushika dola. Wazo la muhimu katika kushika dola ni kwamba ukishika dola una nafasi kubwa ya kueneza itikadi na sera zako kwenye maisha ya kilasiku ya wale unaowaongoza. Mbowe anaonekana kujali Chadema kushika dola zaidi, kuliko mchakato wake.

Wote, Mbowe na Slaa wapo sahihi. Anachosimamia Mbowe kina umuhimu sawa na kile anachosimamia Slaa, kwani huwezi kuwa na lengo bila kuwa na njia madhubuti ya kufikia hilo lengo. Katika huu mtafaruku, unaweza kusema kwamba Slaa ni njia, na Mbowe ni lengo la kufikia hiyo njia. Kinachotakiwa ni kwamba mawazo ya hawa watu wawili yaheshimiwe kwa uwiano sawa. Chukulia mfano wa uwanja wa mpira wa miguu; hapa kila mmoja atoke kwenye goli lake wakutane katikati ya uwanja, kimawazo. Wasipoweza kufanya hivyo chadema imekufa - haijalishi kwamba itashinda urais au haitashinda.

Umeandika vizuri sana mkuu!
Cc: Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
Mkuu najua unahofu zaidi na chama kuliko taifa, sisi tumeshachora mstari ya kwamba uzalendo wetu katika chama hauwezi kuzidi hata nchi moja zaidi ya ule wa taifa na hususani kipindi ambacho maslahi ya vitu hivi viwili vinapogongana kama wakati huu wa sasa.

vyama vinaweza kufa na tukaanzisha vyama vingine kama nchi itabaki salama,ila ni upumbavu uliopitiliza kufikili kiyume chake.

daima tutasimama na kusimamia haya na hilo ndio agano letu kwa taifa

nukukumbushe tu ya kwamba

"Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho"
Mzee Mwanakijiji
Hakuna tatizo kwa manufaa ya nchi lazima tufike mahali tuseme CCM basi inatosha kwa kuunganisha nguvu mahali pengi pamefanyika hakuna shida endeleeni kusema wote tutasema lakini tutafika CCM must go by all means
 
MM....kwavile Mungu kanipa akili....nitaitumia vyema.....haiwezekani tumpuuze Dr Slaa dakika hii.....wengine tunajua mapito yake....nitasimama nae......

Mkuu kwenye siasa mtu ukiwa DOGMA utakumbwa na matatizo. Dr Slaa hawezi kupuuzwa na hatujui ni kwanini yanayotokea yanatokea.

Nadhani viongozi wa CDM wamesema vizuri, kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu au audi wa kudumu. Tukianza na Slaa mwenyewe yeye alikuwa mwana CCM na sasa ni mwana CDM. Na kama mtakumbuka kabla ya kwenda CDM alikuwa na kashfa ya maana tu ya dawa za kulevya, gari yake ilitajwa kukutwa na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya. Sidhani kama ingekuwa biasara CDM kumkana, au kina Mbowe kumkana kwa sababu hiyo.

Lowassa is a controversial politician, lakini is he a plus or a negative on CDM? Is Dr Slaa going personal or there is a hidden agenda?
Au tuanze kujiuliza CDM is built on policies or personalities, does this party have internal shock absorbing Mechanisms? All in all kazi ya CDM ni kuhakikisha kuwa Dr Slaa yuko ndani na sio nje ya CDM.
 
Mliponyamaza wakati haki za watu wengine zinanyimwa ndani ya CHADEMA na hadi kuunga
mkono 'watu wakiminywa'
kina Kafulila,Zitto na wengi wengineo the list is endless...haya ndo mavuno now
Mkuu
The Boss, asante kwa kulizungumzia hili la double standard ya Chadema na wafuasi-waabudu wao!, na kiukweli siku zote huwa naikubali objectivity yako!.

Mimi nimepigia sana kelele suala la kufuatwa kwa sheria, taratibu na kanuni huku baadhi yetu wanajidai kupigania haki, wakinyamaza kimya wakati Chadema ikifanya madudu ya wazi!, lakini sasa inapotokea payback time ya 'karma', what goes around, comes around, eti ndio watu wanasusa!, na kuja na hoja kibao za kutokubaliana na kilichofanyka!, what a double standards!.

Kuna tatizo kwa baadhi ya wapenzi wa Chadema, kuwaabudia baadhi ya viongozi wao na kuwaona kama ni miungu watu!, sasa hii miungu watu wa Chadema, inapopuuzwa, waabudu wao wanaiona hii kama ni blasphemy!, mungu wao amekashifiwa!.

Kuna wakati shetani huwa una disguise as god!, na kuna wakati hata shetani mwenyewe kabla ya kuwa shetani, alikuwa malaika!, hadithi ya Paulo na Sauli ni funzo tosha kwa ujio wa Lowassa ndani ya Chadema!, kama Mungu ndio alipepanga mpango huu, hawa wote wanaoupinga ni mashetani disguised as malaika!.

Ningekuwa mimi ni sehemu ya Chadema, wote hawa ningefukuzia mbali na sio kubembeleza!. Utafiti umeishafanya kuwa kuna watu asilimia 10%, ndani ya Chadema watapinga ujio wa Lowassa, lakini gaini itakuwa ni asilimia 38%, nashauri timulia mbali hii asilimia 10% the sooner the better, gain the 38% safari ya matumaini iendelee!.

Kikukweli Magufuli ni mzuri kuliko Lowassa, na CCM is still stronger than UKAWA kwa ujumla wake wote, ila ushindi kwa UKAWA kupitia kwa Lowassa lies on the "positive will power" kwa wanaotaka mabadiliko ya kweli, sasa hawa kenge kwenye msafara wa mamba, wanatuwekea kiwingu cha "negative will power" ambayo itapunguza margin ya ushindi kwa sababu hata hao nao hizo negative will zao nazo zina power kama alivyo devil or satan mwenyewe!.

NB, pia inawezekana na mimi ndio nikawa wrong kuwa CCM ndio malaika na ndio mpango wa Mungu CCM iendelee kuitawala Tanzania, halafu Lowassa ndio mpango wa shetani, hivyo sisi wote tunaosupport ujio wa Lawassa ndio tunaomtumikia shetani, na wote wanaopinga ujio wa Lowassa Chadema, ndio wanaofanya kazi ya Mungu!, that being the case, naomba kuwaomba radhi hao niliowaita mashetani!, kumbe mashetani ni sisi!.

Pasco.
 
Mzee Mwanakijiji, hebu turudi nyuma...Flashback 1995, kuna mambo mawili yalitokea;

1. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustino Lyatonga Mrema, baada ya kugundua anayo nafasi finyu ya kuteuliwa kugombea Uraisi kupitia CCM, alihamia NCCR - Mageuzi. Mrema hakuwa ametoa mchango wowote katika harakati za mageuzi na badala yake ndiye kinara aliyeongoza majeshi ya Usalama kupinga mageuzi kwa njia ya virungu, mabomu ya machozi na risasi za moto. Wako waliopigwa na kuteswa, wako waliopata ulemavu wa kudumu, wapo waliopoteza kazi na kufungwa na familia zipo zilizosambaratishwa na kusahaulika. Mwaka 1995 ndio mwaka uadui kati ya vyombo vya usalama na raia ulipozaliwa na ni huyo huyo Mrema ambaye awali aliapa kwamba akihamia upinzani laana imkute. Wakati huo tuko wengi wetu tulipinga sana Mrema kukaribishwa NCCR - Mageuzi lakini hatukusikilizwa hadi wengine tukakata tamaa kabisa na kuachana na siasa.

2. Dr. Wilboard P. Slaa aliwekewa mizengwe baada ya kushinda katika kura ya maoni kwa asilimia kubwa tu akiwa CCM na hivyo kuamua kuhamia Chadema na huko akateuliwa kugombea Ubunge. Alishinda kura na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Karatu na akatokea kuwa moja katika wabunge machachari walioichachafya CCM hadi kujizolea sifa nje na ndani ya bunge. Baada ya muda aliweza kuaminiwa na kila mwanachadema na baadaye uteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Mzee Mwanakijiji, kwa bahati mbaya CCM ni zaidi ya chama cha siasa. CCM ni zao la chama dola na ilirithi kila kitu kilichomilikiwa na chama dola, chama kilichoshika madaraka na chama kilichokuwa na mamlaka ya mwisho katika maamuzi yaliyolihusu taifa hili. Serikali ilikuwa chini ya CCM, Bunge lilkuwa chini ya CCM, mahakama zilikuwa chini ya CCM na vyombo vyote vya dola vilikuwa chini ya CCM. Kuipinga CCM kulitafsiriwa kama uhaini na katiba ya nchi ilifanyiwa marekebisho kwa kuangalia na kutanguliza matakwa ya CCM. CCM ilitumia kila njia kuzuia upepo wa mageuzi na hata pale ilipoonekana wazi kwamba kwa mara ya kwanza wanajaribu kupambana na kile kinachowazidi uwezo, walihakikisha wanayapokea hayo mageuzi kwa maneno lakini si kwa moyo wala matendo.

Waliendelea kuhatamia kila kitu walichokimiliki kama vile vyama vya upinzani havikuwepo, waliendeleza mfumo ule ule kwa nguvu zile zile, wakijilinda kwa mbinu zile zile za wakati wa chama kimoja. Kusema kweli hadi leo hali hii haijabadilika; kinadharia tunavyo vyama vya upinzani lakini kimfumo tunacho chama kimoja, CCM. Mijadala ndani ya Bunge Maalum La Katiba mwanzoni mwa mwaka huu yalizidi kuthibitisha kwamba hatuna upinzani nchini, tunavyo tu vyama vinavyotambulika vitabuni kama vya siasa lakini mchango katika mustakabi wa taifa haupewi umuhimu wowote na CCM. Wakikataa kuunga mkono pendekezo lolote la serikali CCM haijali itaendelea na utekelezaji kama kawaida na wakileta za kuleta, vyombo vya dola vipo kuwadhibiti na kuwatia adabu, kama alivyosema Pinda, wamechoka kuwa wavumilivu hivyo hamna namna na dawa ni kupiga tu.

Mzee Mwanakijiji, CCM kama ilivyo, ni ndoto kuamini kwamba kuna siku itakubali kuachia madaraka kupitia sanduku la kura hata kama wananchi watakuwa wamewachoka. Hii ndiyo sababu wengine tunasema, adui wa nchi hii kwa sasa si Kikwete, si Nape, si Kinana, si Makonda, si Lowassa, si Pinda, hapana, adui wa nchi hii ni mfumo unaoiwezesha CCM kubaki madarakani hata kama haina tena sifa wala uwezo. Katika kipindi kifupi kilichopita serikali yetu imeimarisha sana vyombo vya Usalama, imeagiza mabomu ya machozi, maji ya kuwasha, silaha za moto na vitu kama hivyo. Ukitazama kwa undani, tahayari hizi zote ni katika mipango ya kwadhibiti wananchi na zimetokana na woga, woga wa CCM kuketishwa benchi, woga wa mafisadi kukosa pahala pa hifadhi, CCM na woga wa kuwajibishwa na wananchi kwa vitendo vyao.

Mzee Mwanakijiji, najua yote haya unayafahamu. Najua unajua tahadhari yote hii inatokana na nini. Mwaka 2010 kabla ya Uchaguzi alitokea mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jeneral Shimbo, akiwaonya wanachi kuwa tayari kuyapokea matokeo kama yatakavyotangazwa na Tume na kwamba atakayekaidi atashughulikiwa. Siku chache baadaye akatokea Mhariri Mkuu wa Magazeti ya serikali akiapa kwamba katu upinzani hauwezi kutwaa madaraka ya nchi hii. Haya yalikuwa ni matamshi ya hatari sana katika nchi inayoheshimu utawala wa sheria lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwa hawa wachochezi. Badala yake tumeshuhudia wakiongezewa myadhifa ndani na nje ya nchi. Swali kubwa hapa ji je kama wananchi tunao uhuru gani wa kujichagulia nani atuongoze?

Mzee Mwanakijiji, CCM kama ilivyo imejizatiti kweli kweli kwa lolote lile kuhakikisha hakiyumbishwi na mtu, kikundi au chama, wako tayari kutumia kila mbinu, kila nyenzo na kila silaha kujilinda hata ikiwa ni pamoja na kuvunja katiba. Kwamba kuna medium, hata kama ni mtu, inaweza kusababibisha kwa namna fulani kulisambaratisha hili zimwi, mimi ni katika wale watakaoikaribisha hiyo medium. Zaidi ya hapo hakuna namna, labda kwa kuchukua silaha na kuingia msituni kitu ambacho sikiafiki hata kidogo. CCM ikipasuka vipande vipande kama ninavyoomba mimi, siku hiyo hata mimi nitamwagika mtaani kushangilia, wewe je? Bila hivyo tuanze tu kunyoa tukjitayarisha kwa maumivu kama yale yale tulioaminishwa yangeisha mwaka 1985, 2000, 2005 na 2010.
 
Kutoa matamko nje ya vikao kutasaidia nini!? Bora mkae kimya muendelee kufunga novena zenu msituharibie chama. Dr.slaa alikuwa na mwanya mzuri wa kupenyeza maoni yake baraza kuu,lkn hata wajumbe wa baraza kuu kawapuuza. Kifupi nimeshaanza kumchukia dr.slaa na wanaomuunga mguu!!
 
Alaf uje na hoja kama inshu ni dr slaa kunyimwa au kuna jingne?kwanza kwa cdm kuwa inategemea slaa tu ndo awe mgombea ilikuwa n dalili ya kuwa cdm ni chama kinachotembelea nyota ya watu na si taasisi inayoweza kusimama kwa misingi yake
 
Mzee Mwanakijiji Pasco Hosea 1 : 2 - 3. Na lilikua ni neno/agizo lake la kwanza kabisa kwa Hosea ambalo liluhusisha maisha binafsi.
Ingawa maandiko yanatuambia kuwa alitimiza lakini simulizi za kale zinatuambia haikuwa kirahisi hivyo, awali aligoma kabisa akimshutumu Mungu kwamba haiwezekani yeye kujitoa kote na maisha yake kwa Mungu aishie kuoewa maagizo kama yale, jamaa akagoma na kwenda kuoa mwingine lakini alipozaa naye watoto walikuwa wakifa. Ndipo akaona isiwe shida acha tu atii maagizo.
Pia kuna hili hapa Genesis 22 : 2 - 3 na hii Acts 8:1-4.

Lakini, kama watu watamhusisha Mungu na mageuzi haya, basi hili hapa si la kupuuzwa, 2 Samuel 12:1-18 tujiulize kama kuna mambo kama hayo yaliyowahi kumpata Dr na kama aliwahi kutubu katika hili kama ilivyokuwa kwa Daudi.
 
Last edited by a moderator:
Tusubiri tamko la kijasusi kutoka kwa wanaojifanya wenye chama hata kama wanaharibu. Huo ndo uwazi.

Tangu kipindi cha ZZK nilipata mshituko na CDM. Ni mwanachama ila macho yangu yanaangaza kila kitu kabla sijaamua kutenda.

Sakata la ZZK honestly lilinivunja moyo ,what goes around comes around hii style ya ubakaji demokrasia ya Mbowe itawatafuna sana
 
Kwangu mimi ni halali hata kuiba kura ili ccm itoke madarakani,kwanza washindwe uchaguz alaf km ukawa wakigombana na ccm ikarud 2020 tayar otakuwa imejifunza na kuwa na adabu,hv watanganyika sijuh tukoje,miaka 50 chama kimoja?
 
Sio kweli !

Zitto hakuzuiwa kugombea uenyekiti 2009 ! Aliombwa ajitoe na akajitoa, hakulazimishwa. Angeweza kukataa kama angetaka kuendelea kuwa king'ang'anizi !


kama hujui kitu ni bora kunyamaza. Zitto alipochukua form 2009 alizuiwa hata kupigiwa kura. nahapo zikaanza danadana mara wazee wakaambiwa wamshawishi ajitoe. Tena wakati huo akina bob nyange makani wakiwa hai, huyu edwin mtei unayemsikia kila siku na wengine.
kama kweli demokrasia ilikuwa inazingatiwa ni kitu gani kilichopelekea hayo yote. na baada ya hapo likaundwa zengwe la kuhakikisha zito anafukuzwa kabla ya uchaguzi uliofuta. haya unayoyasema kwa zitto ni matokeo tu na wala sio chanzo cha zitto kufukuzwa chadema hii ya wapiga dili.
hata kabla ya hapo sote tunakumbuka kilichotokea kwa chacha wangwe.
tatizo lenu mmekuwa misukule, hamuoni wala hamsikii. au ndo unaanza kujua mambo sasa hivi kwa hiyo hujui ya hapo kabla.
 
Namheshimu sana Dr SLAA ,naamini ni mapumziko ya muda tu ya kimkakati.mapambano ya kuing'oa ccm yapo palepale.viva UKAWA viva CDM.
 
Katika kipindi hiki cha kukopi na kupesti watanzania bado wanakopi hata kufikiri.
 
Back
Top Bottom