A Program Note: Tutaweka Hoja Zetu Wazi

A Program Note: Tutaweka Hoja Zetu Wazi

Mambo haya wanayotaka kuyaweka hadharani sasa ni kwa faida ya nani?Ninathamini sana michango ya wanachama wote wa CDM kuanzia viongozi wakuu na wanachama wa kawaida,ninaamini DR alishirikishwa hatua kwa hatua kwenye hili la kumpokea EL kama hawakuridhiana bado kulikuwa na nafasi ya kuendelea na maridhiano mpaka suluhisho lipatikane,leo hii naona malumbano yanaaza katikati ya mechi ikiendelea,kwa sisi wapenzi wa mpira kocha anaongea na players wake halftime wakiwa changing room,mkijibizana uwanjani katikati wakati mpira unaendelea ni kumpa adui yako nguvu ya kukupiga bao,tena la mkono alilosema Nape.Mzee Mwanakijiji nachelea kusema ya kuwa upinzani wetu bado sana na itatuchukua watanzania miaka nenda rudi kupata mabadiliko,nahisi wananchi tuko tayari ila viongozi wetu hamna dhamira ya dhati,nilifikiri wapinzani wakuu ambao wangevunja UKAWA na kumkataa EL ni CUF,jana nikamuona Duni Hadji(jembe)nikafarijika sana,ila ninaposoma hizi simulizi zenu nikakumbuka ile hadithi ya mwana mpotevu aliepewa sehemu ya urithi wake akaenda kutapanya na makahaba na ailiporejea kwa baba yake kutubu,yule nduguye muaminifu alikasirika aliposikia nduguye karejea na baba amemchinjia ndama alienona na amemfanyia sherehe,Dr hakupaswa kususa,muungwana hanuni kwa mashavu,hununa moyoni.
 
Kuna mahali tutakuwa tunakosea sana. Kama kuna kuna hoja na iwekwe wazi ijadiliwe, lakini hili suala la eti 'wageni', na nini sijui, halitawajenga zaidi ya kuzidi kuwagaweni.
Naona ni mwanzo wa kufungua milango ya kubaguana, kuna watu watadai wanaostahili zaidi chamani ni wanachama waishio nchini kuliko waishio nje ya nchi. Itafika mahali kabla ya kugombea uongezi mtadai ili kukidhi vigezo lazima uonyesho ngeu au jeraha mwilini mwako ulilolipata katika harakati za 'kukipigania' chama au ulete ushahidi wa mtu wako wa karibu aliyeuawa katika harakati hizi. Kufikia hapo tayari mnakuwa mmeshasahau objective yenu ya kimsingi kwa sababu ya madaraka.
Misimamo mingine ni upofu tu kuendelea kuing'ang'ania, the true meaning of victory has hidden in the truth that, 'sometimes the better way to win is to loose'.
Nisiwachoshe bwana maana waingereza wana kamsemo kao kanasema "behavior is comfort zone". Hivyo basi maamuzi ni yenu, 'mfe mkiwa maadui au mshinde mkiwa mmeungana'.
Msitusumbue sisi na hiyo misimamo isiyoeleweka unless kuna ukweli mnatuficha.

These are true fact my men. Kwenye ukombozi hapaangaliwi nani kaja lini na kaja na nini ilimradi wote mna lengo moja hata kama ulichelewa kujua ukweli,. Chama kilianzishwa na watu wachache sana kikakua taratibu,katika kukua huko wengine walifia njiani wengine waka zaliwa ndivyo kikazidi kuaminika na mpaka leo kiko hapa kilipo, sasa ukisema wanao hamia sasa hivi kutoka upande wa pili wasipewe nafasi kisa wapo waliopata vilema na ngeo sababu ya chama ndio wapewe kipaumbele zaidi je waliokufa? Swala ni kwamba chama kibaki kwenye misingi yake Mla rushwa au yeyote mchafu asipewe nafasi ndani ya chama na hata wale waasisi wakionekana wanatenda kinyume na misingi ya chama tuwakatae sababu walituaminisha chama ni chetu wote
 
Mimi ni kati ya watu waliopinga kwa nguvu nyingi ujio wa Lowassa CDM na mwanzoni nilichukia sana baada ya kudhihirika wazi kwamba amejiunga CDM na anakuwa mgombea Urais.

Baada ya kumsikiliza Mbowe, partly nilikuwa convinced lakini bado sikuwa tayari kuunga mkono Lowassa kupeperusha bendera. Lakini baada ya kutafakari kwa kama siku mbili hivi, nimeamua kuwa behind CDM na UKAWA kwenye hili !

Tuna vifurushi viwili tu na kitu ya hivyo inabidi tufanya uchaguzi wa kimojawapo : Kifurushi cha kwanza ni cha CCM kikiwa na magufuli ndani yake, na Kifurushi cha pili ni cha UKAWA kikiwa na Lowassa ndani yake !. Mimi ninachagua kifurushi cha UKAWA kwani alternative yake ni mbaya zaidi !

MM, nakuheshimu sana ila KWA hili sikuungi mkono , labda kama unamaslahi binafsi Au kama umetumwa !!!
Huu si wakati wa marumbano wala si wakati wa kugawana fito !!!
 
MM, nakuheshimu sana ila KWA hili sikuungi mkono , labda kama unamaslahi binafsi Au kama umetumwa !!!
Huu si wakati wa marumbano wala si wakati wa kugawana fito !!!

Wala si wakati wa kupelekwa kama kondoo. Misingi ya demokrasia iheshimiwe.
 
Ni kweli kuwa nguvu ya EL inaweza overshadow mpaka UKAWA na baadae CDM!?
Mabadiliko yana gharama yake na mikanganyiko mingi na kwa zaidi ya miaka 10 sasa Watanzania wanaiangalia ccm kama kikwazo badala ya mtu mmoja mmoja ndani yake hivyo kuanguka kwa ccm inaweza kuwa hatua mbele kuliko kuuogopa kutokuwa tayari kwa UKAWA/CDM.
Of course ccm ni 'mbuyu mkubwa' hivyo unakoangukia ni lazima kuna baadhi ya vimiti vingine chini yake vitaanguka pia na tuangalie woga wetu usijekuwa nasi ni miongoni mwa vimiti vilivyo chini ya mbuyu.
 
Back
Top Bottom