Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 369,733
- 855,779
Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga mkoani Kagera, Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza, amesema kuna watu na makundi katika jamii ya leo yanayotumia nguvu, risasi na mabomu ya machozi kwa sababu ya kushindwa hoja, akifananisha tabia hiyo na akina Herode waliokataa kumpokea Yesu Kristo, Mfalme wa Amani.
Akizungumza katika Homilia yake, Askofu Rweyongeza amesema watu wanaoshindwa katika hoja, tafakari, midahalo na maridhiano mara nyingi hukimbilia matumizi ya nguvu ili kunyamazisha sauti za wanaotumia hoja na fikra.
Amesema kundi la kwanza la watu wasiompokea Yesu ni akina Herode, akiwataja kuwa ni watu wenye ubinafsi, uchu wa madaraka na ukatili, ambao hawapendi kushauriwa, kuonywa wala kusemwa, na badala yake hutumia nguvu pale wanaposhindwa hoja.
Askofu huyo amesema kundi la pili ni Mafarisayo, aliowataja kuwa ni wanafiki wanaotumia dini kama kifuniko cha kufanikisha ajenda binafsi, huku wakijifanya wacha Mungu lakini kwa vitendo wakijihusisha na vitendo vya ufisadi, unyonyaji na uharibifu wa taasisi za dini.
Ameongeza kuwa kundi la tatu ni la Yuda Iskariote, watu wanaomsaliti Yesu kwa busu, yaani wanaoonekana watakatifu kwa nje lakini ndani wakitafuta namna ya kunasa, kuharibu au kunufaika binafsi kupitia mali, sadaka na rasilimali za Kanisa.
Katika homilia yake, Askofu Rweyongeza amesema kundi la nne ni la akina Pilato, watu wanaoujua ukweli lakini huchagua kunawa mikono na kukaa kimya, wakiruhusu dhuluma, uonevu na mauaji ya haki kufanyika bila kuchukua msimamo wa wazi.
Ameeleza kuwa kundi la tano ni la wale aliowafananisha na Wayahudi waliomsulubisha Yesu, akiwataja kuwa ni watu wanaodhalilisha, kuumiza, kupora mali za waathirika, kuwanyonya wanyonge na hata kuwanyima yatima haki zao baada ya vifo vya wazazi wao.
Askofu Rweyongeza amesema makundi hayo bado yapo katika jamii ya leo na yanaendelea kutokumpokea Yesu kwa sura mbalimbali, licha ya kusherehekea Krismasi na kutambua kuzaliwa kwake.
Hata hivyo, amesema bado wapo watu wanaompokea Yesu kwa matendo yao, kwa kuishi katika haki, amani, maridhiano na kulinda utu wa binadamu, jambo ambalo amesema ndilo msingi wa ujumbe wa Krismasi.