A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

"Ndugu zangu,

Najaribu kutuliza mawazo ili angalau niweze kuwapa kidogo tulipofikia na tunakoelekea juu ya suala hili. Kwa kweli haivumiliki ukimwona ulimboka kwa jinsi alivyotendewa na hali aliyonayo; kwa wale wanaojua hali za kitabibu, "this is a very unstable condition that demands permanent watch 24/7".

Kwa taarifa tulizokusanya, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani) na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu". Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi.

Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...

Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili.

Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'. Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na Redio Call, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.


Nashindwa kuendelea....."
NB: Haya ni maelezo ya mwanaharakati Albanie Marcossy aliyehusika kumsaka kama nilivyoyanukuu Mabadiliko Group.

Hapo kwenye red, nani kasimulia!? Just curious!
 
Ndugu zetu wangapi wamepoteza maisha katika mgomo wa kwanza mbona hukusema kitu, leo Uli unajifanya kuongea sana, acha unafiki wa mawazo.

Unajitoa akili kwa kuwabebesha madaktari lawama huku ukijua wazi muhusika mkuu wa kadhia hii....roho za waliopoteza maisha pamoja na damu ya Ulimboka na maumivu yake na Watanzania yako juu ya Serikali ya CCM.
Ulipopiga kura uliingiza jina la Dr Ulimboka kwenye ballot box au jina la Dr yoyote for that matter. THINK
 
Kama huamini kuna serikali na uwe wa kwanza kuingia barabarani wengine tutajifunza kutoka kwako

Kalieni uoga hivyo hivyo na kuja kujisifia kwa uoga,siku tukilianzisha hata waoga kama wewe mtakuwa wa kuwanyonga tu,yaani waue tuwaangalie tu? Ni bora anayepinga serikali haikufanya hili kuliko maneno yako hapo juu!umenikera mno. Kwa hiyo hawa washenzi wakiingia kwako wakamtia vid*le kila mtu mtacheka cheka tu sio? Kama ikithibitika kuna mkono wa serikali katika hili,hii ni sababu tosha ya kuingia barabarani na kudai wahuni waachie nchi yetu!
 
aisee... bora kuharakisha uraia mwinginee...this rotten tz is tooo much...bora uende bongo kama mtalii tu tena unashukia direct home kwenu buuut as mtalii...may be..i hate this injustice
 
if they wanted him dead, he'd be dead by now, na mngekuwa mnaongea mambo mengine kabisa.......probably, they still need him for something..........the big question is wat is it??

And kimtazamo wangu, 1st, wat has bin done to him isnt fair, unless, he(ulimboka) framed it....najua kwa hili, wengi mtanilaumu, but mkisoma stories nyingi kama hizi, mtaona, ulimboka hatokuwa wa kwanza, kufake something like this, but for good reasons..............cause, seriously, kama wangetaka afe, angekufa longtym........

2dnly, killing one person for the benefit of two or more people, i find it reasonable................
umetumwa??? Umelogwa??? Unafake unajivunja mbavu??? Hivi watu kama nyinyi huwa mnaishi wapi?? Ungekuwa karibu yangu maji ya mto kwenye oblangata yako yangehusika! Hebu nenda kaongee na wakina gerald hando na mwenzio kibonde labda mna umbeya mwaweza ongea!
 
kauli tata ya "liwalo na liwe" imeanza kufanya kazi kabla

Watu wasimwamini sana huyu Bwana, kwa haraka haraka unaweza kumwona ni mtu mwenye huruma na mpole lakini amekuwa mtu wa system kwa miaka mingi. Alipomwambia kuwa 'isije ikatokea akagongwa na gari au kushambuliwa na majambazi ---, alikuwa anajua vizuri sana njia ambazo zilikuwa na uwezekano mkubwa kutumika'. Njia ya gari imekuwa ikitumika san. Kayombo, aliyefichua uingizaji wa mihadarati alikufa (kwa kutatanisha), container la cocaine likatoweka, na inasemekana liliondokea bandari ya Mtwara, aliyeenda kufanya uchunguzi kule bandari ya Mtwara, tunaambiwa alifariki kwa ajali ya gari akiwa anatokea Mtwara, Gibons Mwaikambo ambaye inasemekana alikuwa amekuja Dar kutangaza kujiunga na chama cha upinzani alifariki kwa kile kilichotajwa gari yake kugonga mti Oysterbay lakini walioshuhudia gari alilokuwemo wanasema lilibomoka vibaya sana vioo vyake vyote lakini mabaki ya vioo kwenye barabara yalikuwa yanajaa kiganja cha mkono, Imrani Kombe aliuwawa baada ya kutoka kwenye gari kwa kujisalimisha kwa kile kilichotajwa kuwa kufananishwa na jambazi, n.k. hayo ni machache tunayoyajua. Kwa hiyo inaonekana alikuwa akijua njia zinazotumika na hawa wataalam wa vifo.
 
tumeonewa vya kutosha, tumedharauliwa vya kutosha, tumenyanyaswa vya kutosha sisi ma dr. wa tz na wananchi kwa ujumla , nadhani ktk hili tusipoandamana kuuondoa uongozi wa kinazi wa serikari ya tz mawe yatapaza sauti na historia itatushitaki kizazi hiki. URIMBOKA mungu wetu akuponye kwa damu ya YESU.
 
Sasa ndo watu wataamini kwamba tunaongozwa na genge la wauaji. Kikwete na serikali yake ni mumiani wanyonya damu za watu.
Mungu amsaidie dr Ulimboka.
 
DHAMBI HII NI BAADHI YA MAMBO YANAYOLIGHARIMU TAIFA.

SI uzushi wala uchochezi. Tanzania inaelekea pabaya tena sana.

Tangu kuingia kwa mchezo mchafu wa kikundi cha watu tena wachache kujihudumia na kutafuta utajiri kwa kuwauza wenzao, Tanzania si salama ingawa hakuna milio ya bunduki.

Uliza. Yako wapi mapambano dhidi ya ujambazi, ufisadi (ugamba), biashara ya mihadarati, kurekebisha mikataba ya kijambazi ya uwekezaji ambao ni uchukuaji na uwajibikaji? Si siri.

Kwa sasa Tanzania iko mikononi mwa maharamia tuseme majambazi hasa kiuchumi. Imefikia mahali majambazi yaitwayo wawekezaji yanakuja na kutuibia mchana kweupe kwa kushirikiana na wenzetu waroho wachache tuliwaamini.

Uliza uwekezaji kwenye Shirika la Reli uliishia wapi ilipoingia kampuni ya Kihindi iitwayo RITES?

Mijitu inakuja bila hata senti halafu eti inawekeza kwa kuilazimisha serikali iwape mikopo ili waendeleze mradi! Ni wawekezaji wangapi wanakuja na briefcases zao na makaratasi na kurejea kwao wakiwa na magunia ya dola?

Uliza. Ni wawekezaji wangapi hasa kwenye madini wanamiliki ndege na viwanja binafsi vya ndege wanavyotumia kutoroshea madini yetu bila kukaguliwa?

Ni wangapi wanachafua mazingira na hakuna anayewawajibisha?

Hebu zidi kupiga mbizi kwenye uchafu huu uone mengi. Hakuna ujambazi wa wazi kama unaofanywa na makampuni ya simu kwa sasa.

Wanakuja na kuweka mitambo chakavu halafu wanawatoza Watanzania viwango vya juu vya kutumia simu.

Huwa najiuliza. Inakuwaje kupiga simu, kwa mfano, kutoka Canada kwenda Kenya nitozwe senti tano za dola na Tanzania nitozwe senti 27 za dola kwa dakika?

Wakati viwango vya Kenya ni vidogo, mawasiliano baina ya Kenya, Uganda, Rwanda hata Burundi ni bora na rahisi wakati Tanzania ni utapeli mtupu.

Mtu unapiga simu unaambiwa ongeza salio, mara namba ya simu haipo, mara simu inatumika mara hili mara lile.

Kwanini hatusikii upuuzi huu tunapopiga nchi tulizotaja hapo juu kama hakuna namna?

Ajabu ya maajabu, kila mwaka makampuni ya simu yanabadilisha majina ili kuendelea kufaidi msamaha wa kipuuzi wa kodi.

Angalia mahoteli yenu yanavyobadili majina na wamilki kila baada ya miaka mitano ili kuendelea kufanya biashara bila kulipa kodi. Angalia watu wanavyouziana makampuni waliyookota Tanzania kwa bei ya kutupwa.

Anayebishia hili ajikumbushe Richmond ‘ilijiuza’ kwa Dowans kwa bei gani ikilinganishwa na bei ya maandishi tu bila kulipa pesa iliyoianzishia biashara hii hewa.

Leo tunaambiwa kuwa pesa tunayoilipa IPTL, kwa mfano inatosha kununua na kujenga mitambo bora na mikubwa kuliko tunayolipia.


Je, kwanini tunaona kujikomboa ni dhambi wakati tukiabudia maangamizi kama haya ya IPTL na makampuni mengine mengi ya nishati.

Je, hapa hakuna rushwa na ufisadi vya wazi? Je, wahusika hawajulikani? Nani anawagusa wala kuwashughulikia? Tunakwenda wapi?

Imefikia mahali watu wakiuliza ni kwanini uchafu huu unaendelea wakati kuna mamlaka, wanakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Jiulize. Mbunge wetu mmoja alipatwa na nini baada ya kuhoji ni kwanini alikuwa akiona watumiaji wa mihadarati hadharani ambao wangeweza kutuonyesha wanakonunua madawa.

Tufikie mahali tuambiane ukweli bila kuogopana wala kufichana. Bila kufanya hivyo na kubadilika nchi yetu itaishia pabaya.

Ni juzi juzi serikali ya Mali imeangushwa kutokana na hasira za jeshi kushuhudia wauza unga wakiwa ndani ya serikali na serikali isifanye kitu kwa vile wakubwa zake walikuwa wakinufaika na uchafu huu.

Je, sisi tu salama na hawa wauza unga na majambazi wa kiuchumi waliotapakaa nchini mwetu? Je, wananchi wataendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli kila mwaka?

Huwa siachi kusema kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu hata kama hawana mikia au macho kisogoni.

Maana ukiangalia kwa mfano, rasilimali zao zinavyoibiwa, wanavyolanguliwa huduma kama vile umeme, simu na mahitaji mengine na wakaendelea kuvumilia unashangaa hawa ni watu wa namna gani.

Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?

Je, kama KIA wana uwezo wa kutorosha wanyama hai na wengi kiasi hiki wanashindwa nini kuingiza maelfu ya tani za unga?


Ukitaka kujua nini namaanisha, watafute wafanyakazi wadogo na wa kawaida viwanja vya ndege uone walivyo matajiri wa kutupwa.

Unadhani pesa hii wanaipata wapi kama si kuruhusu uchafu na jinai kama ile ya KIA......................

Nenda TRA, Bandari, Uhamiaji. Mambo ni yale yale. Uchafu, uchafu mtupu. Nani anajali iwapo wanaofaidika wameweka watu wao kufanya kazi hiyo? mfano, vituo vyetu vya mipakani vimegeuzwa maduka ya wezi wachache kupitisha wamtakaye na wakitakacho bila kuulizwa na yeyote?

Je, namna hii nchi itakuwa salama? Je, namna hii tunaweza kujisifu kuwa yaliyotokea Mali hayawezi kutokea huko tuendako ambapo wahusika wasiporekebisha hali hii wananchi katika hali yoyote wataamua ‘enough is enough’.

Tumekuwa taifa la hovyo linalowazawadia watenda maovu!

Uliza waliotimuliwa madarakani kwa kashfa wanalipwa pesa ya umma kwa kazi gani zaidi ya kupaswa kuwa mahakamani hata magerezani? Tumegeuka taifa la watenda maovu na waovu kirahisi hivi?

Je, baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini? Tunaviandalia nini vizazi vijavyo iwapo tunafanya mambo kama mataahira kutokana na kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa?
 
Siamini kama Mkuu wa kaya, anayajua haya. Siamini kama hii ndiyo Tanzania, Nchi yangu niliyoipenda sana, Siamini, Siamini, Siamini!!
Nasema tena, sitaki kuamini kama huko ndiko tulikofika.
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA.
 
unajitoa akili kwa kuwabebesha madaktari lawama huku ukijua wazi muhusika mkuu wa kadhia hii....roho za waliopoteza maisha pamoja na damu ya ulimboka na maumivu yake na watanzania yako juu ya serikali ya ccm.
Ulipopiga kura uliingiza jina la dr ulimboka kwenye ballot box au jina la dr yoyote for that matter. Think
eliza sweetherat hawezi ku-think coz akili yake imelewa u.j.i.n.g.a wa chama cha machangu!
Nawachukia wale wote wanaisuport ccm! Ni bora kutokuwa na serikali!
 
Serikali na Usalama wameumbuka walizani wameuwa,
Damu ya Ulimboka itakuwa chachu ya ukombozi wa Tanzania (Tunisia)
ya pili hiyo imewadia
 
kama huamini kuna serikali na uwe wa kwanza kuingia barabarani wengine tutajifunza kutoka kwako
wewe kama ni mwanaume ni hasara kwa nchi hii, huna faida! Na kama ni mwanamke, beba ujasiri tuliojaliwa wa kuleta binadamu duniani tuwapo labour, tetea nchi yako! Acha uoga!
 
Wanaodai/kutetea haki zao wanauwawa wanateswa.Kama Serikali ilidhani kwa kumuua Dkt Ulimboka ndio itamaliza tatizo la mgomo wa madaktari nnadhani wamepiga hesabu vibaya,haki ya mtu haipotei huwa inacheleweshwa tu.Hakuna ufalme utakaodumu milele,utafika wakati tutawafungulia mashitaka viongozi wote waliohusika na mabaya katika nchi hii na sio mbali ni karibu kuliko na wanavyofikiri.
 
Hongera kaka!

Mimi nadhani ingekuwa busara mheshimiwa kiongozi wa madaktari Dr Ulimboka ajiuzulu mara moja kwa sababu wakati anafanya mazungumzo na hao jamaa kama alizungumza nao kama mwakilishi wa madaktari bila kupata idhini ya chama cha madaktari ni makosa makubwa!!
 
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.
 
Back
Top Bottom