Hayati Mwinyi ametufundisha kukiri tunapofanya makosa

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,060
Hayati Rais Mwinyi, tofauti na viongozi wote wa CCM wa sasa hivi, ndiye pekee ambaye alikuwa tayari kukiri kukosea inapodhihirika alifanya makosa. Hiyo ni tabia ya mtu muungwana, mtu anayeamini kuwa kwa kuwa Rais haimaanishi umeuvua ubinadamu.

Hayati Mwinyi aliwahi kujiuzulu uwaziri akiwa waziri wa mambo ya ndani kutokana na polisi kuua raia. Mwinyi aliona kuwa kwenye kosa lile la polisi, yeye kama kiongozi wa wizara inayohusika na polisi, basi anahusika. Viongozi wa sasa, hata pale ambapo wamehusika moja kwa moja kwenye makosa ya wazi, kamwe husikii wamejiuzulu. Kuna mawaziri, wizara zao zinatajwa kuiba na kufisadi pesa za Watanzania lakini kujiuzulu ni kitu ambacho hakipo katika mioyo yao. Wa mwisho kujiuzulu alikuwa Hayati Lowasa.

Mwinyi akiwa Rais, ndipo Zanzibar ilipojiunga na OIC, kinyume na matakwa ya katiba kwani wanachama wa OIC huwa ni mataifa huru na Zanzibar siyo nchi. Serikali yake na yeye mwenyewe waliposhambuliwa sana, siku Hayati Mwinyi alipotangaza uamuzi wa kujitoa OIC alisema yafuatayo:

'Mahali tulipokuwa (akimaanisha shida ya pesa) ni sawa na mtu aliyetumbukia majini, anahangaika kujiokoa, katika kutapatapa, akashika tawi ili kujiokoa, baadaye kuja kulitazama tawi lile limeandikwa OIC. Baadaye ndiyo tumegundua tumefanya makosa. Nawatangazia wananchi wenzangu, Zanzibar imekwishajitoa OIC". Viongozi wetu wa sasa, hata wanapofanya makosa ya wazi, kwao haiwezekani kukiri kufanya makosa. Tena bahati mbaya sana, Rais Samia aliwahi kutangaza wazi kuwa eti Rais hawezi kufanya makosa. Kuna kosa la wazi la IGA kuhusiana na bandari, lakini watu wameng'ang'ania hata wakati ambapo kila mmoja anaona kuna makosa ya wazi.

Tunapomlaza mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, viongozi mjitafakari sana. Mjiulize mnabeba nini kutoka kwa mzee wetu huyu tunayemlaza kesho.

Wakati wa utawala wa Mwinyi, sikuwahi kusikia habari za kutekwa watu kama ilivyokuwa kwa Dr. Ulimboka, wala sikusikia mtu aliuawa kinyama kama alivyofanyiwa Hayati Mwangosi (wakati wa utawala wa Kikwete), au kama alivyofanyiwa Lisu, Ben Sanane, Kanguye, Mdude (wakati wa utawala wa Magufuli), ama alivyofanyiwa Mbowe (wakati wa Samia).

Mzee Mwinyi alielewa na kuthamini uhai wa wengine kama ulivyo wa kwake, alielewa kuwa Urais ni wajibu tu lakini yeye bado ni mwanadamu ambaye anaweza kukosea au akafanya vema. Halafu hakuwahi kuwa na Kisasi. Pale ulipojiuzulu uwaziri, nyumaa yake alipewa Hayati Makweta. Licha ya kumwomba Makweta ampe nafasi ya kujiandaa kuachia nyumba, Makweta alikataaMwinyi akaondoka kwa dharura huku akiitawanya familia yake, wengine wakaishi kwa Kitwana Kondo na wengine kwa Mustafa Nyang'anyi. Lakini alipoupata Urais, bila kinyongo akamteua Makweta kuwa Waziri. Huu ni moyo ambao viongozi wa sasa wa CCM hawana. Wao wanaabudu kisasi. Viongozi, choteni hekima hii toka kwa marehemu maana mmepungukiwa sana.

Mwinyi alipozungumzia kuhusu matokeo mabaya ya sera ya ubinafsishaji, alihihimisha kwa kusema, "mwanadamu hata ukifanya makosa, kama dhamira yako ilikuwa njema, Mungu hulitakatifuza kosa lile. Lakini hata ukifanya vema, kama dhamira yako ilikuwa mbaya, hata lile jema ulilolifanya, Mungu hulitia unajisi". Aliyasema hayo akimaanisha kuna mambo wamefanya vibaya, lakini dhamira yao ilikuwa njema, hivyo Mungu amewasamehe kwa makosa yale.

Pole sana Hussein Mwinyi na wanafamilia wote. Pamoja na mzee wetu huyu kujaliwa umri wa miaka 98, lakini hakika hakuna umri ambao mtu unayempenda unasema unatosha.

Kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu, tumshukuru Mungu kwa kila jambo, tumshukuru Mungu kwa kutupatia mzee Mwinyi, na yale mema yote yaliyoambatana na maisha yake. Msiba wa Mzee mwinyi utulete pamoja zaidi, uwakumbushe watawala walipopotoka, na Watanzania wote tujikumbushe umuhimu wa kuthamini maisha ya wenzetu, umuhimu wa kukiri makosa tunapokosea, umuhimu wa kusamehe na kuachana na maisha ya visasi na kukomoana.

Kwa heri mzee Ali Hassan Mwinyi. Wewe hukuwa mtawala bali rafiki wa Wanadamu wenzako.
 
I'll alituleteee zimwi la OBC kampuni ya kitaeli ya uwindaji loliondo
Ndio inawafanyia vigisu wamasai

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Viongozi wote wana madhaifu yao na hawa wetu kutoka Mikoa ya Pwani na Visiwani udhaifu wao ni kwamba wanawaona Waarabu kuwa ni Ndugu zao katika Imani.

Hali kadhalika Viongozi wetu wa Nyanda za Juu Kusini kwa Wazungu.
 
Kwenye msiba kiwango cha unafiki huwa % kwa kanuni ile ile ya asili kwamba marehem hasemwi vibaya.watawala watao pata nafasi ya kutoa neno wataonesha kiwango cha unafiki kwa kauli za kulinda mazuri na kujifunza kumbe ni maneno ya sifa tu lakini matendo yao ni kiza.

Mzee Mwinyi alikuwa na roho kama ya Nelson Mandela.
 
Kwakweli maisha yake yametufaa sana watanzania

Awe na pumziko jema

Hakuhangaika kutafutia vitukuu mali kwa njia haramu au za mkato. Hata wale walioingia kwenye siasa, waliingia kwa mlango rasmi. Sio kwa giliba wala hila za Mstaafu. Mstaafu alituheshimu sana watanzania na tunachoweza kumpa, ni kumuombea kheri mbele ya haki.

Kama binadamu, sote tunakosea na tunachoweza kusema ni kuombea dua na kheri, ili Mwenyezi Mungu atupe msamaha.
 
Hayati Rais Mwinyi, tofauti na viongozi wote wa CCM wa sasa hivi, ndiye pekee ambaye alikuwa tayari kukiri kukosea inapodhihirika alifanya makosa. Hiyo ni tabia ya mtu muungwana, mtu anayeamini kuwa kwa kuwa Rais haimaanishi umeuvua ubinadamu.

Hayati Mwinyi aliwahi kujiuzulu uwaziri akiwa waziri wa mambo ya ndani kutokana na polisi kuua raia. Mwinyi aliona kuwa kwenye kosa lile la polisi, yeye kama kiongozi wa wizara inayohusika na polisi, basi anahusika. Viongozi wa sasa, hata pale ambapo wamehusika moja kwa moja kwenye makosa ya wazi, kamwe husikii wamejiuzulu. Kuna mawaziri, wizara zao zinatajwa kuiba na kufisadi pesa za Watanzania lakini kujiuzulu ni kitu ambacho hakipo katika mioyo yao. Wa mwisho kujiuzulu alikuwa Hayati Lowasa.

Mwinyi akiwa Rais, ndipo Zanzibar ilipojiunga na OIC, kinyume na matakwa ya katiba kwani wanachama wa OIC huwa ni mataifa huru na Zanzibar siyo nchi. Serikali yake na yeye mwenyewe waliposhambuliwa sana, siku Hayati Mwinyi alipotangaza uamuzi wa kujitoa OIC alisema yafuatayo:

'Mahali tulipokuwa (akimaanisha shida ya pesa) ni sawa na mtu aliyetumbukia majini, anahangaika kujiokoa, katika kutapatapa, akashika tawi ili kujiokoa, baadaye kuja kulitazama tawi lile limeandikwa OIC. Baadaye ndiyo tumegundua tumefanya makosa. Nawatangazia wananchi wenzangu, Zanzibar imekwishajitoa OIC". Viongozi wetu wa sasa, hata wanapofanya makosa ya wazi, kwao haiwezekani kukiri kufanya makosa. Tena bahati mbaya sana, Rais Samia aliwahi kutangaza wazi kuwa eti Rais hawezi kufanya makosa. Kuna kosa la wazi la IGA kuhusiana na bandari, lakini watu wameng'ang'ania hata wakati ambapo kila mmoja anaona kuna makosa ya wazi.

Tunapomlaza mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, viongozi mjitafakari sana. Mjiulize mnabeba nini kutoka kwa mzee wetu huyu tunayemlaza kesho.

Wakati wa utawala wa Mwinyi, sikuwahi kusikia habari za kutekwa watu kama ilivyokuwa kwa Dr. Ulimboka, wala sikusikia mtu aliuawa kinyama kama alivyofanyiwa Hayati Mwangosi (wakati wa utawala wa Kikwete), au kama alivyofanyiwa Lisu, Ben Sanane, Kanguye, Mdude (wakati wa utawala wa Magufuli), ama alivyofanyiwa Mbowe (wakati wa Samia).

Mzee Mwinyi alielewa na kuthamini uhai wa wengine kama ulivyo wa kwake, alielewa kuwa Urais ni wajibu tu lakini yeye bado ni mwanadamu ambaye anaweza kukosea au akafanya vema. Halafu hakuwahi kuwa na Kisasi. Pale ulipojiuzulu uwaziri, nyumaa yake alipewa Hayati Makweta. Licha ya kumwomba Makweta ampe nafasi ya kujiandaa kuachia nyumba, Makweta alikataaMwinyi akaondoka kwa dharura huku akiitawanya familia yake, wengine wakaishi kwa Kitwana Kondo na wengine kwa Mustafa Nyang'anyi. Lakini alipoupata Urais, bila kinyongo akamteua Makweta kuwa Waziri. Huu ni moyo ambao viongozi wa sasa wa CCM hawana. Wao wanaabudu kisasi. Viongozi, choteni hekima hii toka kwa marehemu maana mmepungukiwa sana.

Mwinyi alipozungumzia kuhusu matokeo mabaya ya sera ya ubinafsishaji, alihihimisha kwa kusema, "mwanadamu hata ukifanya makosa, kama dhamira yako ilikuwa njema, Mungu hulitakatifuza kosa lile. Lakini hata ukifanya vema, kama dhamira yako ilikuwa mbaya, hata lile jema ulilolifanya, Mungu hulitia unajisi". Aliyasema hayo akimaanisha kuna mambo wamefanya vibaya, lakini dhamira yao ilikuwa njema, hivyo Mungu amewasamehe kwa makosa yale.

Pole sana Hussein Mwinyi na wanafamilia wote. Pamoja na mzee wetu huyu kujaliwa umri wa miaka 98, lakini hakika hakuna umri ambao mtu unayempenda unasema unatosha.

Kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu, tumshukuru Mungu kwa kila jambo, tumshukuru Mungu kwa kutupatia mzee Mwinyi, na yale mema yote yaliyoambatana na maisha yake. Msiba wa Mzee mwinyi utulete pamoja zaidi, uwakumbushe watawala walipopotoka, na Watanzania wote tujikumbushe umuhimu wa kuthamini maisha ya wenzetu, umuhimu wa kukiri makosa tunapokosea, umuhimu wa kusamehe na kuachana na maisha ya visasi na kukomoana.

Kwa heri mzee Ali Hassan Mwinyi. Wewe hukuwa mtawala bali rafiki wa Wanadamu wenzako.
Siyo Rais pekee aliyewahi kufanya hivyo..Kuna aliyemtangulia.
 
Kwakuwa Mpaka sasahivi vyama vya upinzani havijachukua madaraka ya kuongoza nchi kama nchi nyingine huko duniani kilichobaki kwa sasa angalau ni kuwaweka Mzee Nyerere na Mzee Mwinyi Kama kipimo cha uongozi Kwa wote waliofuata baada yao Kwenye chama chao.
 
Back
Top Bottom