A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

Mkuu wa emergency dept anazuia gari kwenda kumchukua Daktari mwenzake aliyeokotwa akiwa hajitambui?
Aisee ndiyo maana migomo yenu haifanikiwi wakuu...

Hii yote ni sababu ya unafki na ubinafsi wa wa TZ.
 
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.

mnatutia mashaka, wananchi hatuna amani wala imani, hebu tuwekeni sawa
 
Jamaaaaaaaaaani,watayalipa yote haya,damu yako uli,ni ishara ya ushujaaa
 
Kwanza kabisa siungi mkono kwa jinsi iwayo yote matumizi ya nguvu kwa mwananchi wa kawaida kama Dr. Ulimboka. Yeyote aliyefanya ama kuruhusu haya kufanywa ni mtovu wa maadili na hapaswi kuwa uraiani - sehemu stahiki anayotakiwa kupelekwa ni segerea ama eneo jingine linalofanana na hilo. Ila bado nina utata kuhusu mazingira aliyokamatiwa Dr. Ulimboka. Walikuwa wanafanya nini kwenye hivi vikao vya usiku alivyokuwa akifanya na wenzake? Je vilikuwa vinahusu nini? Inakuwaje masuala ya mgomo wa madaktari yajadiliwe usiku wa manane kwani kwani yamekuwa uchawi?

Kwanza kabisa tunatakiwa kupatiwa majibu. Je ni nani alimpigia simu? siku hizi kuna utaratibu maalum wa kusajili simu, kama hatapatikana basi kazi yote ya kusajili simu ni uchwara, haina maana yeyote haiwezi kuwa na maana iliyotarajiwa.

Kama kuna mtu anatarajiwa kuwa polisi watasaidia kitu basi wanajidanganya. Polisi wetu hata siku moja hawapo upande wa haki, wako upande tofauti, wapo kuwalinda wali madarakani na wanaofanya uhalifu mkubwa. So forget it.

Na sasa kuna kampeni moja nzuri ya ku deal na watu kutoka Mbeya, inaonekana wanaisumbua serikali. Kwanza ni yule Profesa aliyeuawa, mwakyembe na Mwandosya wameponea chupuchupu, sasa Ulimboka, the list will go on.

Naamini kuwa hakuna kitakachofanyika, hakuna atakayejiuzulu, hakuna atakayewajibika, wanachi watadanganywa danganywa tu na upepo utapita. At the end of the day, madaktari wataendelea kunyonywa. Tuombe Mungu wanajeshi wadai nyongeza ya mishahara.....walimu na madaktari bure kabisa, ni wa kuchinjwa tu na kupigwa.
 
Ndugu zetu wangapi wamepoteza maisha katika mgomo wa kwanza mbona hukusema kitu, leo Uli unajifanya kuongea sana, acha unafiki wa mawazo.
Acha upumbavu wewe ndugu zako c ndo huwa wanaenda kutibiwa india! Unapenda huduma za dhaifu za hospital zetu?
 
If they wanted him DEAD, he'd be dead by now, na mngekuwa mnaongea mambo mengine kabisa.......probably, they still need him for something..........the big question is wat is it??

and kimtazamo wangu, 1st, wat has bin done to him isnt fair, Unless, he(ulimboka) framed it....najua kwa hili, wengi mtanilaumu, but mkisoma stories nyingi kama hizi, mtaona, ulimboka hatokuwa wa kwanza, kufake something like this, but FOR GOOD REASONS..............cause, seriously, kama wangetaka afe, angekufa longtym........

2dnly, killing one person for the benefit of two or more people, i find it reasonable................

Too low !
 
Hawa ndio watanzania ndugu yangu likishatokea jambo kila mmoja anatengeneza story yake. Hakuna tofauti na hekaya ya Abunuasi


MWISHO WA WA UBAYA NI AIBU,jitahidi usiwe mmojawapo wa wanaosapoti kuwa Serikali haikuhusika na kumbuka maneno yako ya leo ndio pingu yako kesho.
 
Serikali na Usalama wameumbuka walizani wameuwa,
Damu ya Ulimboka itakuwa chachu ya ukombozi wa Tanzania (Tunisia)
ya pili hiyo imewadia

Ni wakati sasa umefika. Tupange tu mkakati sasa wa kuing'oa hii nchi.
 
"Ndugu zangu,

Najaribu kutuliza mawazo ili angalau niweze kuwapa kidogo tulipofikia na tunakoelekea juu ya suala hili. Kwa kweli haivumiliki ukimwona ulimboka kwa jinsi alivyotendewa na hali aliyonayo; kwa wale wanaojua hali za kitabibu, "this is a very unstable condition that demands permanent watch 24/7".

Kwa taarifa tulizokusanya, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani) na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu". Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi.

Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...

Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili.

Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'. Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na Redio Call, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.


Nashindwa kuendelea....."
NB: Haya ni maelezo ya mwanaharakati Albanie Marcossy aliyehusika kumsaka kama nilivyoyanukuu Mabadiliko Group.

Ninaandika maneno machache lkn nikiwa na uchungu mkubwa na ninajua hamna namna ya kuuelezea uchungu nilio nao na hata watanzania walio nao nchi mzima juu ya kilichompata Ndugu yetu Ulimboka!!!! Lkn na sisi tunasema kuwa tuko tayari kufa pia, polisi jueni hivyo, usalama wa taifa jueni hivyo, serikali ijue hivyo na hata CCM ijue hivyo!!!!! NIKO TAYARI KUFA, TUKO TAYARI KUFA!!!!! For the sake of our Nation, we are ready to die, for the sake of the next generation we are ready to die, for the sake of our sons, daughters, children of our children, we are ready to die!!!! lazima Waziri mkuu, waziri wa mambo ya ndani, waziri wa afya wajiuzulu na baadae Rais wajiuzulu, hatuwataki!!!
 
Tatizo kubwa ni siasa kuwa juu ya kada zote muhimu kwa taifa changa kama tanzania kada zote ikiwezekana pasiwepo siasa.Hii inadhihilisha jinsi gani siasa ilivyo mbaya sana kwa kada zote,nasema siasa ni mbaya kwasababu kama daktari asingekuwa na cheo hicho yasingemkuta yaliyomkuta.
 
Wewe unajuaje alikuwa peke yake ?
Umesoma maelezo au unakurupuka tuu as if umeamka kutoka ktk kilabu ya chibuku. Imeelezwa kuwa alikuwa na wenzake, na mtu aliyemuita chembaz ni mtu ambaye wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara. Yaani really unafikiri sio kweli kuna vifaa duni, maslhai mfu na unadhani hao wote madaktari na mabingwa ni wajinga kiasi cha kuweza kushawishiwa kirahisi kugoma just for the sake ya kugoma ? It seems ww ndo una njaa !!

Huyo Dr Ulimboka siyo COMANDO,atakuwa ni mla rushwa (CORRUPT) sana na inavyoonekana anaweza kuwauza wenzake.Nasema hivyo kwa sababu ukiiangalia hii incidence unaona kuwa huyu Dr Ulimboka ana tamaa ya pesa na anaendesha mgomo kwa kushawishi wenzake ili anufaike binafsi.Nasema hivyo kwa sababu hebu fikiria kwa akili ya kawaida tu,wewe una ishu kubwa kama hiyo ya mgomo,halagu unaitwa na mtu usiyemjua ili mkafanye reconcilliation na wewe unaenda tena peke yako!!!!.Bila shaka ni reconcilliation kuhusu mgomo.Hapo naona kuwa anaweza kuitwa na watu asiowajua na yeye akaenda tena peke yake!!!!.Baada ya hapo anaweza kuwageuka wenzake.HAFAI KABISA ANASUMBULIWA NA TAMAA NA NJAA TU.
 
Hii sirikali ya dhaifu ilivyo ya kisanii, it seems mtandao wa hao watesaji washakimbilia ktk forums na kuanza kupotosha au eneza pumba zao ili mradi tu kuvuruga watu akili. I swear to god kwa issue hii, mmejimaliza ! Just just a day after Pindwa kuchapwa maswali juu ya kauli yake wakati akifunga bunge mwaka jana kuwa sirikali yao dhaifu itachunguza na kutoa report juu ya mateso na raia kufa wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola !
 
Mimi hapo penye red ndo panaponifanya nishangae sana juu ya hii skendo. Hata kwenye ile thread nyingine nilijikuta nashindwa kuamini kama serikali imehusika.

Swali langu ni kuwa "Ulimboka alitekwa peke yake, na baada ya kuokotwa alikuwa hana fahamu na hawezi kuongea. Je, haya yaliyomtokea kayasema nani?
Kama umesoma vyema maelezo hayo kabla ya yote alikuwa na Daktari mwenzake, kisha wakamteka pekee, lakini mpaka maelezo hayo yanapatikana, Dk Ulimboka amefanikiwa kuzungumza kwa taabu sana, na hata baadhi ya vyombo vya habari vimeweza kuzungumza naye kama Clouds Tv japo anazungumza kwa taabu sana, lakini maelezo yamesikika.
 
jamani mimi nina swali kichwani mwangu linanisumbua sana.naomba nitangazw kwanza sina upande katika hilim na kwamba walichofanya si sahii kabisa . DR ULIMBOKA POLE SANA
JAMANI NATAKA MNIAMBIE MTOTO WAKO WA KUMZAA ANAUMWA GAFLA AKAPANDISHA DEGEDEGE UMEBATIKA KUFIKA MUHIMBILI KWA SHIDA SANA NAMANISHA SANA MTOTO MACHO YAKO JUU UNAFIKA UNAKOSA UDUMA YA HALAKA KUOKOA MAISHA YA MWANAO MPENDWA ( WALIO NA WATOTO WANANIELEWA ) BAADA YA DAKIKA 16 MTOTO WAKO ANAKUFA .UNAFIKILI MUTU KAMA UYU ANAWAELEWA MADAKTARI WANACHOKIFANYA ? SASA KUNAMTU IMEMTOKEA MTOTO KAFA NA NAKUAMBIA ANGEKUEPO DR KALIBU UYU ANGEMJERUA KAMA SIO KUMUHUA .MAANA YANGU NI MOJA TUFANYE TUSEME ILA KUNA WATU WANAUMIA SANA NA UBABE WA SERIKALI NA MADACTARI . TEMBO WAKIPIGANA NYASI......
JAMANI KILA KITU NA KIASI TUDAI NA KUJITAHIDI KUTAFUTA MUHAFAKA . MSISHABIKIE KWASABABU HAMUHUMWI . KUNA HALI ZINAHITAJI MAHAMUZI YA HARAKA YA DR SI CHINI YA DAKIKA MUTU ANAKUFA . POLE DR ULIMBOKA . ILA TUJUE KWAMBA HAKI JI WAJIBU WETU TUFANYE KWA KIASI ILI NA WANCHI WASIUMIE
 
My GOD! nadhani wanajuta kua kwanini hajafa..Hizi ni dhama za mwisho kwa CCM baada ya kukaa na madaktari wanaamua kuua viongozi...Hivi serikali yetu tena dhaifu haijui kua kuna jumuia za kimataifa na hii inaweza kusababisha mengi kutokea ndani ya muda mfupi and am sure lazima yatatokea tu kwanza Bunge linaendelea...Tumeshuhudia wanaharakati,wabunge wa upinzani wakikatwa mapanga nadhani hakuna marefu yasiokua nancha ingekua ni ZIMBABWE leo BBC,CNN,SYKNEWS na nk na uenda saaivi umoja wa ulaya/US,UK wangekua wameanza kuweka vikwazo vya uchumi na kuwawekea vikwazo viongozi wote wa serikali....my take TOP OFFICIAL WANAJUA NA WALIJUA NINI KINAENDELE MUNGU MKUBWA WAMEUMBUKA NA SASA ITAKULA KWAO....UJANJA WA 1945 HUU HAWAWEZI KUKIMBIA VIVULI VYAO
 
Unaelezeaje uko tayari kufa kwanext gene .. Wakati navyoongea nawewe kuna mtu kafiwa na mtoto wake sabu ya mgomo. Dakika 25 halizokua hosp wangeokoa maisha. Acha kabisa kuingiza siasa kwenye maisha. Mnahaki kudai maslahi yenu lakini kwa hasala ya nani. Mimi napingana na wewe kabisa . Nakubaliana kwamba ni kosa kumpiga dr u. Lakini umeshajiuliza kwamba kunamtu akikusikia unaongea swala kama hili anaweza kukukata na kisu kwa kifo cha mtotot wake mpedwa.
 
ndugu zangu katika ukombozi wa taifa kama Tanzania wengi wametolewa kama sadaka za kuteketezwa!! ndugu zangu tusikate tamaaa ukombozi wa taifa hili unakuja kesho! progress wel Dr
 
wewe kama ni mwanaume ni hasara kwa nchi hii, huna faida! Na kama ni mwanamke, beba ujasiri tuliojaliwa wa kuleta binadamu duniani tuwapo labour, tetea nchi yako! Acha uoga!
cacico, kwa matamshi haya? Umifanya siku yangu kuwa siku muhimu. Thanks for the comments, have no problem I understand you!!!
 
Last edited by a moderator:
Tusiumizane walalahoi kwa walalahoi....wanaosababisha zongwe lote hili ni magamba na serikali yao kwa kufikiria kwamba solution ya matatizo ya watanzania ni nguvu basi...Nampa pole sana Dr-Ulimboka kwa yaliyomsibu Mungu ailinde Roho yake na ashushe nguvu ya uponyaji apone haraka....Aluta Continua
 
Back
Top Bottom