Dr. Mpango, katikati ya simanzi, kuna faraja na tulizo

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,059
Wiki hii imekuwa ya majonzi makubwa, ambapo Watanzania wenzetu zaidi ya 60 huko Hannang wamepoteza maisha, mamia wameumia. Lakini pia wapo walionusurika ambao maisha yao yamevurugwa na majanga.

Mengine ya pembeni ambayo hayakustahili kuwepo, nayo yakajitokeza. Badala ya kushikamana na kuhuzunika na wenzetu hawa, polisi wajatia dosari kwa kuonesha hata maafa yanakuwa mali ya vyama vya siasa.

LAKINI wakati haya yakiendelea kuna roho ziliendelea kuumia kimya kimya kutokana na Makamu wa Rais Dr. Mpango kutoonekana kwa muda mrefu, huku taarifa za kusikitisha na kuogofya zikisambaa, bila ya taarifa rasmi ya kuwatuliza watu. Wengine walisema, yu mgonjwa mahtuti, na wengine walienda mbali zaidi.

Katilati ya simanzi hizi, inakuja faraja. Dr. Mpango ameonekana Kanisani kwenye ibada.

Sijawahi kuwa karibu naye, wala sijawahi kukutana naye ana kwa ana, lakini habari zilizokuwa zikisambaa kuwa huenda yu mgonjwa sana au pengine hayupo katika Ulimwengu huu wa mwili, zilinipa simanzi, sawa na wale walio karibu nami katika maisha ya kila siku. Shukrani nyingi kwa Mungu, yeye atujaliaye uhai na kuweka neema katika mema yote tuyatendayo, na anayesafisha maovu na mapungufu yetu.

Nilipoona picha yake leo akiwa Kanisani, machozi ya furaha yalinitoka. Maana maneno yaliyokuwa yamesambaa yalikuwa yamenivunja sana moyo, na mara kadhaa nilipata simanzi na hasira kwa Serikali kwa nini haijali hisia za watu.

Kama alikuwa anaumwa au alikuwa mwenye afya njema, kama alikuwa nchini au nje ya nchi, kwangu hayo yote si muhimu kwa sasa. Lililo muhimu, Dr. Mpango yu mzima, bado yupo pamoja nasi.

Mungu azidi kumjalia maisha marefu yenye afya njema, furaha na amani moyoni mwake, na zaidi ajaliwe hekima ya kumzuia kujishikamanisha na uovu wowote hasa unaoweza kusababishwa na nafasi yake. Maana kuna wakati madaraka yanakupeleka karibu zaidi na ibilisi.

Kama kweli alikuwa anaumwa, na sasa amepona, kwa hiari yake, na wala hakuna ubaya, akafanya kama alivyofanya Rais mstaafu Kikwete alipotoka kwenye matibabu US. Japo najua itakuwa ngumu kwa mpango, maana kufanya hivyo ataona kama anamdhalilisha PM.

Dr. Mpango, kama mwumini mwenzangu, siyo kama Makamu wa Rais:

Kristo bwana wetu, aliteseka, hata kufa kwaajili yetu. Katikati ya mateso aliwapa msamaha watesi wake. Hakuwa na sababu ya kuteswa na hata kuuawa na wanadamu duni, bali aliyafanya hayo kutuonesha wanadamu tunavyotakiwa kuenenda katika maisha yetu. Mwisho Kristo alimshinda shetani, akayashinda mauti, mauti ya mwili na Roho. Bila kujali yaliyosemwa juu yako, yawe mema au mabaya, samehe na sahau yote, badala yake uombe neema ya kushiriki ushindi wa Kristo.

Dr. Mpango ni miongoni mwa watu ambao ningekuwa na access naye, ningefarijika sana kuonana naye. Lakini kujua tu kuwa yu mzima, ni zawadi kubwa ya kutosha.
 
Lakini pia wapo walionusurika ambao maisha yao yamevurugwa na majanga.
Lakini pia wapo watanzania wengi ambao maisha yao yamevurugwa kabisa na ujambazi na uharamia wa Sabaya na Makonda makalio makubwa ambao kwasasa wanakula bata mitaani.

Kwa dhulma hizi acha mabalaa yaendelee kutupata. Na balaa linalokuja litaondoka na ikulu .
 
Something is wrong. Hata kama kaonekana, ndani kuna fukuto. Haiwezekani Makamu wa Rais aondoke na kurejea kimyakimya licha ya uvumi. Kuonesha kwamba alikuwa nje kweli, taarifa ya kurejea kwake ingetangazwa kama taarifa rasmi
 
Hongera kwa kufurahi Mkuu.

WATANZANIA TUWE TUNAOMBEANA MEMA, CHUKI SIO NZURI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue

Hata tukitofautiana namna gani kisiasa, isifikie mahali pa kuona unayetofautiana naye anastahili kifo au hastahili kuishi. Na hiyo siyo baina ya vyama bali hata ndani ya chama kimoja.

Ndiyo maana, mimi binafsi, hata mtu apige kelele usiku na mchana kunishawishi, kamwe siwezi kuamini mtu yeyote anayeua wenzake ili yeye ayapate madaraka au abakie kwenye madaraka, eti naye ni binadamu. Huyo ni shetani. Anaweza kuwa na mwili kama sisi, lakini ndani yake amebeba roho ya shetani. Unapompa uongozi mtu wa namna hiyo, taasisi nzima inabeba laana ya mtu yule.

Ni sababu hiyo hiyo ndiyo inatufanya tuishangae sana CCM. Kweli miongoni mwa wanachama wote, ilishindikana kumpata hata mtu mmoja wa kupewa uongozi, mpaka kumpa uongpzi mtu ambaye kuna Roho zinamlilia kwa kuzidhulumu maisha ya Duniani?
 
Something is wrong. Hata kama kaonekana, ndani kuna fukuto. Haiwezekani Makamu wa Rais aondoke na kurejea kimyakimya licha ya uvumi. Kuonesha kwamba alikuwa nje kweli, taarifa ya kurejea kwake ingetangazwa kama taarifa rasmi
Siwezi kukupinga.

Kwanza kutokana na ile minong'ono tu, Serikali ilitakiwa kuja na taarifa rasmi isiyo na shaka.

Serikali makini haiwezi kukaa kimya, kuruhusu uvumi usambae. Kwenye leadership and management, inafundishwa wazi kuwa kukitokea crisis, uvumi au janga, kati ya kamati za mwanzo kabisa kuundwa, huwa ni kamati ya habari. Na hii inatakiwa kutoa taarifa za mara kwa mara ili kutotengeneza vacuum ambayo gossiping itaingia kuziba.

Tumefurahi kumwona huyu Ndugu yetu, lakini akiweza vi vema akazungumza na wanahabari. La sivyo, bado minong'ono na uvumi vitaendelea, japo inaweza kuwa ya namna nyingine.

Unakumbuka Kikwete alivyorudi toka US kwenye matibabu, airport palepale alizungumza na wanahabari. Akafafanua sana hali ya afya yake na matibabu aliyoyapitia, tena kwa kiwango zaidi hata ambavyo tulitarajia. Baada ya pale hakukuwa na gossiping tena maana kila mmoja amepata habari kamili kwa mhusika mkuu.
 
Back
Top Bottom