Dkt. Slaa arudishwa kituo cha Polisi Oysterbay kutoka Mbeya. Wakili wake aambiwa akashughulikie dhamana

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,607
93,385
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Jana baada ya ku-file maombi ya kulitaka jeshi la Polisi kuwapeleka Dr. Slaa na wenzake mahakamani ambapo leo tungepangiwa jaji atakayesikiliza maombi yetu na kupewa wito wa mahakama (Summons) ili kuwaita wajibu maombi yetu .

Mimi nilisafiri kurudi Dar kwa ndege na kufika majira ya saa tano usiku.Hivyo kazi ya kufatilia tararibu nilizoeleza hapo juu nilimwachia wakili Jebra Kambore akishiikiana na Chengula na wenzake.

Muda huu nimepigiwa simu na uongozi wa Polisi Oysterbay -Dar es Salaam wakinijulisha kuwa Dr. Willibrod Peter Slaa wamemtoa Mbeya usiku na wako naye kituoni hapo. Hivyo nifike kwa ajili ya kufanya utaratibu wa dhamana yake.

Wakili Dickson Matata
18/8/2023 saa 10:07 Asubuhi

Pia soma
- Dkt. Slaa anadaiwa kusafirishwa Usiku huu (August 14, 2023) kuelekea Mbeya
 
Yuko wapi yule mnafiki Ritz na wajinga wenzie kina faizana ule ushahidi wao wa kutengeneza studio?

Au hawakupeleka ule ushahidi polisi wameishia kuanzisha uzi na kuuacha JF!

Hata hilo kosa lingine la uchochezi nalo ni suala la muda tu, watakubali yaishe.

Adv. Mwabukusi na Mdude nao wanatakiwa kuachiwa huru, kuendelea kuwashikilia wiki nzima bila kuwafikisha mahakamani ni unyama mwingine zaidi ya ule mkataba wa bandari na mwarabu.
 
Siku zote hizi kamatakamata Huwa ni Dili za watu ili kupiga pesa hakuna Cha maana watawafanya Hawa Zaid ya kuzunguka zunguka nao huku wakijilipa pa diem nono OP then wanawaachia.
Pesa za ukamataji washatia mfukokoni.
Ni kikundi tu Cha watu ubuni jambo ili wapige pesa
 
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Jana baada ya ku-file maombi ya kulitaka jeshi la Polisi kuwapeleka Dr. Slaa na wenzake mahakamani ambapo leo tungepangiwa jaji atakayesikiliza maombi yetu na kupewa wito wa mahakama (Summons) ili kuwaita wajibu maombi yetu .

Mimi nilisafiri kurudi Dar kwa ndege na kufika majira ya saa tano usiku.Hivyo kazi ya kufatilia tararibu nilizoeleza hapo juu nilimwachia wakili Jebra Kambore akishiikiana na Chengula na wenzake.

Muda huu nimepigiwa simu na uongozi wa Polisi Oysterbay -Dar es Salaam wakinijulisha kuwa Dr. Willibrod Peter Slaa wamemtoa Mbeya usiku na wako naye kituoni hapo. Hivyo nifike kwa ajili ya kufanya utaratibu wa dhamana yake.

Wakili Dickson Matata
18/8/2023 saa 10:07 Asubuhi

Pia soma
- Dkt. Slaa anadaiwa kusafirishwa Usiku huu (August 14, 2023) kuelekea Mbeya
Polisi ni waongo na leo ni Ijumaa wakili asikubali kudanganywa
 
Siku zote hizi kamatakamata Huwa ni Dili za watu ili kupiga pesa hakuna Cha maana watawafanya Hawa Zaid ya kuzunguka zunguka nao huku wakijilipa pa diem nono OP then wanawaachia.
Pesa za ukamataji washatia mfukokoni.
Ni kikundi tu Cha watu ubuni jambo ili wapige pesa
Dr Slaa hatoki leo waende mahakamani kufile case
 
Back
Top Bottom