A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

Wanaweza wakamuua Dr but hawawezi kuua mawazo yake ya ukombozi kwa wana taharuma ya Udaktari na tasnia ya afya kwa ujumla.Aluta continue, Ata tunisia wanyonge ndio waliotia chachu kuiondoa serikali ya kifedhuli madarakani, sitegemei mwana ccm au mafisadi waunge mkono jitihada hizi za ukombozi but ni wale tu wanaopata shida na kuathirika na wizi huu na uonevu.
 
"Ndugu zangu,
Najaribu kutuliza mawazo ili angalau niweze kuwapa kidogo tulipofikia na tunakoelekea juu ya suala hili. Kwa kweli haivumiliki ukimwona ulimboka kwa jinsi alivyotendewa na hali aliyonayo; kwa wale wanaojua hali za kitabibu, "this is a very unstable condition that demands permanent watch 24/7".
Kwa taarifa tulizokusanya, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani) na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu". Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi.

Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...

Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili.

Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'. Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na RedioCall, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.

Nashindwa kuendelea....."
NB: Haya ni maelezo ya mwanaharakati Albanie Marcossy aliyehusika kumsaka kama nilivyoyanukuu Mabadiliko Forums.
Mkuu ahsante kwa taarifa hivi yamekuwa hayo, wakimuuwa Dr Ulimboka watapata faida gani au wanataka kuwatisha madaktari??? Ndugu zake wawafungulie mashitaka hao waliofanya unyama huo, kuanzia huyo ofisa na watu aliowatumia!!! Hii serikali imechoka kukaa madarakani wamekuwa wauuwaji mara Igunga, Arusha mjini, Arumeru, sasa Dar kwa daktari!!!

Maskini Tanzania yangu jamani, tumefika hapa. uuuuuuuuuuuuuuuwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mkuu wa emergency dept anazuia gari kwenda kumchukua Daktari mwenzake aliyeokotwa akiwa hajitambui?
Aisee ndiyo maana migomo yenu haifanikiwi wakuu...
 
"
Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...
Haya maneno kayasema ulimboka mwenyewe au?
 
If they wanted him DEAD, he'd be dead by now, na mngekuwa mnaongea mambo mengine kabisa.......probably, they still need him for something..........the big question is wat is it??

and kimtazamo wangu, 1st, wat has bin done to him isnt fair, Unless, he(ulimboka) framed it....najua kwa hili, wengi mtanilaumu, but mkisoma stories nyingi kama hizi, mtaona, ulimboka hatokuwa wa kwanza, kufake something like this, but FOR GOOD REASONS..............cause, seriously, kama wangetaka afe, angekufa longtym........

2dnly, killing one person for the benefit of two or more people, i find it reasonable................
 
ilikuwa ni kulazimishwa kifo kisichopangwa na MUNGU,na MUNGU amsimamie aweze ku recover na kupona ili uma upatekujua kiundani kilichomsibu mpaka kufikia hatua ya kuuwawa na hao manyang'au
 
Mbaya sana hii, na ni kuongeza chumvi kwenye kidonda. Alijisema Shaf Adam Shafi kuwa YANAMWISHO
 
Ikiwa serikali ya Kikwete imehusika au haikuhusika ,basi Raisi Jakaya hana budi kujiuzulu kiungwana kabisa . Raisi awe Muungwana ajiuzulu bila ya tatizo lolote.Na hili litapokewa kwa ukunjufu kabisa.Ili kupisha uchunguzi
 
Wapiganaji popote pale mlipo,

kwa misingi ya mwitiko kwa
vitisho vilivyotolewa na baadhi ya maafisa waandamizi wa serikali kwa Dr Ulimboka na kutokea vile vile walivyowahi kutamka, huyu kiongozi mahiri wa masuala ya utibabu nchini huenda tusiwe naye ndani ya siku chache zijazo endapo 'Wale Madaktari Wenyewe Wale' watakua wamemsogelea hapo kitandani mwake kwa sura ya aina yoyote ile.

Na huo ndio udhaifu wa roho zilizojaa chuki, hila na visasi vitakavyoonelea kuwa ni vema na tena inafaa. Maombi ni kwa Mungu Baba Mwenyezi juu mbinguni toka kwa kila Mtanzania tangu dakika hii hapa.

Na enyi Madaktari na watumishi wengine wa tiba nchini; kutawanyika kwenu kutakua na machozi ya DAMU YA DOKTA ULIMBOKA bila chenga.

Lakini endapo Dr Ulimboka ataaga dunia, wala sitoshngaa makubwa zaidi yakitusalimu mitaani baada ya madhila haya yote.
 
If they wanted him DEAD, he'd be dead by now, na mngekuwa mnaongea mambo mengine kabisa.......probably, they still need him for something..........the big question is wat is it??

and kimtazamo wangu, 1st, wat has bin done to him isnt fair, Unless, he(ulimboka) framed it....najua kwa hili, wengi mtanilaumu, but mkisoma stories nyingi kama hizi, mtaona, ulimboka hatokuwa wa kwanza, kufake something like this, but FOR GOOD REASONS..............cause, seriously, kama wangetaka afe, angekufa longtym........

2dnly, killing one person for the benefit of two or more people, i find it reasonable................

Are u naive or plain stupid ? to fake so as to gain what ? for all those injuries sustained ?
 
Back
Top Bottom