30 - 36 years old: An Official Thread

Hizo connection tupeane sote mkuu

Neema za inchi usizifaidi peke yako
 
Watt mboga saba unaona umeyapatia maisha
 
Ondoa tuu hizo chuki kwa bimkubwa inawezekana asingekuonyesha hio hali usingekuwepo hapo ulipo,mama ni mama
 
Watt mboga saba unaona umeyapatia maisha
Nipo katika umri huo bado napambana, sijatoboa bado.( Huko nyumbani nimeacha buku tatu tu mpaka jioni wife ndo anajua atavoipangilia.

Ila nimeamua kuwekeza sana mbiguni
Maana sikuhizi tunakufa mapema tena vijana na angali na ndoto zetu.

Kupanga Ni kuchagua yani nikose kokote mkuu.
 
Okay mkuu nimekuelewa,ila sorry kwa comment yako iliyopita kudhani ndivyo sivyo
 
Just 4give her man, umeshafanikiwa,
 
Ondoa tuu hizo chuki kwa bimkubwa inawezekana asingekuonyesha hio hali usingekuwepo hapo ulipo,mama ni mama
Dingi ni dingi,yaani dingi ndiyo full kujali na kunipa moyo mwanaume mwenzie,nikiona upumbavu wa sijui Nani Kama mama,natukana kinoma moyoni yaani,wanawake wengi wangese Sana yaani!!..honestly simpendi,ndiyo maana sijampa binti yoyote jina lake na sitompa
 
Nimefanikiwa kumjengea nyumba Mama yangu daresalaam japo haijaisha(finishing) ,nimejenga yangu Bado finishing japo naishi hvyo hvyo,..nna kiwanja 45×90 nimepiga msingi wa vyumba vitatu na kutengeneza shimo la choo..nna mbuzi watano,.pikipik boksa moja,laptop,mke na watoto nane..Mama tofaut tofaut..

Mungu akijalia 2025 nataka nivute nding kwa ajili ya kulia maisha...
,.pia natamani Sana niwe na biashara zangu..binafsii...

Kipaji changu Ni uchoraji..na muziki...
 
Huu Uzi utapelekea vijana kupata depression na pressure kwa vitu ambavyo kiuhalisia havipo kabisa........

Vitu vya msingi kwenye maisha ni uhai na afya njema mengine yanayofuata baada ya hivyo ni juhudi zako na kudra za mwenyezi kama unamuamini..........

Usiendeshe maisha yako kwa kutumia maoni na mitazamo ya watu wengine bali kwa muongozo wa akili yako na mazingira yako........

Maisha ni safari ndefu na hakuna ajuaye kesho yake.......

Wapo waliokuwa matajiri Sasa hivi ni masikini na wapo waliokuwa masikini Sasa hivi ni matajiri..................

Kwenye uso wa Dunia mwenye hasara ni mtu asiyekuwa na uhai kwani penye uhai Pana tumaaini............


Vijana pigeni kazi kwa bidii bila kuangalia umri kwani umri ni namba tu.........jitunze, jijali, jithamini, jipende....furahia maisha yako.........
 
Waoooooooooooooòooooh

Man u have a gift.
 
Ushauri wangu kwa vijana na wale tunaolingana umri (personally hapa ndo natumikia mwaka wangu wa 36) ni kuacha mambo yawe kama yalivyo,mimi hapo vimepungua vitu viwili kama siyo vitatu cheo sina nipo nje ya ajira,gari sina sina hobby kununua vitu visivyoingiza kipato na sitegemei kuwa na cheo na vyote nilivyo navyo leo hakuna siku nilikaa nikapanga niwe navyo.

Muhimu ni kuwa makini na kipato chako,obviously kila kitu ni pesa (hii ni kwa wanaume wenzangu) kitu kinachoitwa pesa hakina cha nitapata nyengine kesho uliyoipata leo ifanye itoshe kufanya kitu kitakachokusaidia kesho,heshimu watu maana watu ndo asset zenyewe wewe binafsi jiheshimu usiwe mtu wa kuropoka ropoka hovyo kama wewe dada vaa smart nguo za heshima usijichore tattoos social networks share vitu vya maana siyo picha ulizopiga umebinua makalio kwa juu na punguza uanaharakati maisha yako yataji-set vizuri tu utakutana na watu sahihi type yako mume partner etc.

Africa na maisha yetu haya ya kuunga unga hayupo bado anayeweza kuji-limit kwamba at 40s niwe tofauti na nilivyo sasa zaidi utajitia mawazo kijana mdogo uzeeke bure upo 31 kichwa kijae mvi.
 
😅😂 Vijana acheni kupotoshana, Nani aliyekuambia ukifika huo umri lazima uwe na ndoa, una gari na nyumba na umepanda cheo 😅..? Ndio maana vijana wengi mnajiingiza ktk ushoga ili mpate maisha mserereko...
Ni hivi ktk umri jambo kubwa na la muhimu kwanza linda afya yako don't take risk ktk afya, hakikisha uwe na shughuri yoyote halali inakuingizia kipato, pia hakikisha unawekeza pesa zako kama unapata 5,000 kwasiku basi 2,500 iwekeze sehem kwa ajili ya maendeleo yako... The rest muachie Mungu maana anaona jitihada zako.
 
Maisha ya mwanadamu hayana formula.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…