20m itanifikisha wapi katika ujenzi wakuu?

20m itanifikisha wapi katika ujenzi wakuu?

20M ya kujengea? Wtf! Una haraka gani sasa? Kama umeweza kuipata hiyo pesa yote unangoja nini hadi zifike 30M+ ili ukianza ujenge nyumba ya maana na uikamilishe kwa wakati.
Mill 30 hauwez jenga nyumba ya maana .

Nyumba nzur ni Mill 80 hiv.
 
Yaan Mill 17 aanze msing alaf afike hadi bati?.

Bati zuri kwa nyumba ya wastani.
Nyumba vya vyumba vitatu.
Yenye mita 10 kwa 13.
Mbao , bati na ufund ni kati ya mill 10-15.

Sio kweli mkuu kwa dimensions hizo ulizotaja; ukitaka tupige hesabu kwa uhalisia tunaweza fanya hivyo. Pia hakuna nyumba ya vyumba vitatu yenye dimensions hizo za 10×13 M². Hiyo ni ghala/godown unaisemea hapo. 😊
 
FB_IMG_1785223942793.jpg
 
Habari marafiki.
Mkononi nina kama 20m hivi,kuna kakiwanja kama ka 25×20 nimekapata morogoro road eneo linaitwa madafu kwa 3m,so mkononi nitabakiwa na 17m.je wakuu naweza kweli kujenga nyumba ya walau room 3 ikafika usawa wa lenta au niendelee kusubiri kwanza?
Kwa nini ujenge nyumba ambayo hatautaimaliza? Punguza ukubwa wa nyumba ili ujenge ambayo utaimalizia
Kwa uzoefu wangu kama kujenga Boma tu unatumiwa 17m basi jua total cost ya nyumba yako ni around mil 70
 
Basi asikilizie hadi ikishafikia hiyo hela 80M kuliko kujenga upuuzi kama huo anaotaka
Nyumba inajengwa kwa miaka had mitano.

Kwa vipato vyetu vya kuunga unva ukiwa na mentality ya kusema had uwe na mill 100 ndio ununue kiwanja alaf uanze kujenga chap chap.
Niamin unaweza usijenge.
Maana matatizo yapo na saving inaweza ikavurugika.

Ila ukigawa hii project ya kujenga kwa phase.
Yaan ndan ya miaka 5-7 una nyumba yako nzur tu.

Mwaka 1 - Unanunua kiwanja.
Mwaka 2 - Unajenga msingi na unaanza kupandisha boma.
Mwaka 3 - unamalizia kupandisha na Unapaua.
Mwaka 4 - Unafanya wiring na kupiga plasta, kuvuta umeme.
Mwaka 5 - finishing mdogo mdogo.
Mwaka 6 - Unamalizia finishing, unazungusha ukuta.
Mwaka 7 - unamalizia ukuta, gate na paving.

Nimepitia the same process.
Nilianza nikiwa na 27 yrs Na nilivyofika 33 yrs nikawa na nyumba nzur tu na project ikakamilika.
kama 90+ Mill zimeteketea.
 
Inafika mpk kwenye lenta bila shida kama utasimamia mwenyewe namanisha macho macho hapo sw. Usijenge kwa simu kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Sio kweli mkuu kwa dimensions hizo ulizotaja; ukitaka tupige hesabu kwa uhalisia tunaweza fanya hivyo. Pia hakuna nyumba ya vyumba vitatu yenye dimensions hizo za 10×13 M². Hiyo ni ghala/godown unaisemea hapo. 😊
Kwan nyumba standard inakuwa na mita ngap kwa ngap?.
Upana vs urefu.

Mm yangu iko hivyo. Sikutaka kujibana.
Vyumba vitatu vikubwa vyote master.
Master bedroom kubwa kama sebule hizi za kawaida 😊😊😊😊
 
Kwan nyumba standard inakuwa na mita ngap kwa ngap?.
Upana vs urefu.

Mm yangu iko hivyo. Sikutaka kujibana.
Vyumba vitatu vikubwa vyote master.
Master bedroom kubwa kama sebule hizi za kawaida 😊😊😊😊

Basi hivyo vipimo ni feet mkuu sio mita.
 
Sio kweli mkuu kwa dimensions hizo ulizotaja; ukitaka tupige hesabu kwa uhalisia tunaweza fanya hivyo. Pia hakuna nyumba ya vyumba vitatu yenye dimensions hizo za 10×13 M². Hiyo ni ghala/godown unaisemea hapo. 😊
Upana mita 10
Na urefu mita 13.

Ww umepiga mita square. Wakat mm nimepima urefu na upana.
 
Habari marafiki.
Mkononi nina kama 20m hivi,kuna kakiwanja kama ka 25×20 nimekapata morogoro road eneo linaitwa madafu kwa 3m,so mkononi nitabakiwa na 17m.je wakuu naweza kweli kujenga nyumba ya walau room 3 ikafika usawa wa lenta au niendelee kusubiri kwanza?
17m unatafuta ushauri? Wewe kaanze ujenzi hata ukiishia msingi ni mwanzo mzuri.
 
Kama hauna familia kwanini usijenge chumba na sebule ukahamia kwanza? Kwa uzoefu wangu nyumba vyumba vitatu vya kulala+ choo na sebule , kupaua tu lazima ulaze sio chini ya mil 6 kwa bati za kawaida.
Maana yake ukikaza saana iyo 17 mil unaweza pandisha boma na kupaua tu.
 
M17 unahamia kibishi endapo nyumba haitakuwa na mbwembwe nyingi pia bati ukichukua za kichina sio Alaf na pia usimamizi ukiwa madhubuti

Utaweza kupaua na kuhamia huku ukiweka madirisha na milango ya khanga na vitenge
 
Ni ngumu sana kwa maisha aya

Back
Top Bottom