Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
Mkuu Tujitegemee
Huko nyuma tumeeleza kwa uchache jinsi Da'Amina alivyopenya hadi 3 .
Hilo ni moja ya tatizo linalotukabili nchini. Hatuchagui viongozi kwa merits, bali kuongozwa na eneo au jinsia.
CCM wanaongozwa na hofu ya kukutana na KANU na UNIP kama watu wataamua kubadilika.
Karata inayochezwa ni jinsia
Mkuu, kuelimika ni zaidi ya vyeti mtu anavyopata. Hatunad hamira ya ku criticize elimu yake, tunachosema ni kuwa elimu ni pamoja naweledi na exposure
Inaonekana Da, amepata nafasi nyingi za kumwezesha kuwa na weledi na exposure.
Swali, je alitumia fursa hizo kupata maarifa zaidi?
Nafasi aliyokuwa anawania inahitaji weledi, hatudhani yeye kama yeye alikuwa tayari kwa ‘prime time'.
Kilichotokea aliandikiwa hotuba na washauri wake kwa lengo la kupata nafasi.
Ndio maana alimshirikisha Edo bila kutambua alikuwa anatia nyongo katika kitumbua.
Hakujua kuwa hadi wakati ule kambi ya Edo ilikuwa namaruwe ruwe 'Delirium'
Waliomwandikia hatujui uelewa wao katika mambo ya siasa.
Siasa za siku hizi ni za kisayansi si za kukota wapiga debe.
Nadhani washauri wake walikuwa dhaifu, ukichanganya na udhaifu wake, unaishia kupata suala la middle class kuelekea first world
Ilikuwa ni rahisi kubaini. Wiki iliyopita UN imetangaza nchi zilizoingia uchumi wa kati.
Jirani zetu kenya walikuwa kundi moja vi nchi masikini sana. Hatujui kama alioma habari hizo
Tuna tatizo, sasa huyo ndiye alikuwa awe mgombea!
Kuna baadhi ya watu wakupata wadhifa wanautumia kutanua. Lakini kuna watu wanautumia zaidi ya matanuzi. DaAmina alikaa kwenye kiti cha kuzunguka, alikuwa anazunguka kwa hiyo siwezi kumlaumu. kama kweli yeye na Dr Migoro wangekuwa rais ingekuwa hatari sana kwa nchi.
If the two had realistic chances, naweza kusema ni hatari sana. Lakini kama walikwekwa as symbol of unity, symbol of solidarity, symbol of proving that they got close to top job, lakini Pombe alikuwa ameandaliwa, si jambo baya. Lakini ukiangalia upigaji kura unaweza kuona kuwa kura za watu kutoka visiwani zote zilienda kwa da Amina.