2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

Mkuu Nguruvi3,
Tafadhali mpuuze huyo jamaa labda kama hakufuatlii vizuri msimamo wako na mabandiko yako, kimsingi ww ni mtetezi wa maslahi ya taifa na huwa unakosoa chama tawala au upinzani popote unapoona pana mapungu, so asiku discourage kwa namna yyt, tumeshuhudia mabandiko mengi wewe na wenzako mkikosoa na kupongeza pasipo kupebdelea.

kimsingi wengine tumejifunza mengi so wanaokukebehj hawajui thamani yako wapuuze kabisa, kinachotokea ninupande wanaoshabikia una mapungufu mengi ndio maana wanadhani ww ni mshabiki fulani kumbe ni mkosoaji huru

wewe na wewe ni mhanga, jifariji tu!

tumetoka mbali na nguruvi, ndio maana kawa mpole.........

sikujiunga JF baada ya uchaguzi wa 2010!
 
Una roho mgumu kama ya Lowassa! ona aibu mkuu

post za emotion na ubishi bila kutumia akili zipo na unazifahamu!

kwa kifupi akina Mbowe wamewavua nguo, wamejitofautisha wao ni akina nani

yaani juzi ndio umejua Mbowe ni opportunist? how many times mliishaambiwa??

sema yote, jifiche kwenye kivuli cha uzalendo na maslahi ya nchi hii.......ila haukuwa fair hata kidogo

hii ni aibu na mtu mzima anachutama chini kwanza!!

kisiasa narudia tena, alichofanya mbowe ni 100% correct!!! ila the same mbowe huwa anacheza dirty politics kwa watu wazuri na wasafi kama zitto na kucheza dirty politics ambazo huwa mnazikubali!!

Mbowe is a nigga! level zake ziko juu mno

ila lwa wwenye akili kama wewe maipaswa kujua!!

Is your thread ACT mpini wa kumaliza upinzani...is it still valid?? kabadili title

nadhani kwa sasa tunaweza kuwa in the same ground, tukajadili kwa afya na amani tele

kubali tu sometimes you were wrong thinking these guys are saints!
Mkuu Waberoya

1. Unaweza kujadili hoja bila kutukana. Kutukana hutokea pale ambapo kuna ombwe la hoja.
Nadhani unafahamu kwanini jukwaa lilianzishwa. Kama unaona pana ugumu wa kujenga hoja bila kutukana,hamia kule

2. Midhali upo hapa unachangia na kusoma kwa bidii, hoja zilizopo zina akili. Vinginevyo, unawezaje kuhangaika na eneo lisilo na akili la wapumbavu. Nadhani ujiangalie kama kweli unatumia akili kusoma vitu visivyo na akili

3. Tumekuuliza uweke ushahidi wa chuki dhidi ya jamaa yako Zitto. Hujaweka! hivyo, maneno yako hayana uzito au mashiko

4. Tuweke kumbu kumbu sawa. Kwamba Zitto litenda mabaya, hilo halina ubishi. Atasimama ima kutetea au kuhukumiwa nalo. Wala hakuna hoja itakayondoa ukweli wa uzi huu

5. Yes ACT ni mpini wa kumaliza upinzani. Hoja ipo valid kwasababu ACT ya Cheyo inahukumiwa kama ACT si UDP

6. Tumesimama katika utaifa, hilo tumelisema na tunalisema. Hatutakubali siasa majitaka kama za ACT

7. Tumesimama kama taifa na umma umetuelewa.
Muulize 'mzee' kama anakanyaga Tanzania kama ilivyokuwa. Na hatutasimama, tutaendelea bila kumuonea mtu au kumhurumia

8. Unakumbuka kauli yangu kwako kila mara ?

Ukweli unatuweka huru ndio maana tunasimama bila na kusema hili tunalikubali hili hapana.

Kama tunavyomueleza Zitto na siasa zake za chuki dhidi ya kanda na makabila, vivyo hivyo tutaeleza mwingine na wengine kwa yale watakayotenda

Hapendwi mtu inapendwa hoja
 
wewe na wewe ni mhanga, jifariji tu!

tumetoka mbali na nguruvi, ndio maana kawa mpole.........

sikujiunga JF baada ya uchaguzi wa 2010!
Nipo hapa nafanya kazi na maisha mengine kwavile mkate wetu hautegemei kubeba viatu vya mtu. Wala usitaraji kutoweka

Nimesimama kutetea kile ninachokiona ni kweli kwa mujibu wangu. Tunaandika bila woga wala hofu. Hatuandikii chooni

Tunathubutu mchana kweupe, hatuandiki waraka tunajenga hoja

Mkuu hasira zako hazisadii maana mwisho wa siku kinachochambuliwa ni hoja.

Mjadala unaendelea
 
Nguruvi analia when is too late!! Mbowe ni opportunist na in politics ni sawa kabisa. Kuweka matumaini yako na moyo wako kwa watu wa aina ya mbowe ndio huwa wana waaibisha,

usafi?? sio kweli kuwa akina mbowe ni wasafi, mbona lilipigiwa sana kelele na nguruvi, mag3 na yule mchambuzi walikuwa watetezi wa kwanza?/

wala haijapita miaka mingi mnaanza kulia usaliti wa mbowe na slaa?? hivi hamna akili?/ akina Nguruvi na mag3???

kwa siasa hizo hizo mbowe alifanikiwa kuwaaminisha zitto ni msaliti ( nadhani mlisema usiku na mchana hata kulala hamkulala) na mpaka mkaanzisha thread nyingi mno....na kusema sana Lowassa ndie anaifadhili ACT!! kiko wapi??

Nguruvi, i thought angekaa kimya sana na sio kulialia kitoto when all was so clear kuhusu tabia ya mbowe

kisiasa hii move ya mbowe iko sahihi kabisa, siku nyingine mkome kuamini wanasiasa kiasi hicho, muwe mnatumia akili zenu, kama mngekuwa wasichana mmeishapewa mimba!! kueni sasa

Una roho mgumu kama ya Lowassa! ona aibu mkuu

post za emotion na ubishi bila kutumia akili zipo na unazifahamu!

kwa kifupi akina Mbowe wamewavua nguo, wamejitofautisha wao ni akina nani

yaani juzi ndio umejua Mbowe ni opportunist? how many times mliishaambiwa??

sema yote, jifiche kwenye kivuli cha uzalendo na maslahi ya nchi hii.......ila haukuwa fair hata kidogo

hii ni aibu na mtu mzima anachutama chini kwanza!!

kisiasa narudia tena, alichofanya mbowe ni 100% correct!!! ila the same mbowe huwa anacheza dirty politics kwa watu wazuri na wasafi kama zitto na kucheza dirty politics ambazo huwa mnazikubali!!

Mbowe is a nigga! level zake ziko juu mno

ila lwa wwenye akili kama wewe maipaswa kujua!!

Is your thread ACT mpini wa kumaliza upinzani...is it still valid?? kabadili title

nadhani kwa sasa tunaweza kuwa in the same ground, tukajadili kwa afya na amani tele

kubali tu sometimes you were wrong thinking these guys are saints!

Wakishindwa hoja uleta viloja....
 
hii habari ENL inaniumiza sana nafsi yangu.. mungu tusaidie waja wako.. fanya moyo wa farao uwe mgumu..

Habari hizi hazikuumizi wewe tu bali ni watanzania wote, tuliokuwa na imani na Chadema/Ukawa, tuliokuwa na imani na viongozi wetu, tuliopata majeraha kwa ajili ya Chadema/Ukawa, tuliokuwa mstari wa mbele kuelemisha wananchi jinsi ufisadi unavyowaadhiri wao na familia zao na nk.

Leo hii hawa viongozi tuliowaamini kuwa viongozi wetu wanajifungia chumbani na kuja na maamuzi ya kipumbavu namna hii. Hawezekeni viongozi wasiozidi 20 wajifungie ndani na kutuchagulia mgombea urais, hii haki hawana na hawatawahi kuwa nayo. Na kama wakingángánia na msimamo wao, ambao kipaumbele kwao ni matumbo yao basi huyu Lowassa wakamchague wenyewe..

Pendekezo langu ni kuwa watuache wananchama tuchangue ni nani tungependa hawe mgombea wetu.. Huitishwe uchaguzi kila kanda/ au hata baadhi ya mikoa ili wanachama wapinge kura ya ni nani kwa mtazamo wao wanaona anafaa kupeperusha bendera ya Ukawa. Kinyume cha hapo ni "usaka tonge tu hakuna lolote"n Maana haiwezekani miaka yote viongozi wetu wamnage kuwa Lowassa ni fisadi halafu leo hii ndo awe lulu ya kupeperusha bendera ya chama.

Kama ni tamaa ya pesa/madaraka hii ni too much. John Mnyika , Dr.W.Slaa na wengineo oneni aibu..
 
Last edited by a moderator:
UKAWA wamevunja mioyo ya watanzania wengi sana hasa wahafidhina wa Chadema ambao ndugu zao na wao walipigwa kwa ajili ya chama.
Kwanin wasijiamini wamsimamishe mgombea wao? Ina maana Dr. Slaa haaminiki kuwaongoza watanzania?
Nadhani huu ni mpango wa CCM kuihujumu Ukawa, umesukwa toka siku nyingi sana. Ni kwamba Lowassa akatwe CCM aje kugombea Ukawa.
Uchaguzi wa mwaka huu ni kama tumewekea wagombea wawili wa CCM katika rangi mbili tofauti. Lowassa akikosa urais watamlaumu? Watajilaumu? Watamlaumu nani hasa?
Akikosa ina maana Ukawa watakuja na wimbo gani kurudisha imani za wananchi zilizokufa?
Lowassa akipata atasimamia maslahi ya nani? Kwanza anajua kwanza kile Ukawa wanataka?
 
Kura za huruma za Lowassa wanazozitegemea hawatapata zote na wakakosa kura za wana ukawa walizokuwa na uhakika nazo. Mwisho wa siku watajikuta walichokuwa wanategemea hawakipati. Kwasababu waliokuwa wanataka kumchagua Lowassa ni walewale wanazi wa CCM na sio wanazi wa Lowassa. Kinachaguliwa chama na sio mtu, Lowassa ameacha kura nyingi sana CCM.
 
Ni aibu unawezaje kumchangua mgombea urais mtu aliyejiunga/atakayejiunga ndani ya wiki 1? kama ACT wangefanya hivyo niwaelewa maana ni chama kichanga. Lakini si Chadema si Nccr si Cuf wala si NLD hivi vyama ni vyama vikongwe vina wagombea walioiva, vimejengwa usiku na mchana, mvua na jua leo hii unachukua kapi kutoka CCM na kulipa ugombea urais? Inamaana wakati mnajigenga hamkufahamu kuwa baada ya miaka 5 kuna uchanguzi hivyo ni muhimu kuandaa watu kama 3 au zaidi kwa ajili hiyo?

Ni aibu ni fedheha na ni masikitiko. Ila kura yangu, familia yangu na majirani zangu kamwe hazitakwenda kwa Lowassa.
 
Hivi ni vipengele vya katiba ya CHADEMA:
7.7.8
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu Taifa watakuwa wafuatao:
-
(a)
Wajumbe wote wa Kamati Kuu
(b)
Wajumbe wote wa Baraza Kuu
(c)
Wenye viti wa Wilaya/Majimbo
(d)
Makatibu wote wa Majimbo/Wilaya
(e)
Wajumbe ishirini watakaochaguliwa na Mikutano Mikuu ya kila
Baraza la cham
a kuingia kwenye Mkutano Mkuu Taifa kwa
uwiano wa:
-
(i)
Wajumbe kumi na tano kutoka Tanzania Bara
(ii)
Wajumbe wa tano kutoka Tanzania Zanzibar kwa kila
baraza
(f)
Mjumbe Mwakilishi wa kila Wilaya
7.7.9
Mkutano Mkuu Taifa utakutana mara moja katika
kipindi cha miaka
mitano. Mikutano Mikuu maalum / dharura inaweza kuitishwa wakati
wowote ukiwepo ulazima kwa utaratibu utakaowekwa na Kanuni.
7.7.10
Kazi za Mkutano Mkuu wa Taifa ni:
-
(a)
Kuchagua Mwenyekiti wa Chama Taifa na Makamu wake wawili
(b)
Kuja
dili taarifa za Baraza Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo
kwa utekelezaji.
(c)
Kuteua mgombea wa Uraisi na mgombea wenza wake kwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea Urais wa
Zanzibar.

(d)
Kujadili na kuridhia Itikadi, falsafa na sera za Chama kisha
kuweka mikakati na miongozo ya utekelezaji.
(e)
Kujadili na kuridhia programu ya Chama kwa kuzingatia
mapendekezo ya Baraza Kuu.
(f)
Kuzingatia na kutoa maamuzi juu ya rufaa na masuala ya
kinidhamu yanayowakilishwa na Baraza kuu.
(g)
Kupokea na kujadili t
aarifa ya Bodi ya wadhamini wa..

Viongozi wa Chadema tunaomba mtwambie ni lini mkutano mkuu umemchangua Lowassa kuwa mgombe urais??
 
Sehemu ya I

SIASA ZA JAMII NA SIASA ZA NCHI YETU

Kuna somo la political science au ni sehemu za siasa zajamii ambalo ni pana sana lisiloweza kujadilika kwa kurasa chache.

Ni somo linalohusu uchambuzi(analysis) likihusisha tabia na mwenendo wa siasa kuhusiana tawala na migawanyo na yanayotokana na, iwe kiuchumi, kisiasa na kijamii na kisiasa

Political science inaangalia mwenendo na tabia za wanadamu katika mambo yanayohusiana na siasa katika serikali au taasisi ,wakiangalia, kuchambua kutengeneza na kutathmini matukio au sera

Wanataaluma, sayansi ya jamii husoma tabia na mwenendo wa wananchi na huongoza mijadala ya eneo, taasisi au nchi.

Ieleweke, wao huongoza baada ya kutathmini na kuchambua hoja za wananchi na siyo wao wanaopandilkiza hoja.

Mifano, Uingereza inapojadili ushiriki wake EU, hilo ni zao la hoja za wananchi ambalo hufanyiwa kazi na wanasiasa ili kupata ridhaa ya kutawala na kuongoza.

Kama mtakumbuka, kuna nyakati Rais Nyerere alikuwa anatoa kauli tofauti na mtarajio ya wengi.
Mfano, wakati uchumi ukiselelea, Nyerere alisimama na kukemea mfumo wa rushwa uliopo serikalini.

Hakuongelea mfumuko wa bei wala umasikini wa watu wakati huo.

Nyerere kama mwanasiasa mzoefu alifahamu sayansi ya jamii , tatizo la nchi ni rushwa

Nchi fulani ikiwa na agenda ya ufisadi,ndilo tatizo linalowakera wananchi.

Leo Ujerumani haiwezi kuongelea rushwa wala uchumi isipokuwa itaongelea uchumi katika mukatadha wa EU

Na hilo ndilo linasukuma wanasiasa kuiangalia EU kwa vile kero ya wananchi ni uchumi wao dhidi ya matatizo ya EU

Hoja hupatikana baada ya wanataaluma kuzifanyia kazi na kuelewa nini kilichopo katika jamii

Wanaofanyia kazi hoja hizo si wanasiasa au wataalamu wote.

Kwa kawaida kuna timu ya watu ikishirikiana na wataalmu wengine inayokaa na kutoa majibu(Think tank).

Kundi hili hushirikiana na mengine ya wana saikolojia, takwimu, population, wachumi na wanataaluma kutathmini nini kinaendelea katika jamii, na ni nini majibu yake

Inatosha kusema, siasa si kusimama majukwaani, ni taaluma iliyopo kisayansi inayofanya kazi kwa kutegemea taaluma nyingine na mifumo husika katika kuwapa wanasiasa ridhaa ya kuongoza.

Hili ni somo pana sana lisiloweza kujadiliwa kwa ukamilifu na utimilifu katika muda mfupi.
Tunatumiani hoja zitakazojengwa zitaagalia kwa uchache hayo yaliyotajwa kwa uchache sana

TANZANIA

Kwa nchi yetu, tatizo la wananchi ni mfumo na si watu, mfumo uliojengwa ambao wananchi hawana kauli ‘say' .
Taasisi zote zimeundwa ili kutetea mfumo huo badala ya masilahi mapana ya wananchi

Mfumo hauwezi kuwepo bila watu wa kuutetea. Na wala hauwezi kuondoka watu wanaoulinda wakiwepo

Tatizo letu ni mfumo uliotengeneza watu wanaoutumikia,wasioweza kuacha uporomoke kwasababu wanaoutegemea

Kipaumbele cha Watanzania baada ya miaka mingi ya utawala wa CCM ni kubomoa mfumo ili kujenga mazingira mapya ya mfumo manufaa. Suala si kubadili wamiliki wa mfumo, bali kuwaondoa, waje wengine nje ya mfumo wafanye mabadiliko

Kwa kuangalia tabia na mwenendo wa jamii, nchi ipo katika wakati mgumu wa uovu wa ufujaji, ufisadi, wizi n.k.
Maovu yanatendwa na kusimamiwa na watu

Mwenendo wa jamii unaonyesha wazi Ufisadi ndilo tatizo linalozaa matatizo mengine

Hivyo, Ufisadi ndiye adui namba moja wa wananchi

Inaendelea...
 
Sehemu ya II

WAPINZANI NA AGENDA YA UFISADI

Kwa kuzingatia tuliyosema, wapinzani walijipambanua katika kupiga vita ufisadi. Hilo liliwapa nguvu kama agenda ya wananchi

Wapinzani wamejipambanua nalo na limewap ' political milage' katika kukabiliana na CCM
Mwelekeo ulikuwa wazi CCM kuondoka madarakani, au udhibiti wa mhimili kama bunge kupotea

Katika uzi huu, tumewaeleza wapinzani mambo mawili.

Ima wakazane kuchukua dola(Plan A1) na Bunge(Plan A2)
Uwezekano huo ulikuwepo, na CCM walisaidia sana uwepo wake

CCM WALIONA TATIZO
Kwa kutambua agenda umma, CCM iliwatosa makada wake nguli. Kishindo cha kushindwa kwa EL kinaeleza kila jambo.

Tukiri kuwa wanasayansi jamii wa CCM waliliona hilo , wakalifanyia kazi.

Ilikuwa ni kwa gharama kubwa kwa kutambua chama kitapoteza sana katika uchaguzi.

Hata hivyo, hiyo ilikuwa hatua mahususi kujibu hoja za wananchi

CCM wanatambua, mfumo uliopo unawatambua watu wake na kuwahudumia.

Hawakuona tatizo kwa mtu bali kwa wananchi. Walitambua, watuhumiwa wa ufisadi walitumia fedha nyingi ili ‘kununua' wapiga kura katika maamuzi vikao vyao Ukawekwa mkakati wa kuwaondoa(Rejea mabandiko ya nyuma)

LOWASSA
Ni mwanasiasa alijijenga ndani ya chama licha ya makando kando aliyo nayo.

Tulieleza katika nyuzi hii na nyingine, nguvu ya Lowassa haitokani na utashi wa jamii bali watu wanaoona ipo haja ya mheshimiwa kupata uongozi ili kulinda masilahi yao.

Wanaompigania si waumini wa sera au maono, kwamba mwisho watamwacha mwenyewe.

Tuliwaita ‘wafanyakazi' na kwamba kazi itakapokwisha , itategemea kama upo ushindi au la.
Kinyume chake watajiunga na makundi mengine. Kwao haikuwa siasa bali masilahi.

Ndivyo ilivyotokea. Tulisema pia, Lowassa hawezi kuhama na watu.
Atakaohama nao ni wale wale waliokuwa na masilahi na CCM itabaki kama ilivyo.

CCM KUPASUKA

Tulisema pia CCM haiwezi kupasuka kwasababu wanaoondoka si wanachama watiifu ni wanachama wenye masilahi.

Lowassa hawezi kuimega, wafuasi wake wanaitegemea CCM, haiwezi kupasuka isipokuwa upo uwezekano wa kudhoofika

KUUDHOFIKA
Katika kudhoofika, wapo wanachama watahama kwenda upinzani katika makundi matatu

  1. Waliochoshwa na utaratibu wa chama kushughulikia masuala ya kitaifa
  2. Walio na hasira za mgombe wao kupigwa chini
  3. Wanaoona ni wakati nchi kubadilika, hasa tukizingatia mijadala kama ya BMLK, Bunge la JMT n.k.

Kutokana na hilo, uwezekano wa wapinzani kutwaa dola(Plan A1 na Plan A2) ulikuwepo.

Hata kama ungekuwa ni kwa asilimia ndogo, kilichowazi ni kuwa Plan A2 ya kumiliki bunge ingefanikiwa.

Kumiliki ina maanisha CCM wasingekuwa na wingi 2/3 jambo ambalo lingewezesha wapinzani kupata nguvu ya kushughulikia mfumo mbaya mahala pa kuanzia

Mfano, serikali isingeweza kufanya kazi bila makubaliano na wapinzani.

Hapo pangewezekana kujenga mazingira ya mambo makubwa ya kitaifa kama Katiba, kubadilisha mifumo ya taasisi kama zile tume za uchaguzi na kuweka udhibiti wa vyombo kama Polisi ili vitoe haki.

Hadi hapo mfumo wa CCM ungeshaanza kudhoofika na pengine rungu lingefuata.

Lakini pia ingesaidia sana kuwajenga wapinzani mbele ya macho ya wananchi, tayari kushika dola .

Wangalikuwa mstari wa mbele kujenga hoja za kitaifa, ikiwemo kubadili mfumo taratibu kwa kuudhofisha kisha kuua kabisa

Inaendelea…
 
Sehemu ya III

LOWASSA WAVURUGA WAPINZANI

Baada ya kuona kuna wimbi nyuma yake, wapinzani wakavurugwa kwa kudhani ujio wake utaambatana na wingi wa wanachama au kutwaa majimbo na dola.

Wapinzani wakapoteza mtazamo wa kuchagua mtu anayekubalika kuendeleza agenda waliyokuwa nayo mbele ya uso wa wananchi

HESABU, TAKWIMU NA KUSHINDWA KWA WAPINZANI KATIKA SIASA ZA JAMII

Wapinzani wameshindwa kusoma tatizo la jamii ambalo ni mfumo mbaya uliozaa ufisadi

Lengo la wapinzani halikuwa kupata Rais wa nchi tu, bali kubadili mfumo mzima.

Hakuna namna ya kubadili mfumo kama wanaotumikia mfumo ule ule wapo.

Nia ya wananchi ni kuona sura mpya zikishughulikia tatizo la mfumo.

Hivyo, hoja si watu au mtu ni taasisi itakayobadili mfumo mzima

Wapinzani wameshindwa kusoma sayansi ya jamii ya wananchi, tatizo ni ufisadi wakiamini umasikini unaowakumba ni zao la mfumo Wananchi hawapendi kuona wanaotumikia mfumo ndio wanabadili ‘jezi' kubadili mfumo wa miaka nenda rudi

Wapinzani wameshindwa kusoma,hali ya uchumi ndiyo inawapa wananchi fadhaa ‘frustration' na kuchukia mfumo wa CCM

Wapinzani wameshindwa kusoma alama ya kwanini CCM waliacha ‘dhahabu' mchangani wakaamua kwenda mbele

Lakini kubwa zaidi, wapinzani wanaposhindwa kufanya hesabu pengine kwa kukosa wataalamu wa mambo ya kisiasa

HESABU MBAYA

Endapo wanaamini Lowassa ana nguvu, kwanini wasimwache akaenda kujiunga na chama kingine?

Hapa maana yake, yeye angekuwa upinzani na wabunge wake, na wapinzani na wabunge wao, kwa pamoja wangeweza kupata zaidi ya 2/3 na kudhibiti mfumo bila kuathiri taathira yao mbele ya jamii

Wapinzani hawana hesabu, ni watu wangapi watajiunga nao kama zao la kumokea Lowassa.

Kuna uwezekano kundi lake dogo lenye masilahi naye likamuunga mkono, na kuacha umma mwingine ukiwa umeduwaa.

Hadi sasa wanaomuunga mkono wamechukua fomu CCM , nao wana wafuasi nyuma yao. Nini wapinzani watarajie hapo

Ukawa, na hasa Chadema upepo wa kisiasa ulikuwa unavuma kuelekea kwao.

Kwa hali yoyote wangebaki na politicala base yao na kuchukua makundi mengine.

Kihesabu wangeongeza zaidi ya kupoteza lakini sivyo!

Inaendelea..
 
WAPINZANI WATAPOTEZA

Ukawa iliungwa mkono na makundi yafuatayo
1 Wasomi
2 Vijana
3 Na watu wenye kiu ya mabadilo bila kujali itikadi zao

Nguvu yao ilikuwa kuhakikisha makundi hayo yanabaki kama yalivyo, na kuendelea kupigania makundi maengine ya CCM

Agenda wanayo na inakubalika usoni mwa wananchi.

Hakukuwa na sababu za kuamini mtu mmoja na si taasisi anaweza kuiondoa CCM madarakani.

Kutokana na mwendo huu Lowassa anahamia na kupewa kazi ya uchaguzi , yapo maswali mengi sana ya kujiuliza

Hivi lini Lowassa aliwahi kusimama na wapinzani pamoja? Tunaweza kusema Filikunjombe amewahi japo mara moja

Hivi lini Lowassa alisimama na kuunga mkono hoja za wapinzani?

Hivi ni nani kama si huyu Lowassa aliyewashughulikia wapinzani wakiwa waziri mkuu

Ni lini Lowassa amesoma sera za chama akazikubali na kuzielewa

Hivi wakati Ukawa wanatoka BMLK na Bungeni, Lowassa alikuwa wapi kuwaunga mkono ?

Ni lini Lowassa alionyesha kuchukizwa kwake na wapinzani kunyanyaswa?

Ni lini Lowassa alisimama kupambana na hoja ya ufisadi, hoja waliyokuwa wamebeba wananchi?

Na endapo ana nguvu za kisiasa, nini kimekwaza asiaznishe chama chake bali ajiunge na upinzani?

Je, tatizo la watanzania ni mfumo mbaya au ni kupata viongozi wale wale kwa jima la wapya?

Nini agenda ya Ukawa mbele ya mahakama ya wananchi?

Je, Lowassa anakuja peke yake au na mizigo yake?
Wenyeji watakuwa na hali gani katika kuhimili kishindo cha wenye nazo?

Hoja hizi zitakapogonga katika vichwa vya watu tutarajie haya

Ukawa watapoteza kundi kubwa sana la wasomi

Ukawa watapoteza kundi kubwa sana la political base yao

Watapoteza kundi kubwa la vijana

Ukawa watapoteza kundi kubwa sana la wananchi waliokataa tamaa

Tutakachokiona ni watu wengi kujiandikisha, wachache kupiga kura.

Katika sanduku la kura, wananchi watajiuliza maswali juu ya uchaguzi, ima zimwi likujualo au mvinyo wa zamani katika chupa mpya.

Hapo hesabu hazisimami na Ukawa hata kidogo

Haiwezekani kupoteza watu 100 ili kupata wapya 70 ukasema kuna mafanikio.

Haiwezakani chama kikapoteza political base yake, kitarajie ushindi

Haiwezakani kuleta mtafaruku ‘confusion' kwa muda mfupi utarajie ushindi

Inaendelea..
 
HITIMISHO

Wapinzani wamecheza karata mbovu bila kuzingatia ukweli.
Maamuzi yao yanajengwa katika uharaka wa kwenda kugawana vyeo na si kubadili mfumo.

Hakuna uwezekano wa kumleta mtu aliyelea mfumo unalolalamikiwa wananchi wakawaelewa

Wapinzani wana kazi kubwa kwa muda mfupi wa kubadilisha akili za wananchi.
Kitendo cha kuamini mtu na si taasisi ni dalili njema kuwa hawakuwa na maandalizi.

Hakuna hesabu, takwimu au tarakimu zinaonyesha kumwalika Lowassa kunaweza kubadili hali ya mfumo

Tatizo la Watanzania si mtu au kundi la watu. Ni mfumo mbaya uliojijenga kwa muda mrefu

Mfumo huo hauwezi kubadilishwa na watu wale wale wenye tuhuma nzito za kuutumikia.

Kama lengo ni kwenda Ikulu, karata iliyochezwa ni mbovu sana.

Miaka 20 wapinzani wanaposhindwa kutoa mtu mbele ya wananchi ni kitendo cha dhalili

Duru tunaamini kwa dhati kabisa, tendo la wapinzani ni kusaliti mageuzi.

Hakuna uwezekano wa kuondoa mfumo uliopo na kuleta mabadiliko kukiwa na watu wale wale.

Kitakachotokea ni kumfanya mtu kuwa taasisi na wananchi kukosa kauli

Hakuna namna yoyote inayoweza kueleza jinsi wapinzani walivyofikia hatua hiyo.

Ni hatua isiyoonyesha mwisho si mzuri, ni hatua iliyojaa ubinafasi zaidi ya masilahi mapana ya taifa

Tunasimama kusema, kwa hili, Chadema na Ukawa wanaompokea Lowassa wameyakana mabadiliko

Mwisho wa siku, historia itawakumbuka si kwa wema bali kwa haya mnayoyafanya,

Umma hauwezi kuelewa mikipigana na ufisadi huku mkiosha mafisadi

Safari mnayodhani imeanza, huenda ikawa imefikia tamati.

Tunarudia, kijamii , kisiasa, kitakwimu na tarakimu tendo mlilolifanya halina tija na msimame kuhesabiwa wakati ukifika.

Mbowe, Lipumba, Mbatia, Slaa mlichokifanya ni zaidi ya fedheha!

Taifa mbele, na kila mtu ataubeba mzigo wake

Haonewi mtu wala hahurumiwi, hoja zitasimama duru za siasa bila kupepesa macho

Ukweli unatuweka huru

Tusemezane
 
Binafsi nimekata tamaa sana, iti will take many years kupata mabadiliko, maana tuliotegemea watuvushe kumbe nidhaifu hawajiwezi nao wanahitaji kuvushwa, ohoooo Tanzania my country, i feel cry why why?? wamekosa maarifa kabisa ma busara mpaka kuamua jambo hili kubwa na la hatari kiasi hiki? Kimsingi hawa viongozi hawaaminiki tena na ni dhaifu mno hawajiamini.
 
Habari hizi hazikuumizi wewe tu bali ni watanzania wote, tuliokuwa na imani na Chadema/Ukawa, tuliokuwa na imani na viongozi wetu, tuliopata majeraha kwa ajili ya Chadema/Ukawa, tuliokuwa mstari wa mbele kuelemisha wananchi jinsi ufisadi unavyowaadhiri wao na familia zao na nk.

Leo hii hawa viongozi tuliowaamini kuwa viongozi wetu wanajifungia chumbani na kuja na maamuzi ya kipumbavu namna hii. Hawezekeni viongozi wasiozidi 20 wajifungie ndani na kutuchagulia mgombea urais, hii haki hawana na hawatawahi kuwa nayo. Na kama wakingángánia na msimamo wao, ambao kipaumbele kwao ni matumbo yao basi huyu Lowassa wakamchague wenyewe..

Pendekezo langu ni kuwa watuache wananchama tuchangue ni nani tungependa hawe mgombea wetu.. Huitishwe uchaguzi kila kanda/ au hata baadhi ya mikoa ili wanachama wapinge kura ya ni nani kwa mtazamo wao wanaona anafaa kupeperusha bendera ya Ukawa. Kinyume cha hapo ni "usaka tonge tu hakuna lolote"n Maana haiwezekani miaka yote viongozi wetu wamnage kuwa Lowassa ni fisadi halafu leo hii ndo awe lulu ya kupeperusha bendera ya chama.

Kama ni tamaa ya pesa/madaraka hii ni too much. John Mnyika , Dr.W.Slaa na wengineo oneni aibu..
Alinda, kama utakumbuka, hapa duru tumewahi kuwaeleza UKAWA kuwa hawana rasilimali na muda.
Walitakiwa wakimbie wenzao wakitembea. Leo ni August bado wana kigugumizi

Sioni utaratibu gani wanaotumia. Tuliwahi kuandika kuwa Ukawa ni top-bottom na hilo ni tatizo. Kinachoendelea si kujipanga ni kubabaika.

Katika siasa hii ni moja ya set back na itawagharimu sana. Gharama zake ni za maamuzi ya zimamoto yasiyozuingatia hali na wakati. Haiwezekani miaka yote watu hawa wasijue wanataka nini! Si kuwa inashangaza, bali inatia shaka sana
 
Binafsi nimekata tamaa sana, iti will take many years kupata mabadiliko, maana tuliotegemea watuvushe kumbe nidhaifu hawajiwezi nao wanahitaji kuvushwa, ohoooo Tanzania my country, i feel cry why why?? wamekosa maarifa kabisa ma busara mpaka kuamua jambo hili kubwa na la hatari kiasi hiki? Kimsingi hawa viongozi hawaaminiki tena na ni dhaifu mno hawajiamini.
Mkuu kama tulivyosema, hesabu zilikuwa zinawapa nafasi sana Chadema na Ukawa, hawahitaji msaada wa mtu

Mfano, Lowassa angeenda popote au kubaki CCM kura za CCM zingepungua kwa hali yoyote, ima kumfuata huko aendeko au wafuasi kususa wakiwa CCM. Hakuna athari kwa ukawa, ipo faida kwasababu ilikuwa kudhoofika kwa CCM

Kwa hali inayoendelea, hesabu zimevurugika, watapata na kupoteza sana wakikumbatia haya yanayosemwa

Inasikitisha sana!
 
sasa yametimia rasmi, Tanzania hakuna upinzani kwa sasa, makelele yoooote tunayopiga hayana maana hawajayaona wametupuuza, out of all people wamemuona Lowassa kama mkombozi, so painful, inaniuma sana. Siamini, Ndani ya mwezi mmoja UKAWA hususan CDM wameharibu taswira yao nzuri na mazuri yooote wameyaharibu. Let us wait mwisho wake
 
UKAWA wamevunja mioyo ya watanzania wengi sana hasa wahafidhina wa Chadema ambao ndugu zao na wao walipigwa kwa ajili ya chama.
Kwanin wasijiamini wamsimamishe mgombea wao? Ina maana Dr. Slaa haaminiki kuwaongoza watanzania?
Nadhani huu ni mpango wa CCM kuihujumu Ukawa, umesukwa toka siku nyingi sana. Ni kwamba Lowassa akatwe CCM aje kugombea Ukawa.
Uchaguzi wa mwaka huu ni kama tumewekea wagombea wawili wa CCM katika rangi mbili tofauti. Lowassa akikosa urais watamlaumu? Watajilaumu? Watamlaumu nani hasa?
Akikosa ina maana Ukawa watakuja na wimbo gani kurudisha imani za wananchi zilizokufa?
Lowassa akipata atasimamia maslahi ya nani? Kwanza anajua kwanza kile Ukawa wanataka?
Nadhani wanakusoma vema.
 
hii habari ENL inaniumiza sana nafsi yangu.. mungu tusaidie waja wako.. fanya moyo wa farao uwe mgumu..
Mkuu Nguruvi3,
I feel so disappointed kwq habari hizi, kama zina ukweli wa aina yyt inauma sana kwamba kumbe wapinzani hawaezi kusimama kwa miguu yao, so embarrassing so painful, why?? Kwa nn wasubiri waliokatwa ndio waje wawabebe kwenye uraisi,
Naamini wanancji wengi wanawakubali na wapo tayari kuwaamini kama tu nao watajiamini sio kumtegemea mtu mwenye uchu na madaraka awabebe.
Poor UKAWA/CHADEMA.

Mtajutia hicho mnachotaka kukifanya.

Ni usaliti wenye manufaa yaliyo tabiriwa. Upinzani Wa Kweli Utatokana CCM yenyewe.

Alinda;13427218]Habari hizi hazikuumizi wewe tu bali ni watanzania wote, tuliokuwa na imani na Chadema/Ukawa, tuliokuwa na imani na viongozi wetu, tuliopata majeraha kwa ajili ya Chadema/Ukawa, tuliokuwa mstari wa mbele kuelemisha wananchi jinsi ufisadi unavyowaadhiri wao na familia zao na nk.

Leo hii hawa viongozi tuliowaamini kuwa viongozi wetu wanajifungia chumbani na kuja na maamuzi ya kipumbavu namna hii. Hawezekeni viongozi wasiozidi 20 wajifungie ndani na kutuchagulia mgombea urais, hii haki hawana na hawatawahi kuwa nayo. Na kama wakingángánia na msimamo wao, ambao kipaumbele kwao ni matumbo yao basi huyu Lowassa wakamchague wenyewe..
'This is one too many'' Sauti hizi zinaweza kupuuzwa na UKAWA kwa muda, mbele ya safari zitasikika pamoja na zile za nyikani, sitaki kubashiri ...!!!

Kwamba, taasisi inasimama kama mtu, I can't wrap up my head

Kwamba, mtu anachukua umiliki wa taasisi! Real
 
Back
Top Bottom