2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,406
31,387
UTANGULIZI

Joto la uchaguzi 2015 linapanda kwa kasi.
Tofauti na nyuma,mwaka huu kutakuwa na mitazamo tofauti baina ya vyama na ndani ya vyama


CCM ikitaka kuendeleza utawala wa miaka 50, wapinzani wakitaka kumaliza miaka 50 ya CCM.

Ni uchaguzi uliotanguliwa na wa serikali za mitaa uliotoa matokeo yasiyotarajiwa
yanayoitia CCM hofu ya kuungana na UNIP–Zambia au KANU-Kenya
katika maktaba

Kwa updande mwingine, ni uchaguzi unaokuja wapinzani wakizidi kuimarika katika vyama vyao au umoja wao wa UKAWA

Na ni uchaguzi unaokuja wananchi wakiwa katika hali tofauti zamitazamo

1 Kuondokewa hofu kuhusu upinzani kama vyama vya kuvuruga Amani

2 Hali ya maisha wakitazama umasikini waku titia na utajiri unatopea

3 Kupanda kwa gharama za maisha na kuvia kwa huduma za jamii na umma

4 Kupoteza matumani (hope) ya hatima ya nchi yao na kizazi kjacho

5 Kubobea kwa rushwa kama mfumo wa maisha ya nchi naWananchi

6 Kukiwa na mtafarauku wa zoezi la katiba kushindwa

7 Majaaliwa ya nchi katika muskabali mzima wa muungano

Kwa vigezo vyovyote uchaguzi hautabirikii .Siasa ni mchezo usiotabirika na wenye kutoa matokeo tofauti na inavyodhaniwa

Majibu, utabiri na ukweli wa uchaguzi upo kwa kundi moja tu,Wananchi.

Je, wananchi wanatambua wameshika karata muhimu kwa mustakabaliwao?

Je, wananchi wanajua maana ya uchaguzi na athari zake chanyana hasi?

Je, chamatawala kitaendelea kushika hatamu ya nchi?

Je, wapinzani wamejipanga kusahihisha makosa ya siku zilizopita?

Je, mvutano ndani ya CCM,utabiriwa kuparaganyika utatimia?

Je, Wananchi wamechoka, na watatafuta mabadilikonje ya CCM?

Je, hali ya wapinzani na upinzan iipoje kuelekea Oktoba?

Tutakuwa na mfululizo wa mabandiko kuangali uchaguzi kwa ujumlawake.

Katika mfululizo wa mabandiko, tutajadili

Umuhimu wa uchaguzi na kwanini Watanzania hawajaelewa

Changamoto zinazokabili pande mbiliza uchaguzi(watawala na wapinzani)

Mtazamo wa wagombea watarajiwa katikahatua za awali. Hali ya chamatawala baada ya miaka50

Mbinu mpya za CCM kuzuia mabadiliko ya kisiasa nchini(miswada ya sheria inayokimbizwa bungeni kwa hati za dharura)

Tunaomba uvumilivu wakati ukifika tutasemezana

Hakitaachwa kitu, mtu, watu au kundi. Nchi kwanza
 
SEHEMU YA I

Uchaguzi ni madiwani wabunge, na Rais (atakayeunda serikali)kutoka kwa wabunge

Mtiririko unaonyesha viongozi watakavyogusa maisha ya wananchi popote walipo

Ni zoezi la kuchagua au kuchaguliwa, kuchukua nafasi ya ofis ikwa njia ya demokrasi .
Ni hatua ya kupata wanasiasa wenye mamlaka kuhusu maisha yetu ya kila siku


Kutakuwa na uchaguzi wa awali(preliminary elections), na uchaguzi mkuu (general election) ukishindanisha hoja, sera na mitazamo tofauti ya kuendeshanchi

Wachaguliwa watatunga sheria,watapanga na kutekeleza mipango inayotuhusu sote

Ni kosa kudhani ni msimuwa mavuno au sadaka kati ya wachaguzi na wachaguliwa.
Ni uinga kushabikia mavunoya siku kadhaa, tukibaki na adha ya miaka kadhaa


Uchaguzi si suala la bahati nasibu, ni suala la fikra na maamuzi sahihi
Wanasiasa hutafuta makundi muhimu ya kulaghai na tayari wameshaanza

Haiwezekani wazee wa EAC wadai bilioni 10 hadi leo
na wengi wameshafariki, eti liwepo kundilinalodai bilioni 80 na kuahidiwa kulipwa kabla ya uchaguzi mkuu!!


Uchaguzi ni suala la hatima ya miaka 5 na ijayo. Siyo khanga na kofia kwa siku moja.
Hatuchagui machifu wa makabila, viongozi wa dini au kanda.
Tunachaugua viongozi wataifa


Kujiandikisha, kupiga kura, kufanya uchaguzi sahihi unaozingatia ukweli ni muhimu.

Kinyume chake, Watu wawe tayari kwa maumivu ya miaka mingiijayo


Inaendelea…
 


SEHEMU YA II
CCM NA HATIMA YA UTAWALA

Mfumo wauchaguzi wa CCM ni ule uliozingatia uteuzi wa mtu kutoka kikundikilichoaminiwa, Si ushindanishi wa wagombea kwa hoja na kura(popular vote)

Na ndivyovyama vya upinzani vilivyoacha taratibu zao nakuiga CCM. Ni ule utaratibuVanguard party ambapo kamati ya utendaji (politburo) iliamua kuhusu uongoziwanchi katika nchi za kikomunist

Utaratibuhuo ulikuwa mzuri zama za TANU ili kuwaunganisha wananchi.


Kwamba,anayechaguliwa na kamati ndiye anakuwa mkuu wa nchi ili kujenga mshikimano naumoja.Utaratibu uliwezekana katika mazingira ya nyakati zile ili kujenga uzalendona umoja wa kitaifa

Dhana hiyoilijenga hali ya chaguzi za Rais na Wabunge kuwa pamoja.

Uchaguzi waRais ulikuwa ‘uteuzi' na wabunge ilikuwa kushirikisha wananchi (participation),Rais akiwa alama ya umoja inayoshirikisha wananchi kupitia wabunge

Hata hivyo,uchaguzi wa Rais na Wabunge ni vitu viwili vyenye maana tofauti.

Ule wa Wabunge ni kuwashirikisha katika kuchagua(popular participation andpopular choice) na wa Rais wananchi hawakuchagua bali walichaguliwa na kundi lawatu
lililoaminiwa

Lengo lakuwa na mfumo wa uchaguzi wa TANU/CCMilikuwa kujenga utaifa ndio maana mwandishi E.Sigmund (One party rule)anamnukuu Mwalimu Nyerere akisema

"New nationslikeTanganyika are emerging into independence as a result of a struggle forfreedomfrom colonialism…



Once the first free government is formed, its supreme task lies ahead, thebuilding up the country's economy, so as to raise the living standards of thepeople, to eradicate disease, to banish ignorance and superstition.

This isno less than the struggle against colonialism, calls for maximum united effortby the whole country it is to succeed.
There can be no roomfor difference or division…



This is our time of emergency and until or war against poverty, ignoranceand disease has been won, we should not let our unity be destroyed by a desireto follow somebody else'sbook of rules''

Harakati za kutokemeza ukolonihaziwezi kuwa kichocheo cha umoja wetu tena.
Hata hivyo, maadui watatualiosema mwalimu, ujinga maradhi na umasikini bado wapo.
Hatuwezi kupigana na maadui haotukiwa tumepraganyika.

Hivyo, umoja wa kitaifa ni jambolinalohitaji hata sasa, itakuwa upuuzi kumsikiliza mgombea asiyeweza kutoa hojazenye kujenga umoja wa kitaifa

Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumiyanapaswa kuakisiwa na vyama vya kisiasa bila kuathiri hoja muhimu za kitaifakama umoja.

MwalimuNyerere aliliona hilo nakutahadharisha ''CCM isipofanya mabadiliko, wananchi watayatafuta nje ya CCM'

Mwalimualifahamu mbadiliko ya kisiasa na kiuchumi duniani yaisngeweza kuicha CCM nanchi pembeni.


Aliwataka wanaCCM kufanya mabadiliko ili kukidhi haja ya nyakati mpya.

CCM hawakumelewa Nyerere wakaenda njia wanaojua wao,ambayo leo inawatesa, na initishia kuwaondoa katika ulimwengu wa siasa!

Inaendelea...
 

SEHEMU YAIII


CCMNA MAHANGAIKO

Mabdiliko aliyosema Nyerere ilikuwa kukirudisha chama mikononi mwawananchi.
Mfumo wakiuchumi wa soko huriaukaambatana na kufutwa kwa azimio la Arusha
.

Azimio la Arusha halikuwa na kitukingine zaidi ya kile Nyerere alichosema matumaini(hope) kama tunavyo mnukuu hapa akiwaambia viongozi'' The fact is not that the Arusha Declaration hasbanishedpoverty even by an iota – nor did it promise to do so.

The ArushaDeclarationoffered hope. A promise of Justice, hopes to the many, indeed themajority ofTanzanians continue to live this hope.

So long as there is this hope,you will continue to have peace..

Arushadeclarationdid not do away with poverty but it has given you all in this hall,capitalistsand socialists alike, an opportunity to build a country which holdsout a futureof hopes to the many''

CCMwalipofutaAzimio la Arusha badala ya kulifanyia maboresho, matatizo yakaanzakuwapata
Maadilinauadilifu kupotea na kuchomoza kwa ubepari(tycoons).

Mabepari wakajipenyezakatika nafasi muhimu za chama na kushika hatamu.
Chama kikaondoka kwa wananchina kwa taasisi binafsi (NGO)


AzimiolaZanzibar likazika matumaini(hope) na kuzaa matajiri( tycoons).

Matajiri wakatumiapesa kumiliki chama kwa vile CCM haikuwa na vyanzo vya mapato kama ilivyokuwaawali(serikali)

Mabepari wakajengamatabaka aliyoonya Mwalimu Nyerere'' Here inTanzania we have poverty but no‘social cancer'.
It is possible it has justbegun. But otherwisewe don't have asocial cancer.


There isn't aVolcano in the making, that one day it is bound to erupt. We have notyet reached thatstage because the people still have hopes based on the standtaken by theArusha Declaration''

Wananchi wameendeleakuichagua CCM si kwasababu inatoa majibu ya matatizo yao, bali mazoe ya kuwandicho chama kinachosimamia amani na utulivu wa nchi.

MwalimuNyerere aliwahi kusema kwa viongozi ''To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzaniansthroughcoercion, When there is no hope, and then expect that they will sitquiet inpeace?


Peace is born of hope, when hopeis gone, there will be social upheavals.
I'd be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel''

Tunaona watanzania wakiwa‘rebel' kutokana na kushamiri kwa mtabaka yamasikini na matajiri, rushwa kamamfumo rasmi wa maisha na uvunjwaji wa haki za binadamu


Nyerere akasema ‘Unless these people are fools. Many in these countriesare fools, toaccept being ruled just like that.

To be oppressed just like thatwhen they have the force in numbers, theyare fools.

So Tanzanians would be fools…. ifthey continued to accept to be oppressed by minority in their own country


Inaendelea…




 
SEHEMU YA IV

CCM YAPOTEZA USHAWISHI . INA ‘SURVIVE' KWA MBINU NASI SERA

Wananchi wameonyesha ‘rebellion' aliyosema Nyerere. Wamekumbatia mbadiliko aliyoonya Nyerere, wanatafuta mabadiliko nje ya CCM. Ni kwa kupoteza matumani(hope) kunakotishia amani na utulivu

CCM haishindi chaguzi kwa nguvu ya ushawishi iliyokuwa nayo, wala mazoea ya wananchi kuiamini tena.

Wengi wanaiona kama gulio la wachuuzi wenye fedha na wao wananchi kama wapagazi


Uasi' rebellion' aliyozungumzia Mwalimu ipo wazi si kwa wananchi bali ndani ya CCM yenyewe.

Chama kimegawanyika kati ya matajiri nawazalendo. Matajiri wana nguvu ya pesa, nguvu ya kuamua nani akae wapi kulinda masilhi yao.


Chaguzi zilizopita zinaonyesha CCM kuishiwa mbinu.Udanyaifu wa amani na utulivu hautui tena katika masikio ya wananchi.

Mbinu za kutumia vyombo vya dola zinadhibitiwa na wananchi. Wizi na udaganyifu katika sanduku la kura sasa imekuwa kazi ya wananchi.

‘Uasi' dhidi ya CCM umeshika kasi na zipo dalili huenda ukawa ndio mwanzo wa mwisho


MBINU MPYA ZA CCM KUENDELEA KUTAWALA

Kuvurugwa kwa mchakato wa katiba ni zao la matajiri wanomiliki chama kuhofia mabadiliko yenye kutishia masilahi yao.

Kwa makusudi wakatisa uongozi wa chama na kufanikiwa kuharibu mchakato


Mbinu nyingine ni kuhakikisha wanadhibiti maeneo muhimu sana katika udanganyifu.

Sheria ya mitandao haikulenga kuzuia uhalifu tu, ndani yake ililenga kuhakikisha hakuna habari zinazovuja zitakazo watia hasira wananchi zaidi. Ndio maana mleta habari na mtoa habari wamewekewa sharia


Sheria ya takwimu ilikusudia kudhibiti habari nje yazile CCM wanazotaka zisitumike.

Kwa maana, NBS ikshatangaza takwimu hakuna wakuzipinga.Hakuna atakyeweza kuhoji kwasababu sheria haimruhu kuja na takwimu mbadala.
Ni katika kuzuia mitandao isilete au kuanika uozo wama tycoon, na serikali kwa ujumla.

Mbinu zinazidi kutengenezwa. Kuna mswada wa sharia unaoelekeza kuwa vyombo vya habari vijiunge na TBC saa mbili kwa taarifa yahabari.

Hili ni jambo lililotengenezwa makusudi ili kuhakikisha kuwa sheria ya habari za mitandao, sheria ya tawimu zinatumika kwa kupitia habari za TBC.

Wananchi wanalazimishwa kusikia habari CCM. Ikitoa takwimu, taarifa na maelekezo yafuatwe na watu wote


Ni mbinu za kuhakikisha CCM inashinda, si katika kura bali kwa kwa kutumia vyombo vya umma na sheria ziziliotengenezwa kuwasaidia na si kusaidia nchi

Hivi kwanini serikali ya CCM isitunge sheria ya kulazimisha vyombo vya habari kama BBC na CNN kuwa na muda wa kusikika kamaTBC?

TBC haiwezi kusikilizwa kama haikidhi haja. Hili nisoko huria lililoanzishwa na CCM hao hao, leo wanataka turudi enzi za kulazimisha wananchi kusikiliza habari wanazotaka wao zisikike

CCM wangejiuliza, ni kwanini wananchi hawasikiliziTBC ?
Kuna kitu gani cha ziada kwenye vyombo binafsi kinachovutia wananchi?


Vyombo binafsi vinalipa kodi, nani atafidia muda wao?
Na ule uhuru wa habari upo wapi? Ni wapi duniani wananchi wanalazimishwa kusikiliza habari za serikali?


Yote ni katika kuminya uhuru wa habari, ili CCM itumie sheria inazotunga sasa,kulazimisha matokeo ya uchaguzi kwa namna wanayotaka na si wananchi wanavyotaka

Chanzo cha CCM kuwaya waya ni kupoteza ushawishi,kuporwa kwa chama na matajiri na kuacha misingi iliyokianzisha, kukikuza nakukilea.

Mbinu zinapangwa kukinusuru chama kutokana na kuporomoka kwa ushawishina umaarufu.


Sheria ya mitandao, takwimu nah ii inayoandaliwani ''utatu mtakatifu wa CCM'' kushinda kwa mbinu


Inaendelea....
 


SEHEMUYAV

MINYUKANO NDANI YA CCM.

NI KATI YA MAKUNDI YALIYOPORA CHAMA

WAZALENDO WAMEBAKI WATAZAMAJI NA WAHEMEA NJAA

Uteuzi wamgombea wa CCM si kama ulivyokuwa awali chini ya ‘politburo' naNEC.

CCnaNEC zitatoa jina la wagombea. Mkutano mkuu utapiga kura ya kuamua.
Ukweli,CC na NEC huamua hatma ya mgombea awali kabisa. Vyombo hivyo vimetekwanatycoon!watasema nini


Mnyukano uliopo si kupata mgombea safi, ni kati ya makundi yenye fedha yanayotaka kupeleka mtu wao wanapotaka

''Watekaji''wanafahamu,ili kuidhibiti nchi ni lazima wadhibiti uongozi mkuu wa chama, na udhibiti wabunge.

Kufanikisha hayo,lazima uwepo udhibiti wa CC na NEC ya CCM


HAKUNAMSAFINDANI YA CCM

CCM imeongoza miaka 50, hali inazidi kuwa mbaya kisiasa, kiuchumi na kijamii.


Imefika mahali magenge ndiyo yanayoamua hatma ya nchi chini ya mwamvuli wa CCM.

Miaka ya karibuni na hasa minne iliyopita, mwenyezi mungu amewaonyesha Watanzania tatizo linaloikabili nchi.

Hakuna asiyejua nchiyetu ‘imetekwa ' na mafisadi. Rushwa kubwa na ufujaji ni mifumoiliyokubaliwa


CCM haisimami kukemea au kudhibiti rushwa. Serikali ya CCMni eneo la kusafisha watu waliolitia taifa hasara kwa masilahi yao. Wezi wanatakaswa hata ushahidi unapovuka kiwango cha kawaida cha akili za wanadamu

Tumeona matajiri walivyoweza kukidhibiti chama hata kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wale wanaokichafua.

Viongozi wanatishwa na kutishika, wamebaki kubweka kama mbweha.


CCM-serikali inapolalamikia kuongeza rushwa,inaeleza ukali wa tatizo na jinsi ilivyoshindwakulikabili

Ili awaye aweze kukubali au kudumu ndani ya mfumo wasasa wa CCM ni lazima mtu huyo akubaliane na mfumo uliotengenezwa rasmi na matajiri, mafisadi na walaghai ndani ya CCM

Tujiulize,hivi kuna uwezekano wa kupata mtu mwadilifu kutoka katika kundi la wahalifu?

Mtu msafi atapatikanaje ikiwa yupo katika mfumo ule ule anaoshindwa kuuzuia au kuukemea sasa hivi?

Wazee wanafunzi wa Mwalimu na viongozi (mawaziri wakuu) wameondolewa katika vikao vya maamuziya chama.
Ni nani ndani ya CCM amebaki msafi
Miaka10 tumeshuudia kila aina ya ‘wahalifu' ndani na nje ya serikali.

Ni nanani katika serikali ya CCM alisimama nawananchi? Ni nani ndani ya bunge la CCM alisimama na wananchi?

Ni na nindani yabunge la katiba alismama na wananchi? Leo ni nani kutoka ndani ya CCM anawezakusema ni msafi?


Maamuzi yote tumewasikia wakiegemea maamuzi ya chama. Hata nchii lipoporwa, bado walisimama nachama.

Ni chama tunachojua si cha wanachama bali matajiri waliopora kutoka kwawananchama.

Hivi nani anaweza kuwa na msimamo wa CCM, akaja na msimamo mwingine nje ya ule wa chama alioutetea kwa nguvu zote kwa miaka yote?

Wananchi wajiulize kwa wepesi. Unawezaje kufuga Chui ukategemea ipo siku atazaliwa Mbuzi?

Ni lini ufugaji wa fisi uliwahi kutoa uzao wakondoo?

Ni lini mwewe anaweza taga mayai yakatotolewa kama Njiwa na kuku wazuri? Lini nzi wanaweza tengeneza masega ya asali?


Ndani yaCCM na serikali yake iliyofikisha tulipo, ni mwananchi gani anaweza kutushawishi‘mnyukano wa fisi na Chui' utatueletea Mtamba(Heifer)mzuuri wa maziwa na tani za nyama saafi?

Tunauliza swalihili mara nyingi kwasababu kiwewe walicho nacho wananchi kuhusu wagombea wa CCMni kana kwamba, lipo shindano la manabii na wananchi wanatakiwa kuchagua mmoja!!

Wengine wanaona lipo shindano la kufuga fisi na Chui,na ndio maana tunauliza, hivi chui au Fisi,wana uwezo wa kutuzalia kondoo! mitamba ya maziwa au mbuzi wanyama choma?

Inaendelea….



 
Tunasubiri umalize mnakasha ili tujimwange,,

Nimeguswa na sehemu ya kwanza hasa kuhusu Ukawa. (Vyama vya upinzani) tuna vyama vya upinzani zaidi ya 20 lakini kwa bahati mbaya sana ni vyama viwili tu vilivyo "busy" na uhamasishaji wa uandikishwaji katika daftari la kudumu..

Hatusikik chochote kuhusu "Tume huru" sasa sijui wanasubiri baada ya matokeo ndo waanze zile hadithi zao za tumeibiwa kura?!
 
SEHEMU YA VI

WANANCHI MNAKUMBUKA AU MNASOMBWA NA MKUMBO?

Wananchi wa Tanzania ni watu wa ajabu sana. Ni wepesi wa kulalamika, ni wepesi wa kusahau.

Ni wepesi wa kunung'unika ni wepesi wa kusamehe.
Ni wepesi wa kukubali huduma za mdomo'lip service' ni wepesi wa kukubali maumivu.

Miaka nenda rudi wamepiga kura katika kutafuta hali nzuri.
Miaka 50 suruali walizovaa zimejaa viraka na mashimo yanaongezeka. Kanga walizojitanda zimegueka kuwa magunia.

Hakuna anayejiuliza, kupiga kura kwa jambo lile lile lisolo na matokeo tofauti lipo tatizo! Hawajiulizi
Leo tuna wagombea wakitangaza nia zao.

Hakuna hata mmoja aliyetoka nje ya mfumo ule wa miaka 50 uliotufikisha hapa.

Wote ni wajumbe wa kamati kuu, NECm Wabunge na mawaziri hadi mawaziri wakuu.

Ni sehemu ya mfumo ule ule. Bado wananchi wanahemka utadhani wamepata tangazo la kufutwa kwa kifo kutoka kwa mungu.

Wamesahau kuwa Chui hawezi kutoka katika zizi (zoo) akageuka kuwa Mbuzi

Hakuna anayejiuliza kwanini tunafanya yale yale kwa miaka 50 na hatubadiliki?

Hakuna anayeangalia kaskazini kwa wenzetu, wala kusini kwa Wazambia.

Tumebaki kupokea kauli tamu tamu.
Tunaambiwa X anachukia umasikini, hatuelezwi alikuwaje tajiri.

Tunaambia kwaheri umasikini akichaguliwa X, ambaye kwa miaka 30 amekuwa sehemu iliyozaa umasikini.

Hatukubali kazi ya miaka 30 ingeshamaliza umasikini, tuna kumbatia miaka 5, umasikini utafikia tamati.
Watanzania wameshasahau, ndivyo walivyo!

Tumeona Wabunge katika nyakati tofauti. Mambo mazito ya kitaifa wamejificha nyuma ya pazia la msimamo wa chama. Msimamo wa mabepari , mafisadi na waporaji ndio msimamo wao.

Hakuna aliyeonyesha kuchukizwa na rushwa, umasikini, mipango mibaya n.k. Wamejificha nyuma ya chama kisicho chao.

Wamekubali misimamo ya kifisadi kuwa yao.Hao hao wanarudi kuweka malengo yao nje ya chama wachaguliwe Wabunge au Rais. Wanaeleza kuchukizwa sana na huduma hafifu za elimu na afya, umasikini na rushwa.

Kwa miaka 10 walikuwa kimya nyuma ya chama, leo wanakuja na kauli kana kwamba wamezaliwa upya na hawakuwa sehemu ya uozo tunaoishi nao.

Wametumikia mfumo wa uozo uliopo kwa utiifu na unyenyekevu, kwa ulaghai wanakuja na mbinu za kuukana.

Walikuwemo ndani wakivuta allowance, leo wanatuaminisha si wao , ilikuwa mizimu inayofanana nao.
Wao wanachukia rushwa, umasikini na ujinga!

Bado tunaamini fisi anaweza kuwa mwema kwavile ameomba kazi ya ulinzi wa bucha yetu

Inaendelea...
 
SEHEMU YAVII


WANANCHIMUNGU KAWAPA FIMBO, ZITUMIENI KUADHIBU WALAGHAI
BADILISHENIMFUMO WA ULAGHAI, CHUKUENI HATMA YA NCHI

CCMwanatambua uchaguzi utakuwa na matokeo katika mtazamo huu

1 CCM kupoteza 2/3 ndani ya bunge kwa kupoteza Wabunge wengi


2Kupoteza umiliki wa Bunge kabisa na CCM kuwa chama cha upinzani

3 Kupoteza dola

4 Kupata dola, na kupoteza bunge au kupata bunge na kupoteza dola

Hizi ninadharia kutokana na hali ya kisiasa nchini.
Ukweli, mteremeko wa CCM kuanza kupanga nafasi sasa ni historia.


WAANACHIWANA KAZI MOJA

Wabungewanajulikana kwa historia, utendaji na uzembe . Waliosimama nyuma ya vyama badala ya taifa,waadhibiwe

Mbunge anayetaka nafasi aeleze vision yake na jinsi gani ataitekeleza kwa namba, tawimu na hoja. Sio
kusema
‘nitawaletea maendeleo''.



URAIS
Ni suala la taifa. Historia, kumbukumbu, kauli, matendo, na utendaji wa wagombea viwekwehadharani .
Waulizeni, nini watafanya, kwa njia gani na kutumia rasilimali zipi.

Sio kusema Fulani ana maamuzi magumu, atamaliza umasikini. Si sualala kusikiliza wapiga debe au bendera za vyama

Hatuwezikuwa na Rais asiyejua kwanini sisi ni masikini, anayeshiriki wizi na ufisadi akituaminisha wema siku za baadaye. Rais anayetiliwa shaka uadilifu wak, wala tusiyejua anasimamia nini, kwa nini na kwa njia gani.

Wananchi wasikubali kuwasikiliza wagombe wanaorodhesha matatizo.
Mfano, atakuza elimu, kilimo kwanza, anakerwa na umasikini, atapambana na ufisadi na uhalifu!


Hapana,matatizo tunayajua na hatuhitaji watu wa kuorodhesha tena.
Tunahitaji watu watakaotueleza matatizo yanatatuliwa kwa kutumia njia na rasilimali gani.


WaulizeniWabunge, nini wamefanya miaka 5 iliyopita katika majimbo.

Pesa za mfuko wa jimbo zimetumikaje hadi senti ya mwisho. Miaka 5 iliyopita ni kipi kipya mbungealibuni.

Mbunge amewakilisha vipi wananchi na si chama chake.
Amesimamia vipi ahadi, ngapi ametekeleza na ngapi hakutekeleza


Msikubali kuambiwa hakuna fungu. Waulizeni, mbona fungu la kiinua mgongo limepatikana mwezi wa saba bunge lilipovunjwa? Msiowaone haya, kama hawana majibu msihangaike nao weka pembeni songa mbele

Tumeona wagombea wa CCM wakiorodhesha matatizo yetu.

Tutawajadili mmoja baada ya mwingine bila kumuonea au kumhurumia.


Kwa sasatuwaangalie wapinzani

Inaendelea..
 
VYAMA VYA UPINZANI

BILAKUONYESHA NJIA NANI ATAWAAMINI?

Nyerere aliposema wananchi watayatafuta mabadiliko nje ya CCM wakiyakosa CCM alimaanisha wananchi wana kiu ya mabadiliko.

Kama
hawataona mbadala ni rahisi kusema Zimwi likujualo halikuli likakwisha


Hali ya kisiasa inaelemea sana CCM kama tulivyojadili hapo juu. Hata hivyo,siasa ni kitu kinachoweza kubadilika siku moja.

Mwanasiasa
mmoja wa Uingereza alisema maisha ya kisiasa kwa siku moja ni marefu sana.


Kule Marekani uchaguzi uliopita kura za maoni zilitabiri ukaribu sana kati ya Obama na Romney katika tofauti ya viti3 au 4(close to call) Matokeo yalipotoka Obama alishindakwa Zaidi ya viti 20

Uingereza,kura za maoni zilionyesha chama cha Labor kikiwa karibu sana na Conservative.
Matokeo yameonyesha
Labor wamepoteza vibaya sana tofauti na ilivyofikiriwa


Chama cha upinzani cha Democrat kilichounda serikalin na Conservative kimepoteza na kuwa cha 4 bungeni.

Chama cha SNP kimekuwa
cha tatu katika bunge.
Haya
yote nikuonyesha kuwa wananchi wanaweza kubadili mitizamo wakati wowote matarajio yao yasipofikiwa


Matarajio ni kuongoza, kuonyesha njia na kutia matumani(hope)

Wapinzani waTanzania wasibweteke kwa kudhani hali tete ndani ya CCM itawapa fursa.

Wapinzani wana wajibu wa kuwahakikishia wananchi , wapo tayari kuongoza kwa kuonyesha njiasi kuongoza nyuma ya CCM.

HALI YA UPINZANI

Kusahihisha makosa ya kuvurugana siku za nyuma hakutoshi.

Ndio, wapinzani wameunda
UKAWA ilikupunguza mivutano kati yao na kukabiliana na CCM.

Tunajua chaguzi
zilizopita na hata zaserikaliza mitaa, CCM iliweza kushinda pale palipokuwa na upinzani mkali kati ya wapinzani wenyewe. CCM ilishinda kwa kura 40 au 100 wakati wapinzani wakiwa na maelefu waliyogawana.


UKAWA

Ukawa imeanzishwa wakati wa bungela katiba. Ni mpango uliotokana na haja ya wakati.

Pamoja
na hayo, fursa hiyo ikatumika kusahihisha makosa. Hata hivyo, ni ukweli kuwa UKAWA imeundwa katika mtindo wajuu kwenda chini( top to bottom) na siyo bottom -top


Ujenzi wa taasisi katika njia hiyo unachangamoto kama tahadhari haitachukuliwa.

Moja ya changamoto ni kuwa ‘vulnerable' kwasababu wengi ambao wako chini hawaelewi kwa undani dhana nzima na hivyo migogoro itaanzia huko kwenda juu ( bottom to top)

Kwanini kunatatizo kubwa ukawa?

Tutajadili sehemu ya mwisho ili tuweze kusemezana

Inaendelea…
 
UKAWA

Tumeeleza jinsi ulivyoanza na changamoto kubwa ambayo ni ‘vulnerability' kwasababu ya kutojengwa kutoka chini kwenda juu bali juu kwenda chini.

Mfumo wa top to bottom ni kama ‘commanding' ya majeshini. Kwamba, wakubwa wamesema, hoja hutiririka hadi chini.
Obama. katika kinyang'anyiro cha Urais, alikuwa seneta mdogo asiye na jina .Alijenga kampeni kuanzisha chini

Aliweza kuwashinda akina Hillary wenye mitando tayari,Mcain wenye majina

UKAWA kwavile wanajenga kutoka juu wanatakiwa wahakikishe walichokusudia kinawafikia walio chini.

CCM haijisikii vema na uwepo wa UKAWA,wanaweza kutumia ngazi za chini kuchochea vurugu.

Haionekani kama viongozi wa UKAWA wanaiona hatari hiyo, wameridhika, umoja wao ni imara.

Hawajishugulisha kwenda chini kutoa elimu kwanini UKAWA, wamelenga nini na kwa sababu zipi

UKAWA NA ''VISION''
Kenya waliungana kuhakikisha KANU inaanguka ili kutoa nafasi ya mageuzi.
Wamefanikiwa . Zambia walihakikisha UNIP inavunjwa mgongo, wamefanikiwa

Huko kote haikuwa na maana ya kuungana kisera,ni kuungana kuondoa ubabe ilikuwe na fursa sawa.
Ndivyo UKAWA ilivyo kwa sasa


UKAWA haina sera wa malengo sawa ya kisiasa. Ni muungano utakaohakikisha, kwanza CCM inavunjwa mgongo ili kufanya mabadiliko.

Bunge la katiba ni mfano mzuri kuwa CCM inapigika.

Waliweza si kwasababu wana sera na itikadi sawa, bali wana kundi linalowaunga mkono(wananchi)
Hivyo Lengo la UKAWA, ni nguvu ya pamoja kufumua mfumo uiopo sasa hivi
 
PLAN A1 NA PLAN A2

Lengo la ukawa ni plan mbili A1 na A2 na siyo A na B

Kwanza, kushika dola (A1) na pili kudhibiti bunge (A2) na siyo Plan A kushika dola na Plan B kudhibiti bunge.

Unapokuwa na plan A na B ni dalili ya kukata tama. Ni lazima kuwe na plan A1 na A2 kwa pamoja


NAFASI WALIYO NAYO UKAWA
1 Wananchi wanawaunga mkono kwa kile wanachokiona, uhuni wa CCM kutumia serikali na Bunge kwa agenda zao.

2 Ukawa wana hoja zinazojieleza, kwamba wananchi hawahitaji tena kuelezwa ufisadi, mabomu ya ufisadi, wizi au ufujaji

3 Kazi kubwa ya wabunge wa upinzani ina wapa nguvu ya kujenga hoja ya kupewa wingi zaidi

4 Hawana makando kando kama waliyo nayo CCM zikiwemo historia na misimamo iliyokwenda kinyume na wananchi

5 Wanaonekana kama mbadala baada ya wananchi kuchoshwa na uhuni wa CCM

MATATIZO YANAYOIKABILI UKAWA

1 Hadi sasa hawajaelewa wanakwenda kwa wananchi wakiwa na ujumbe gani wa pamoja na si wa vyama vyao.

2 Hawana campaign slogan ya pamoja ya kuhamasisha, kujenga matumaini na kufikisha ujumbe.
Hivi hili linahitaji fedha kweli?

3 Hawajaweza kueleza wanachi, nchi hii watafanya nini kwa njia na rasilimali gani. Kuna mapungufu gani, watayarekebisha vipi na kwasababu zipi

4 Hawajaweza ku address matatizo ya wananchi kwa kueleza vipau mbele vyao, na kwanini vipau mbele hivyo na wanavishughulikiaje na kwa njia gani

5 Hawajaweza kuonyesha wananchi kwanini CCM imeshindwa, na kwanini wananchi watashindwa iwapo wataendelea kuikumbatia CCM

6 Hana mkakati wa kuhamasisha uandikishaji, na kuhakikisha watu wanapiga kura

7 Wana tatizo la tume ya uchaguzi ambalo hawalioni kama ni mwiba kwao


Itaendelea sehemu ya mwisho
 
MTAZAMO WA JUMLA

Upo umuhimu wa kuwaeleza wananchi umuhimu wa uchaguzi na athari za khanga na kofia za siku.
Kuwaamsha watambue wanaowachagua si viongozi wa vyama ni wa nchi.

Wananchi wafahamishwe, muda wa wagombea 'kuleta maendeleo nchini au jimboni' umepitwa na wakati.
Maendeleo ni zoezi linaloshirika wananchi, wabunge au Rais ni kiungo.

Wagombea hawana makontena ya maendeleo bandarini.
Wanachotakiwa kueleza ni matatizo waliyo nayo wananchi na watayatatua vipi.

Tumeona wagombea wa CCM wakiorodhesha matatizo ya wananchi, wanayajua kwasababu walikuwa ndani ya mfumo huo wengine kwa miaka 40. Hatutarajii kusikia wakiimba nyimbo za elimu, umasikini, afya n.k.Tunajua hayo ni matatizo yaliyopo nchini siku zote.

Tunataka kuwasikia wakitumia takwimu, vielelezo na namba kutoa suluhu za matatizo yetu.
Miaka 50 ni nchi masikini, watueleza kwanini ni masikini na wanadhani kwa kutumia rasilimali gani ,zinazotoka wapi tunaweza kuondoka kundi hilo

Tunataka kuwasikia wakitueleza, kwanini miaka 50 bajeti ya nchi asilimia 40 ni wafadhili.
Tunafanya nini kuondokana na ufadhili unaouza uhuru wetu na kutufanya dhalili kila tunapotembea duniani

Tunataka watueleze, mmomonyoko wa maadili katika jamii chanzo chake ni nini.
Mivutano ya kidini iliyopo na hii inayozuka ya kikanda chanzo chake nini, watafanya nini kurejesha umoja na mshikamano wa kitaifa. Hatutaki kuwasikia wakilipa masheikh na maaskofu kuwasadia katika kampeni. Tunataka suluhu ya tatizo

Tunataka watueleza, wakisema wanamaliza umasikini, ni kwa hesabu gani, kutoka rasilimali zipi na kwa njia zipi.
Hatutegemei utajiri wao wataugawa kwa wananchi. Tunataka tuone kwa namna jinsi wanavyomalaiza umasiki

Tunataka kuwasikia, wanakbailiana vipi na tatizo la rushwa, ufisadi. Hatutaki kusikia wakilaani maana wanaishi nao kila siku

Tunataka kuwasiki, wakisema wanaendeleza jimbo, ni kwa rasilimali zipi, utaratibu gani na kwa vipi.

Hatutaki wajenge madaraja na shule kwa pesa zao. Hatutaki walete ambulance kwa pesa zao, tunataka tuone sisi kama wananchi tunapangaje, tunachagua vipi na tunatekeleza vipi wao wakiwa viungo.

Kampeni za kuorodhesha matatizo ya wananchi ni za kipuuzi za watu waioijua nchi hii.

Hata wale wanaoijua kama waziri mmoja aliyepo madarakani anayegombea, ambaye miaka 40 yupo serikali, bado hana cha kutuambia, anatuorodheshea matatizo tena kama waziri wa sera na mipango

Kampeni zetu zibadilike, tunataka uhalisia. Mtu akisema atafanya ABC atuonyeshe, hatutaki 'lip service'' miaka 50 inatosha.

Tunataka kama anaongelea uchumi aweke namba, takwimu, vielelezo na ushahidi na si kutuambia atachukua mirahaba ya madini wakati hajui hata madini yaliyopo nchini

Wananchi wachague watu kutokana na mitazamo yao ya kuendeleza taifa na si vyama vyao.

Ukimuona mtu anakuja na ilani au sera za chama ujue hajui tatizo la jimbo lako, hajui tatizo la nchi yako, amebeba makabrasha ili kukuibia tu aendele kulala Dodoma.

Kataeni matapeli hawa wawe wa CCM au Upinzani. Ni matapeli tu waambie wabebe sera warudi nazo kwenye vyama vyao.

Tunataka kiongozi anayeeleza sera zinazoendeana na mazingira aliyosimama
 
VYAMA VYA SIASA

CCM imetawala miaka 50. Wananchi wanatarajia majibu na si orodha ya matatizo.

Hali ya kisiasa ndani ya chama ni tete, na hilo huenda likasaidia sana kutueleza uozo ulivyotamalaki.
Hata hivyo Wapinzani lazima wasimame na kuonyesha mbadala halisi. Lazima wasimame na kuongoza

Hadi leo hii wapinzani wanaonekana kutojua hasa nini wafanye miezi 3 iliyobaki.

Wanasubiri kuanza kukimbizana na CCM.
Wasichokijua ni kuwa hawana resource. Wakuu wa Wilaya na Mikoa ni makada wa CCM wanaotumia rasilimali kusaidia CCM.

Kuisubiri CCM ni kutaka kukimbazana na mtu mwenye Jet wakati una kibajaji

Wapinzani waende kwa wananchi wakiwa na ''substance'' na si mabomu ya ufisadi.

Wananchi wanajua nchi imeoza na inanuka, si rushwa bali kila aina ya uovu unaojulikana. Wanatakiwa kukumbushwa tu

Mfano, juzi kampuni maarufu ya simu imkwepa kodi kwa kuhapisha vocha feki.

Mkurugenzi wake kahamishwa ili kufunika kombe. Pesa hizo ndizo zinatumika kuandaa mikutano ya nia ya kugombea tunayoina.
Hilo linajulikana, waeleze wananchi bilioni 320 zilitosha kufanya nini kwao.

Waelezeni kwa takwimu za kiuchumi, jinsi gani uozo kama wa Richmond unavyokula bajeti ya nyumba ya kila mtu hadi leo.

Na jinsi gani uozo huo unavyotumika kuwanunua leo hii kwa sh 10,000

Waeleze nini mtafanya mbadala kuzuai uozo huo, kwa rasilimali zipi na lini. Tumieni uozo kama chombo cha kubeba ujumbe wenu na si kutumia uozo kama agenda yenyewe.

Na mwisho, wananchi tukumbuke kauli ya Nyerere. Ikulu ni mahali patakatifu, ukiona mtu anataka kwenda kwa pesa jiulize kuna biashara gani huko. Ikulu ni sehemu ya kuogopwa, na wapogopeni kama ukoma wanaoitamani.


TUSEMEZANE wanajamvi
 
TUANGALIE TULIYOJADILI KWA UHALISIA
SUMAYE ATANGAZA NIA

ASEMA ‘WAZIRI MKUU' SIYO SERIKALI. MLARUSHWA ANAKAMATWA NA SERIKALI!
Moja ya maswali aliyoulizwa ni kuhusu ubinafsishaji wa NBC n.k.

Jibu la Sumaye, hiyo ilikuwa sera, serikali ya Mkapa akiwa waziri mkuu waliikuta hivyo wasilaumiwe

Hoja yetu
Kiongozi wa namna hii anasikitisha sana. Kwamba, alikuta madudu na kuamua kuyaendeleza. Huyu wakati anaomba kura kuwa Mbunge na wakati anaapa kuilinda katiba ya nchi aliyasema hayo kwa moyo wake.

Leo anakana kuwa yeye alikuta. Kwa lugha nyingine anakwepa kuwa responsible na kitu alichosimamia.
Huu kama si udanganyifu ni kitu gani.

Swali la 2
Kuhusu ununuzi wa Radar kwa njia za Rushwa
Jibu la Sumaye: Nchi haikuwa na Radar, kama kulikuwa na rushwa anayehusika ni serikali na si Sumaye

Hoja yetu: Huyu ni waziri mkuu anayesema ‘inayohusika ni serikali'' Hapa ana maana yeye hakuhusika. Hata hivyo katiba inamhusisha, ubunge unamhusisha na Uwaziri mkuu unamhusisha.

Anakwepa Lawama ili tuamini kulikuwa na waziri mkuu mwingine

Kwa lugha nyingine, Mkapa ndiye serikali yeye alikuwa waziri mkuu

Mtu kama huyu ni wa kuogopa sana, maana hayupo tayari kuwajibika.

Tutaendelea kuchambua kauli zao mmoja mmoja bila huruma wala kuonea
 
SUMAYENA JIBU JEPESI

Katika mkutano wa kutangaza nia, Waziri mkuu mstaafukaulizwa

Kuna tuhuma nyingi za yeye kuchukua ardhi kubwa kwakutumia nafasi yake

Jibu la Sumaye:
Kuna Watanzania wenye ardhi kubwa kulikoyeye.
Gharama za kujenga nyumba Dar zinaweza kununua shamba kubwa mikoani


Hoja yetu:
Swali halimuulizi hivyo, anachotakiwa kujibu nituhuma za kunyang'anya watu ardhi, kupata ardhi kwa kutumia jina la PM .


Hakuna anayetaka kujua ana ekari ngapi na wala haziwezi kufananishwa na za mtu mwingine.


Hawa wanaokwepa maswali hivi ndio wanataka kuondoa umasikini!

Tusemezane
 
TUANGALIE TULIYOJADILI KWA UHALISIA
SUMAYE ATANGAZA NIA

ASEMA ‘WAZIRI MKUU’ SIYO SERIKALI. MLARUSHWA ANAKAMATWA NA SERIKALI!
Moja ya maswali aliyoulizwa ni kuhusu ubinafsishaji wa NBC n.k.

Jibu la Sumaye, hiyo ilikuwa sera, serikali ya Mkapa akiwa waziri mkuu waliikuta hivyo wasilaumiwe

Hoja yetu
Kiongozi wa namna hii anasikitisha sana. Kwamba, alikuta madudu na kuamua kuyaendeleza. Huyu wakati anaomba kura kuwa Mbunge na wakati anaapa kuilinda katiba ya nchi aliyasema hayo kwa moyo wake.

Leo anakana kuwa yeye alikuta. Kwa lugha nyingine anakwepa kuwa responsible na kitu alichosimamia.
Huu kama si udanganyifu ni kitu gani.

Swali la 2
Kuhusu ununuzi wa Radar kwa njia za Rushwa
Jibu la Sumaye: Nchi haikuwa na Radar, kama kulikuwa na rushwa anayehusika ni serikali na si Sumaye

Hoja yetu: Huyu ni waziri mkuu anayesema ‘inayohusika ni serikali’’ Hapa ana maana yeye hakuhusika. Hata hivyo katiba inamhusisha, ubunge unamhusisha na Uwaziri mkuu unamhusisha.

Anakwepa Lawama ili tuamini kulikuwa na waziri mkuu mwingine

Kwa lugha nyingine, Mkapa ndiye serikali yeye alikuwa waziri mkuu

Mtu kama huyu ni wa kuogopa sana, maana hayupo tayari kuwajibika.

Tutaendelea kuchambua kauli zao mmoja mmoja bila huruma wala kuonea

Mkuu nakumbuka huyu jamaa alisema kama uchumi wakati wa mkapa ulienda vizuri basi yeye ndio alikuwa msimamizi wa utekelezaji wa sera za uchumi, na anastahili kuchaguliwa kuwa rais, kwa hiyo alikuwa proud na matokeo ya sera zile, leo kuanza kukataa sielewi maana yake nini.

Lakini nakumbuka pia alisema kuwa baada ya kukosa uteuzi wakati JK anaingia Madarakani alisema anaenda Marekani na hata jishughulisha tena na kugombea urais, ingekuwa vizuri akieleza kwanini amebadilisha uamuzi. waadhishi wamekosea sana kuacha kumuuliza swali hilo.
 
SUMAYENA JIBU JEPESI

Katika mkutano wa kutangaza nia, Waziri mkuu mstaafukaulizwa

Kuna tuhuma nyingi za yeye kuchukua ardhi kubwa kwakutumia nafasi yake

Jibu la Sumaye:
Kuna Watanzania wenye ardhi kubwa kulikoyeye.
Gharama za kujenga nyumba Dar zinaweza kununua shamba kubwa mikoani


Hoja yetu:
Swali halimuulizi hivyo, anachotakiwa kujibu nituhuma za kunyang’anya watu ardhi, kupata ardhi kwa kutumia jina la PM .


Hakuna anayetaka kujua ana ekari ngapi na wala haziwezi kufananishwa na za mtu mwingine.


Hawa wanaokwepa maswali hivi ndio wanataka kuondoa umasikini!

Tusemezane
Majibu mengine ya Sumaye haya hapa.


Kwanza kama waziri mkuu naweza kumshauri wa rais, Ameziita kashfa lakini mimi siziiti kashfa. Kama NBC ni ubinafsishaji wa kawaida. Sijui watu wanatoa wapi taarifa kuwa walikuwa wanapata faida, regulator wa benki zote ni BOT hivyo ndio ana taarifa sahihi. Hakuna kwamba tuliuziana benki hotelini Hizo zingine zote zinafanana, Radar na ndege ya rais, unatakiwa utofautishe maamuzi ya serikali na kama kuna ufisadi, nchi ilikuwa haina radar. Katika ununuzi ule kama kuna mtu alifanya foul anatakiwa akamatwe, ilimradi imethibitika mtu alifanya ovyo ni jukumu la serikali kumkamata sio Sumaye,
 
Tanzania hatuna upinzani wa kuweza kuwasaidia watanzania kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine. Wapinzani wangekuwa na nia ya dhati wangejiunga na umoja wao kama vyama vilivyounda UKAWA na kuhakikisha wanaisimamia serikali kuandikisha watu wote wenye vigezo vya kupiga kura. Hii ingewasaidia sana kuitoa CCM madarakani. Wasimamie zoezi zima la kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo.

Nguvu ya umma.
Watanzania ni waoga na wasahaulifu sana. Ukiangalia toka JKikwete aingie madarakani hadi leo madudu mengi yamefanyika, kuna ufisadi wa wazi sana na hadi waziri mkuu kujiuzulu. Lakini sisi tumesahau kiasi kwamba huyo waziri mkuu tunamuona amegeuka lulu.

Maswala nyeti yanayohusu maslahi ya taifa tunayasahau sana. Watu wanaendelea na shughuli zao kana kwamba hayawahusu kumbe wao ndo wahanga wakuu wakubwa.

Binafsi naona dhahiri kuwa ukombozi tunaoudhania utatokea 2015 hautatokea kwasababu wananchi hatujatambua nguvu tulionayo.
 
Back
Top Bottom